SCENE 42: -
BAADA YA SIKU TATU: -
(jioni ya siku ya tatu, baada ya Raymond na mchumba
wake (Angelina)kurudi kutoka Serengeti, Raymond anafika nyumbani kwa baba na
mama yake, anawakuta wazazi wake wamekaa wametulia huku wakiburundishwa na runinga
kubwa iliyopo sebuleni hapa)
Raymond:(anaingia
ndani) shikamoo mama, shikamoo baba
(wanaitikia)
Mrs.Bembele: oh, my son…za Serengeti?
Raymond:(anashangaa) Serengeti tena mama?
Mr. Bembele:si uliondoka ukaenda Serengeti wewe na
mchumba wako?
Raymond: nani Christina?
(wazazi wake wanaangaliana)
Mrs.Bembele: embu acha masihala…mchumba wako ni Christina?
wewe si ulikuja kutuambia kuwa umemvalisha pete ya uchumba Angelina?
Raymond:(anaonekana
haelewi kitu chochote) Angelina wa wapi?
Mrs.Bembele:ni msichana wako wa kazi ila umempenda
kisha ukaamua kumvalisha pete ya uchumba na unataka kumuoa
Raymond: mimi? mama mimi naanza saa ngapi kuoa
msichana wa kazi?
(wazazi wake wanashangaa sana)
Raymond: anyways…mimi nimechoka nilipokkuwa hata
sipajui kwakweli mara watu waniite dokta mara sijui nini?
(wazazi wanashangaa)
Raymond: naenda kulala… (anaingia chumba ambacho alikuwa analala wakati anaishi katika jumba
hilo la kifahari)
Mr. Bembele: Raymond…siku hizi una nyumba
yako…hicho chumba siku hizi sio chako
Raymond: baba unanifukuza nyumbani kwako au?
Mrs.Bembele: umekuwaje? wewe Raymond umekuwaje
mwanangu wamekufanya nini huko Serengeti mwanangu?
Raymond: sijawahi kwenda Serengeti na wala
sijamvalisha pete ya uchumba mtu hata Christina bado sijamvalisha ila
nitamvalisha mpenzi wangu nampenda
(wazazi
wanashangaa sana)
Mrs.Bembele:(anachukua
simu na kumpigia Angelina)
(simu ya Angelina inaita)
Angelina: (anapokea)hello
mama, shikamoo mama yangu…
Mrs.Bembele: marahaba mtoto wangu hujambo?
Angelina: sijambo…
Mrs.Bembele: wewe unajua hatumuelewi huyu mwenzio
Angelina: kwanini mama yangu?
Mrs.Bembele: kaja hapa sijui kapoteza
kumbukumbu…sijui kafanyaje…hakumbuki kuwa yeye sasa hivi ni dokta, hakumbuki
kuwa sasa hivi ana nyumba yake mwenyewe, hakumbuki kama wewe ni mchumba wake na
wala hakumbuki kuwa mlienda Serengeti
Angelina: yaani acha tu mama…mimi mwenyewe leo
nimempigia simu yaani hanikumbuki nimejitambulisha hakumbuki wala nini…mimi
nikajua masihara yake kumbe kaja na huko
Raymond: jamani…mimi kichwa kinaniuma sana…naomba
nikalale
Mr. Bembele: baba…una kwako…twende nikupeleke
Raymond:(anatabasamu)
umenipa surprise baba…nimependa hiyo…
Mrs.Bembele:(bado
anaongea na Angelina) yaani sijui amekuwaje huyu mtoto…ngoja tunakuja nae
huko akiamka maana anasema anataka kulala kichwa kinamuuma
Angelina: sawa mama
Mrs.Bembele: haya mwanangu (anakata simu kisha anamgeukia Raymond) haya nenda kalale mwanangu
Raymond: sawa mama (anaingia ndani)
Mr. Bembele: nini tena hiki jamani?
Mrs.Bembele: yaani sielewi nini kimemkuta mwanangu
(wanasikitika sana)
Mr. Bembele: sijui tu
(Upande wa kina Christina anamalizia kupokea simu ya Raymond)
Mama :( anakuja
alipo Christina) unaonyesha furaha sana, una yapi mwenzetu
Christina: wala…nina raha zangu tu (ananyanyuka na kwenda chumbani kwa shangazi
yake)
Shangazi :( hana
uchangamfu wa kawaida)
Christina :(
anacheka Sana)
Shangazi: mwenzetu vipi? Mbona una raha Sana?
Christina: yule mtaalamu noma…
Shangazi: kivipi?
Christina: Raymond yupo kwao
Shangazi: kwahiyo kama yupo kwao?
Christina:(anacheka
sana) nilichomfanyia mpaka mimi binafsi nimejiogopa
Shangazi: umemfanyia nini mtoto wa watu?
Christina: nimeirudisha akili yake nyuma…hakumbuki
chochote kilichotokea hivi karibuni
Shangazi :(anaguna)
kwahiyo unaona ufahari? kuroga?
Christina: sana…katoka kunipigia simu ananiita jina
alilokuwa ananiita…tena na sauti ya madeko… (anaiga sauti ya madeko) Darling (anacheka kwa nguvu)
Shangazi:(anacheka)
nasikitika kuwa sisi wenyewe tulikuharibu halafu tumejikuta tu tumekushindwa…Christina
hata iweje…Raymond hawezi kukuoa maana Mungu mwenyewe hajapanga wewe uolewe na Raymond...
Christina: muone…wewe mwanamke una wivu wewe
Shangazi: moyo wa Raymond…upo kwa huyo kijakazi
wake…wewe umemchezea akili tu…ila amini nakwambia Raymond akimuona Angelina kwa
macho yake moyo wake utapingana vikali sana na akili yake…utakuwa umepoteza muda
na pesa kijinga
Christina: tutaona…
Shangazi: tutaona…Christina…Raymond anampenda sana Angelina
Christina: hapana…ananipenda mimi
Shangazi: umemroga…hata ungemrudisha kumbukumbu za
miaka 30 iliyopita bado Raymond akimuona huyo binti moyo wake utamtamani sana
huyu binti
Christina: tutaona… (kwa hasira) tutaona, kama Raymond hatanioa
Shangazi: unajua kwanini mimi nilianza kwenda
kinyume na wewe kwasababu niliona mapenzi waliyonayo Raymond na Angelina ni
mapenzi ya dhati na hakuna aliyewahi kuyatenganisha mapenzi ya dhati iwe uchawi
au nini, Angelina anampenda kweli Raymond yaani hajali kwamba Raymond ana hela
au lah
Christina :(anafyonza)
Shangazi: utafyonza sana Christina ila ukweli ndo
huo hapo…ukubali, mchezee sana Raymond na akili yake maskini ila hakuoi…hawezi kukuoa,
anampenda sana Angelina yaani hata wewe hakuwahi kukupenda kama anavyompenda Angelina
Christina :(
machozi yanamlenga)
Shangazi: habari bure…
Christina: atanioa
Shangazi: sawa…toka chumbani kwangu nataka
kupumzika…umefikia mpaka kuroga ili umpate mwanaume na sio kwamba unampenda
unataka pesa zake…hivi unadhani Mungu haoni? Utaaibika vibaya na siku wala sio
nyingi
0 Comments