SCENE 40: -
(Asubuhi
nyingine ya siku nyingine tena, Ramadhani yupo chumba kidogo kilichowekwa kwa
ajili ya mlinzi, anaonekana ana mawazo sana)
Ramadhani: yaani sina hela halafu boss yupo busy
kweli hata hanisikilizi tena jamani…mara aniambie nimsubiri atanipa jioni…jioni
penyewe mbali na mama yangu kijijini anaumwa sana wanataka kumpeleka hospitali
nitafanyaje sasa (anachukua simu yake
anapekua majina) ngoja niangalie mtu ambae anaweza kunikopesha kwa muda
jioni boss akinipa nitamrudishia (anaona
jina la Christina) sijui nahangaika nini huku bank hii hapa ngoja(anampigia)
(Simu inaita)
Christina :(bado
amelala kwahiyo haisikii)
Ramadhani: ah hili nalo ndo maana halijaolewa si
cha ajabu bado limelala, (anapiga tena)
(Simu inaita)
Christina :( anashtuka)
nini? (anapokea)hello
Ramadhani: shemela langu la ukweli hilo
Christina: nini…asubuhi asubuhi
Ramadhani: nimekumisi mie jamani uko wapi?
Christina: bwana ee(anafyonza)sema shida yako haraka mimi nina usingizi bwana
Ramadhani: duh…shemela saa nne hii bado una
usingizi wewe noma…ila nakukubali…mwana
Christina: unataka nini?
Ramadhani: mama anaumwa
Christina: kwahiyo?
Ramadhani: naomba unisaidie mwanangu
Christina: hapo nikusaidia utanipa nini Mimi?
Ramadhani :( anacheka
kidogo) kama kawaida nitakupa yaliyojiri wiki hii…
Christina :( anakaa maana alikuwa amelala) unataka sh.
ngapi?
Ram adhani: elfu hamsini tu
Christina: niambie kwanza
Ramadhani: Raymond kamvalisha Pete ya uchumba Angelina
Christina :( anashangaa
sana) eti nini?
Ramadhani :( anashangaa)
inamaana ulikuwa hujui au unajifanyisha?
Christina: hivi Raymond ana kichaa huyu mwanaume,
si alitakiwa anioe mimi? yaani kanivalisha pete ya uchumba halafu kaniacha
solemba kaenda kumvalisha pete ya uchumba huyu mwanamke ambae haeleweki…ngoja
niongee na baba yake...
Ramadhani: umechelewa Sana mama…baba mtu
amekubali…waoane na mipango ya kwenda nyumbani kwa kina Angelina imeanza
kupangwa tena kwa siri wanataka kumpa surprise Angelina
Christina :(
anasikitika sana) jamani huyu mwanamme ndo wakunifanyia mimi hivi?
Ramadhani: mapenzi mubashara nakwambia hapa tu kila
jioni wanakaa bustanini watashikana weeeee mpaka sisi huku tunaomba po!!Yaani
ndugu yangu na hapa analetwa mfanya kazi mwingine huyu keshakuwa maza hausi
sijui upo? haya leta hamsini yangu
Christina: nakutumia
Ramadhani: nasubiri (anakata simu)
Christina:(huku
anatetemeka, anaenda kwenye menyu ya mpesa na kuanza kutuma pesa kwenda namba
ya Ramadhani) Mungu siamini mimi leo nimewakosa baba na mtoto nani tena
atanipa pesa? pesa jamani ndo byebye loh!!!!Wamenikomesha jamani wanaume
wanajua kukomoa hawa jamani (anamaliza
kutuma)
(Meseji inaingia kwenye simu ya Ramadhani)
Ramadhani :( anaangalia)
mpesa imethibitishwa… (Anacheka) kumbe
umbea nao kazi eeh (anabusu simu yake)
haya bwana…ngoja niwatumie mie, embu ngoja nimshukuru (anapiga simu ya Christina)
(Simu ya Christina inaita tena)
Christina :( anapokea)
umepata?
Ramadhani: ndio Asante
Christina: utaendelea kuniambia
Ramadhani: poa (anakata
simu)
Christina:(ananyanyuka
kisha anaenda mbele ya kioo kikubwa kilichopo chumbani humo) kwani mimi
nina kasoro gani mpaka Raymond asinipende mimi na kunioa? kaona nini kwa huyo
msichana wa kazi za nyumbani ambacho hakuona kwangu?
(shangazi
yake anakuja)
Shangazi: wee mtoto
Christina:(anashtuka)
Shangazi: vipi mbona unaongea peke yako?
Christina: sijui kwanini ila najiona nimeshindwa
Shangazi: umeshindwa na nini?
Christina: nimeshindwa maisha
Shangazi: kivipi?
Christina: baba na mtoto wote hawanitaki
Shangazi:(anashangaa kidogo)
yamekuwa hayo tena?
Christina: acha tu shangazi…yaani huyo mzee hapokei
hata simu zangu na mtoto mtu sasa nasikia kamvalisha pete ya uchumba yule
kijakazi
Shangazi:(anashangaa
sana) eh makubwa (anakaa kitandani)
Christina:(anaguna
kisha anakaa kitandani pia) sijui huyo kinyago kampa nini Raymond mpaka
kaamua maamuzi makubwa ndani ya muda mfupi hivi?
Shangazi:(anashangaa
sana)
Christina:(machozi
yanamlenga) yaani Raymond nimehangaika nae miaka mingi leo hii anakuja
kuniacha mimi na kutaka kuoa mwanamke mwingine…nimemvumilia mangapi leo anakuja
kuniacha na kutaka kuoa mwanamke mwingine…kwakweli (anafuta machozi) siwezi kukubali…Raymond ni mume wangu namtaka…na
ninamtaka baba yake pia maana alikuwa ananipa pesa za kutosha aliuwa ananisaidia
sana
Shangazi:(anavuta
pumzi ndefu kidogo) Christina mimi naona sasa uwaache…kiukweli naona mambo
yamegoma
Christina: hakuna kilichogoma hapa shangazi…nitafanya
kila mbinu Raymond na baba yake warudi kwangu…mimi ndo mwenye mamlaka ya kuwa
na Raymond na baba yake na sio kinyago mwingine…utaona nitakachofanya hutaamini
Shangazi: kila mara ukipanga jambo Fulani
linakurudia vibaya kwanini mwanangu usiwe na Peter wako…? wenyewe mnapendana
hadi raha
Christina: namtaka Raymond na Bembele
Shangazi: Raymond ni wa Angelina na Bembele ni wa Glory
waache mwanangu…wewe ni wa Peter…
Christina:(anapandwa
na hasira) sitaki sasa na usinilazimishe niache kufanya haya…yote na
nahitaji msaada wako
Shangazi: wangu tena?
Christina: nipe namba ya yule mtu aliyetusaidia
mara ya kwanza…namuaminia
Shangazi: wewe Christina…unataka kuroga si uache
mwanangu jamani sio kwamba hauna mwanaume anayekupenda
Christina: taja namba huwezi usiniongeleshe tena
Shangazi:(anataja
namba)
Christina:(anaziandika
kisha anapiga)
Shangazi :(
anaondoka zake)
Christina:(anaonekana
amepandwa na hasira) sishindwi kitu mimi…mwisho wa mpambano mimi ndo
nitakuwa mshindi… (anatupa simu pembeni kwa hasira) mbona huyu nae hapokei simu
yangu (anapiga tena)
(Anaendelea kujaribu kupiga simu)
0 Comments