SCENE 43: -
(Asubuhi ya siku iliyofuata, wazazi wa Raymond na Raymond wanafika
katika jumba la kifahari la Raymond, wanapofika Raymond anaonekana kushangaa
mazingira hayo kama mtu ambae hajawahi kuliona hata siku moja, mama yake
anamuangalia na kugundua kuwa mwanae anashangaa sana)
Mrs.Bembele: mtoto wetu amefanyaje mbona kama
kapoteza kumbukumbu…yaani anakumbuka tu sisi ni wazazi wake ila hakumbuki kuwa
ana nyumba yake na kazi yake
Mr. Bembele: tulia mke wangu hakuna
kitakachoharibika tutulie na tujaribu kujua nini kimemsababishia kusahau kila
kitu labda ameumia kichwa na kama ni hivyo tumuwaishe matibabu
Mrs.Bembele: kweli kabisa mume wangu…ngoja nimuulize
mkwe wetu Angelina labda walipokuwa Serengeti labda mtoto wetu alipata jeraha
kichwani tunatakiwa tujue
Raymond: mama, mbona baba kawa mpole hivi yaani
hata hanigombezi tangu jana
Mrs.Bembele:ni baba yako mwanangu…anakupenda sana…
Raymond: anyway…tuachane na hayo… (anamuona Ramadhani) habari yako kaka?
Ramadhani:(anashangaa)
He!!bosi
Raymond:(anashangaa)
boss???boss yupi?
Ramadhani:si wewe…mimi Ramadhani
Raymond: wa wapi?
Ramadhani:(anashangaa
sana) Ba!!!mazito haya jamani nyie
Mrs.Bembele: Ramadhani kaendelee na kazi zako
Ramadhani: mama mbona boss kasahau au
anajifanyisha?
Mrs.Bembele: hapana…wewe nenda tu kila kitu kitakaa
vizuri
(Angelina anakuja, Raymond anamuona lakini katika hali ya kushangaza
anavutiwa nae)
Raymond: mama huyo dada ni nani?
Mrs.Bembele: ndo yule mchumba niliyekuwa nakwambia
Raymond: mmenichagulia?
Mr. Bembele: hapana mwanangu…ulimchagua mwenyewe...
Raymond: lini?
Mrs.Bembele: mna muda kidogo tangu mmependana…
Raymond: hata sikumbuki vizuri lakini wow…ni Mrembo
sana, amenivutia sana
(Mr na Mrs. Bembele wanaangaliana)
Mrs.Bembele: amekuvutia?
Raymond: ndio…mpaka leo nilikuwa sijawahi kuona
mwanamke Mrembo Zaidi ya Christina… (kimya
kidogo huku anamuangalia Angelina anayekuja kwa mwendo wa kuvutia) kwani
huyu dada anaitwa nani?
Mrs.Bembele: anaitwa Angelina…
Raymond: wow…Angel
Angelina:(anawafikia
na kwa heshima anawasalimia wazazi wa Raymond kwa heshima kubwa sana)
shikamoo mama, shikamoo baba (anapiga
magoti)
(wazazi wanamuitikia)
Angelina:(kwa
Raymond) dear…shikamoo
Raymond:(anatabasamu)
marahaba…Angel hujambo? Ee wewe mzuri jamani
Angelina: sijambo… (kwa wote) karibuni sana (anawaongoza mpaka bustanini)
(wanafika bustanini wanaketi na Angelina anaenda jikoni kuleta vinjwaji)
Raymond: mama…huyu dada ana heshima Christina hana
hata heshima si huwa mnamuona?
(wazazi wanaangaliana)
Raymond: mbona mnaangaliana? kwani nasema uongo?
Mrs, Bembele: hausemi uongo mwanangu
Raymond: sijui mlinichagulia au nilijichagulia
mwenyewe nimempenda sana huyu dada na nitamuoa…kesho nitaenda kumwambia
Christina kuwa sitaweza kumuoa…ila sijui atanielewa kweli?
Mr. Bembele: atakuelewa tu…
Raymond:(anamuangalia
baba yake) baba…asante kwa nyumba…nzuri na kwa mchumba mzuri Angel…
Mr. Bembele: usijali mwanangu, ila Angel ulimchagua
mwenyewe
Raymond: sawa, labda nimesahau kidogo(anacheka)hivi Edmond yupo wapi?
Mr. Bembele: atakuwa kwake
Raymond: anatakiwa awepo hapa kwenye ufunguzi wa
nyumba yangu
(Angelina anarudi na vinywaji, anawatengea kisha anaenda jikoni, Raymond
anamfuata)
Raymond: Angel…
Angelina: nambie dear, nini kimekupata? mbona jana
asubuhi uliondoka vizuri kwenda kazini?
Raymond: kazini? kwani mimi kazini kwangu ni wapi?
Angelina:(anamshangaa)
jamani umekuwaje leo? au unanitania?
Raymond: sikutanii Angel sema nini yaani
nimekupenda kweli...wewe mtaratibu sana una heshima unafaa kweli kuwa mke wangu
yaani wazazi wangu wamefanya vizuri sana kunichagulia mke na wenyewe wameona
kuwa Christina hatanifaa kama mke, kwanza nimemfumania na yule hawara yake kama
sio mara kumi basi mara kumi na mbili yaani…nampenda ndio ila hatanifaa kuwa
mke wangu nitakufa siku sio zangu
Angelina:(anacheka)
yaani wewe huo utani wako siupendi bwana baba na mama wanahofia sana bwana
Raymond: haki ya Mungu jamani mimi sikutanii…Angel
Angelina: inamaana hukumbuki kuwa tumetoka
Serengeti siku sio nyingi?
Raymond: hapana sikumbuki yote hayo…inamaana kumbe
tumeanza kuwa pamoja?
Angelina:(anamuangalia
usoni kwa muda) ulifanyaje Raymond mpaka umesahau kila kitu…
Raymond: sio kwamba nimeshau kila kitu…ila
nachoshangaa sijui kwanini Edmond hajaja kuniona muda Mrefu
Angelina: Edmond alikuja kabla hatujaenda Serengeti
Raymond: mimi sijawahi kwenda Serengeti Angel…
(Mrs.Bembele anakuja)
Mrs.Bembele: Angelina, naomba nikuulize kitu kama
hutajali…
Angel: sawa mama
Mrs.Bembele: Raymond naomba utupishe kidogo
Raymond: sawa (kwa
Angelina) nimekupenda kweli (anamshika
shavu kisha anaondoka)
Mrs.Bembele:ni ajabu ila ni kweli…Raymond amesahau
baadhi ya vitu ila moyo wake haujasahau kuwa anakupenda Angel
Angelina :( anatabasamu)
mama kwani amefanya nini?
Mrs.Bembele: sijajua ila tunahisi labda ana jeraha,
huko Serengeti hakujipigiza sehemu labda?
Angelina: hapana mama…hakujipigiza sehemu…
Mrs.Bembele: sijui amefanyaje…ila afadhali hiyo
haijaathiri mahusiano yake na yako…yenu namaanisha
Angelina: yaani hilo ndo la kumshukuru Mungu mama
Mrs.Bembele: usijali mwanangu kila kitu kitarudi
kama kilivyokuwa…na baada ya hili mipango ya harusi yenu itaanza
Angelina:(anacheka) asante mama…
Mrs.Bembele: haya andaa andaa kwa ajili ya
mumeo…amesema amekupenda
Angelina:(anacheka)
Mrs.Bembele :(
anacheka kisha anatoka) haya mie ngoja nikawakute huko sijui wanafanya nini
Angelina: haya mama…ngoja Mimi niandaeandae… (Anaendelea na shughuli zake)
0 Comments