SCENE 39: -
(Usiku mwingine, Raymond amejipumzisha katika bustani yake nzuri iliyopo
mbele ya nyumba yake huku mchumba wake ambae alikuwa msichana wake wa kazi yupo
jikoni anaandaa chakula cha usiku)
Raymond:(anachukua
simu yake kisha anampigia Angelina aliopo jikoni)
(simu inaita)
Angelina:(anaipokea) dear...
Raymond: hujamaliza kupika tu jamani? mimi nimekaa peke
yangu nasikia upweke…jamani
Angelina:(anacheka
kidogo) nameshamaliza kupika nasubiri maziwa yachemke, nikuletee
(maziwa yanachemka)
Raymond: fanya haraka bwana nataka kukaa na wewe…bwana
Angelina: haya nakuja (anakata simu kisha anamimina maziwa katika vikombe viwili vikubwa kisha
anatoka navyo na kuelekea alipo Raymond)
Raymond:(anamuona
kisha anampokea kikombe kimoja) asante kwa kuja…dear
Angelina:(anakaa
pembeni yake)
Raymond:(anamsogeza
karibu yake na kumkumbatia)
Angelina:(anacheka)
nini?
Raymond: kwani siruhisiwi kumkumbatia mchumba
wangu?
Angelina:(anacheka
sana) jamani…unaruhusiwa
Raymond: sijui ulikuwa wapi miaka yote…wewe ni
kiboko yangu
Angelina: hata wewe ni kiboko yangu…
Raymond: nakupenda sana Angelina wangu
Angelina:
nakupenda pia Raymond…
Raymond: Mungu atusaidie tuzae watoto mapacha
Angelina:(anacheka)
yaani wewe… unahisi nina mimba
Raymond:(huku
anacheka) inamaana hujapata tu mimba…?
Angelina: hapana sijapata mimba
Raymond: bahati yangu mbaya mwenzenu…
Angelina: nitabeba tu tukishaoana
Raymond: nitakuoa uleule mwezi tuliopanga mara ya
mwisho wakati nataka kumuoa Christina…nitabadilisha tu bibi harusi
(Wanacheka)
Angelina: yaani unajua siamini
Raymond: huamini nini?
Angelina: baba yako amekubali jamani
Raymond: ndo hivyo hata hivyo Mungu alipanga tu Mimi
na wewe tuoane kwahiyo amini tu kwamba tunatarajia kuoana
Angaelina:(anacheka
kidogo)
Raymond: hukujua tu
Angelina: kujua nini?
Raymond: ungenipa mapema sasa hivi ungekuwa
umeshakuwa mke(anacheka)
Angelina: Ha!!kwa hiyo Raymond ile siku ndo
imekufanya unichumbie?
Raymond: sasa je si nikapagawa?
Angelina:(anashangaa)
Raymond:(anacheka
sana)
Angelina: makubwa basi…kwahiyo nisingelala na wewe
usingefikiria kunioa?
Raymond: nakutania mke wangu…nilipanga kukuoa tangu
kipindi naanza kukupenda wewe ni wa tofauti sana…una akili nikikuweka ndani
tunajenga nyumba hizi Zaidi na Zaidi au unajifanya?
Angelina:(anaguna)
kwahiyo nijifanye siku zote za maisha yangu?
Raymond: nakutania…una hasira wewe…
Angelina:(amenuna)
Raymond: basi mama…tema mate tumpige
Ray…amekuchokoza ee…haya (anakinga mkono
mdomo kwa Angelina) tema mate mama…tumchape
Angelina:(bado
kanuna)
Raymond: tema usiogope urefu wake…tema tumkate
makofi Raymond
Angelina:(anajikuta
anacheka sana) yaani wewe
Raymond:(anacheka
pia) sipendi kukuona unanuna wewe…kwakweli basi tu
Angelina: mbona unapenda kuniudhi?
Raymond:si kawaida…mimi unajua sasa hivi ndo mwanao
eeh wa kwanza
Angelina: He!!! Yaani niwe na litoto likubwa hivi?
lina mandevu makubwa hivi…
Raymond: ndo lizuri…linakuwa linakutetea hilo lenye
mandevu mengi
Angelina:(anacheka
kidogo)
Raymond:(anacheka
sana halafu anaacha kucheka ghafla, anamuangalia Angelina kwa muda)
Angelina: nini?
Raymond: wewe Mrembo…sana, nina bahati kukupata
wewe
Angelina: mimi ndo nimepata bahati ya kukupata wewe
mpenzi wangu
Raymond: Edmond alichelewa sana kukuleta
Angelina:(anatabasamu)
wakati wetu ulikuwa haujafika
Raymond: nina furahi kuwa muda wetu umefika mpenzi
Angelina: nina furahi kuwa na wewe
Raymond: mimi Zaidi Angelina wangu…
Angelina: hivi kwanini ulinipenda mimi?
Raymond: swali gumu sana maana hata mimi sijui kwanini
nilikupenda mpenzi wangu, ilitokea tu mimi na wewe tukawa hivi, pamoja na
kwamba nilijitahidi kuzuia hisia zangu kwako ila moyo ukalemewa
Angelina: naupenda sana moyo wako
Raymond :(
anatabasamu)
Angelina: wewe kweli ni mume mwema
Raymond: hata wewe ni mke mwema
Angelina :(
anacheka)
Raymond: weekend hii naomba tutoke nje ya mji
Angelina: tutaenda wapi?
Raymond: Serengeti mpenzi wangu
Angelina: kwenye mbuga za wanyama?
Raymond: ndio, au utakuwa na kazi
Angelina: nyingi sana
(wanacheka)
Raymond: twende bwana tukatulize mawazo bwana
Angelina: sawa tutaenda
Raymond: (anambusu)
0 Comments