SCENE 5: -
(Christina
anafika nyumbani kwao akiwa anaonekana ana hasira sana juu ya kitu Fulani, anaingia
ndani bila kuwasalimia mama na shangazi yake anaelekea moja kwa moja mpaka
jikoni anafungua friji anatoa bia aina ya castle lite na kuanza kunywa huku
akirudi sebuleni)
Mama: sasa shoga yetu mbona umepita hapa hata
salamu kwani tumekukosea nini?
Christina: yaani acha tu mama yaani kichwa changu
kimevurugwa achene tu...
Shangazi: tatizo nini?
Christina: Raymond...
Mama: huyu mumeo mtarajiwa?
Christina: ndio…huyu huyu…mshenzi Sana huyu mtoto…ananipa
wakati mgumu
Shangazi: kafanyaje tena jamani mbona kelele Tu...
Christina :(
anakaa maana muda huo wote alikuwa amesimama)
Shangazi: tatizo nini shoga yangu?
Christina: hivi mnaweza kuamini kuwa Raymond leo
kanifanya nimpigie magoti…mimi Christina Damas ni wa kumnyenyekea mtu
mimi…kanidharirisha sana na ni lazima atalipa (anakunywa bia yake ambayo wakati wote alikuwa ameishika mkononi)
Mama: umempigia magoti kisa nini…?
Christina: aliniambia kuwa tuachane
Shangazi: hivi huyo mumeo ana akili timamu? Miezi
miwili imebaki mfunge ndoa anaanza kuleta ushenzi wake
Mama: hata iweje haitawezekana hata siku moja Raymond
kumuacha Christina…yupo kiganjani mwetu hana ujanja acha tu ajipe moyo
(Wote
wanacheka kimbea)
Shangazi: ila hizi hela zitatutoa roho haki ya
Mungu loh!!
Mama: kwanza mama na baba yake hawawezi kukubali Raymond
aoe mke mwingine hiyo aibu ataificha wapi?
Shangazi: anajipa moyo tu (kimya kidogo) hivi shosti ile dawa niliyokupa uliioga vizuri
Christina: hata sijaioga
Shangazi: ioge…
Mama: halafu Ili kumkomesha beba mimba yake
Christina: nyie mnajua kabisa kuwa nampenda Peter
na kwa Raymond nachuna tu pesa nikale na Peter wangu
Shangazi: tunajua sana tu…ila njia ya kumkamata ni
kubeba tu ujauzito wake basi mambo mengine yatajipa
Christina: ngoja nitafikiria…
Mama: shoga yangu fikiria haraka haraka maana miezi
miwili sio mbali kesho kutwa tu mama
Christina: naelewa Sana tu na ondoa shaka kabisa
kila kitu kitakuwa sawa wala usijali...
(Simu ya Christina inaita)
Christina :( Kwa
sauti ya kimahaba) hello my love, nilikuwa nakufikiria, sasa hivi
Peter: kweli? (Anacheka
kidogo) nimekumisi Christina, mbona huji kuniona mpenzi wangu
Christina: nitakuja tu, honey wewe ondoa shaka
Peter: ok haina shida, uko wapi na unafanya nini
sasa hivi…
Christina: nipo nyumbani nipo tu sina cha kufanya
Peter: njoo kwangu sasa hivi
Christina: no, baby, nitakuja baadae tufanye usiku
nije nilale huko
Peter: ok hiyo iko vizuri Sana hapo sasa ndo
umenena, poa nitakuona baadae…
Christina :( anakata
simu yake)
Mama: mwenzangu umekufa umeoza kwa huyo Peter mtu
mwenyewe hana hata hela
Christina: hivyohivyo tu mama, sijali ananifikisha
napotaka
Shangazi: wacha weee…
(Wanacheka
kimbea)
Christina: sio huyo fala, mwaka wa sita sijawahi
hata kubeba mimba hata kwa bahati mbaya loh!!!
Shangazi :(
anacheka) hivi Raymond alikubamba na Peter eeh…
Christina: ndo maana yake yaani siku hiyo
walipigana kumbe na mimi mzuri ee yaani wanaume wawili tena wazuri wanapigana
kwa ajili yangu (anacheka)
Shangazi: yaani we chizi kweli
Mama; shoga yangu hukutupa michapo nakwambia Raymond
alikuja hapa kapaniki kuliko maelezo kweli ilimuuma
Christina: atajijua mwenyewe mi napenda tu
anavyonipa hela yaani Raymond hanifikishi yaani mshamba huyo
Shangazi: tatizo ulokole kila saa Yesu, Kha!!Hata
huyu Yesu jamani anachokwa kutajwa
(Wanacheka
tena kimbea)
Shangazi: ila tuache utani Raymond, mzuri huyo mtoto
duh!!Ningekuwa kijana ningejiweka hapo mazima…ana kifua unasemaje huwa
hakufikishi?
Mama: mlokole yule (anacheka) si cha ajabu huwa anaona dhambi kuzini
(Wanacheka
tena)
Christina: Kwa kifupi pamoja na uzuri, sijui
utajiri yaani hajiwezi kabisa mjinga yule
Shangazi: basi usimtukane
Christina: yaani Raymond kanichosha basi tu, yaani
hapa nataka anioe baada ya miezi kadhaa naenda kuomba talaka mahakamani
Mama: na umejipanga
Shangazi: kikubwa tu oga ile dawa miezi miwili ni
mingi sana mambo mengi yanaweza kutokea hapa katikati anaweza akakomaa kuwa
anataka kukuacha halafu ndoto zako zikaishia hapohapo kuwa makini sana
(Wakati huo
wanaendelea na mazungumzo msichana wao wa kazi aliyekuwa anafanya kazi ndogondogo
sebuleni anawasiliza maneno yao ya kebehi na umbea)
Mama :( Kwa
msichana wa kazi) we mbwa unasikiliza nini yaani hiyo kazi umechukua masaa
mia kuimaliza embu toka hapa nenda kapike huko tule
Msichana: sawa mama (anaondoka)
Mama: eti mama Mimi mama yako Mimi, sina mtoto
maskini kama wewe
Shangazi: au sio!!!
Christina :( anacheka)
wacha we
Mama: olewa mwanangu niishi Zaidi ya malkia maana
hiyo familia (anaguna) wana pesa
jamani loh…
Shangazi: hivi hili danga Christina alilipataje?
Mama: danga gani?
Shangazi: Raymond…
Christina: baba yake na baba yangu ni marafiki sana,
sasa siku moja kulikuwa na sherehe nikawa nimeenda na baba nay eye akawa
amekuja na wazazi wake hapo ndo tukaonana, baba zetu wakaanza kusema upumbavu
kuwa tunaendana na ingefaa kama tungeoana basi na yeye sijui akanipenda ndo tukaanza
urafiki mwisho tukawa wapenzi ndo leo hii tupo hapa
Shangazi: duh...
Christina: Na kipindi hicho Raymond alikuwa
ananipenda balaa jamani loh…nilie nini…Mimi tayari Napata …leo hii kawa mshenzi
sijui kaopoa mhindi huko...
(Wanacheka)
Mama:
wewe hawezi kuchanganywa na mhindi wale huwa wanachanganyana wenyewe…tu
Christina:
sasa nini jamani unajua amebadilika yaani kawa mkali (anaguna)
Mama:
atajijua mwenyewe
0 Comments