SCENE 41: -
SAFARI YA KWENDA SERENGETI: -
(Mchana wa siku ya jumamosi, Angelina na Raymond wanashuka katika kiwanja
kidogo cha ndege kilichopo Serengeti mbuga za wanyama)
Raymond: pole dear…ulikuwa unaogopa sana(anacheka)
Angelina: acha tu…unajua sijawahi kupanda ndege
katika maisha yangu na wala sikudhani kama kuna siku nitawahi kupanda ndege
Raymond: yote yanawezekana na unajua hilo…
Angelina:(anashangaa)
naweza kupiga picha?
Raymond: ndio…unaweza kuwa huru baby
Angelina:(anapiga
picha)
Raymond:(anafurahia
mazingira ya mbuga hiyo)
Mhudumu:(anakuja
na kuwakaribisha) karibuni sana…
Raymond: Asante sana…
Mhudumu: mngependa kufanyaje?
Raymond: ningependa kila kitu, kula, kulala,
kuangalia wanyama na kuwa na wakati mzuri mimi na mchumba wangu
Mhudumu: sawa…kuna vyumba vina elfu 40 na kuendelea
kuna chakula cha asili na vya kizungu
Raymond:(anacheka)
Angelina:(bado
anapiga picha kila kitu anachokiona)
Raymond: kwanza naomba ukatuonyeshe vyumba, baada
ya hapo tukatembee na kisha tuje tumalizie na kula
Mhudumu: sawa karibuni (anawaongoza njia)
Raymond: malaika…twende
Angelina:(anamfuata)
Raymond:(anaangalia
mazingira) wow jamani pazuri...
Angelina: sana
Raymond:(kwa Angelina)
umepapenda baby?
Angelina: pazuri…
Raymond: leo utapapiga picha mpaka tuelewe somo
Angelina: yaani we acha tu
Raymond:(anambusu
mdomoni) nakupenda sana
Angelina: hata mimi…ila (anamuangalia mhudumu) tusifanye ujinga mbele ya huyu dada
(wanacheka)
Raymond:(kwa mhudumu)
eti anakuogopa
Mhudumu:(anatabasamu)
wala asijali kabisa ndo maeneo yenu ya kujidai haya
Raymond:(kwa Angelina)
nilikuambia sikukuambia?
Angelina: uliniambia ila mwenzio nasikia usingizi…hatufiki
tu
Raymond:(anashangaa)
yaani wewe una vituko sana tumekuja kuenjoy au kulala
Angelina: vyote
Raymond:(anacheka
huku anamuangalia mhudumu)
Mhudumu: acha adeke jamani
Raymond:(anaguna)
haya bwana…mimi naenda kukuacha halafu ukiwa peke yako chumbani simba huwa
wanakuja kukutembelea (kwa mhudumu)
si eti dada ee
Mhudumu:(anacheka)
yaani nyie
Angelina: basi kama ni hivyo turudi nyumbani
Raymond: rudi peke yako…
Angelina: napajua basi hata huko tulipotoka
(wanacheka)
Mhudumu: yaani mna vituko kweli
Raymond: sio mimi ni (anamshika Angelina) ni huyu
Mhudumu:(anawafikisha
kwenye chumba kimoja kizuri na kinaonekana ni cha gharama sana) enhe!!mnakionaje?
Raymond: wow…kizuri kweli
Angelina: embu nione changu
(mhudumu na Raymond wanaangaliana kisha wanaangua kicheko)
Raymond: chako???
Angelina: ndio
Mhudumu: mnalala wote si wachumba?
Angelina:(anakaa
kimya)
Mhudumu: haya bwana mimi ngoja niwaache mtaenda
kulipia pale mapokezi
Raymond: sawa
Mhudumu:(anatoka)
Raymond:(anamfuata
Angelina na kumkumbatia kwa nyuma)
Angelina:(anaona
aibu)
Raymond: najua unaogopa sana mke wangu…naomba
usiogope mimi wala sitakudhuru na kama hutaki na hujisikii mimi nitakuelewa tu
Angelina: sawa nimekuelewa…
Raymond: okay dear…unataka kuoga kabla ya kwenda
kuangalia wanyama au unatakaje?
Angelina: kuoga sawa nitaoga kwanza
Raymond:(anamuonyesha
bafu) bafu ndo hili
Angelina:(anafungua
begi lake na kutoa khanga kwa ajili ya kuoga)
Raymond:(anacheka)
yaani unaniogopa wewe(anashangaa)sasa utamuogopaje mumeo?
Angelina:(anacheka)
Raymond: basi sawa ngoja nijipe adhabu naondoka
naenda zangu nje wewe oga ukimaliza nitarudi(anatoka)
Angelina:(anaingia
kuoga)
Raymond: (amekaa
nje anachezea simu yake)
(Baada ya dakika kama kumi na tano, Angelina anatoka kuoga na Raymond
anarudi ndani, anavua nguo kisha nay eye anaingia kuoga, nae ndani ya dakika
kumi na tano anamaliza kuoga, anatoka bafuni anakuta Angelina tayari ameshavaa anamsubiri,
anavaa mbele yake na anaonekana hajali, Angelina anaona aibu anatoka nje)
Raymond:(anacheka)
yaani wewe sasa usiponizoea sasa hivi utanizoea lini?
Angelina:si bado (anatoka nje)
(baada ya dakika kadhaa Raymond nae anatoka nje)
Raymond: haya twende
Angelina: nishike mkono maana naogopa kweli
Raymond: usiogope nipo na wewe mpenzi wangu
Angelina: (anatabasamu)
(Wakiwa wameshikana mikono wanaelekea mbugani kuangalia wanyama, huko
wanafurahia mandhari, wanapiga picha kwa kifupi wanaonekana wanafurahia
mapumziko yale ya mwisho wa wiki)
0 Comments