SCENE 44: -
(Asubuhi
nyingine iliyo ya kawaida kabisa, Christina anafika katika ofisi ya Mr. Bembele,
Kama ilivyo kawaida anaingia bila kumsalimia mtu yeyote, anapita na kufika
alipo Mr. Bembele)
Christina: habari yako
Mr. Bembele :(
ananyanyua uso maana alikuwa ameinamia kitabu Fulani kisha anacheka kwa kejeli)
Christina: nimekusalimia
Mr. Bembele: nimesikia lakini je unahisi wewe
unaweza kunisalimia mimi hivyo? Ndo maana Raymond anasema huna adabu (anacheka)
Christina: wewe si mpenzi wangu lakini?
Mr. Bembele :(
anacheka sana, kisha anajizungusha kwenye kiti chake) umesahau? au umekuwa Raymond?
Christina: kafanyaje?
Mr. Bembele: kasahau…mambo mengi sana
Christina:(anajisemea
moyoni) ushindi huo(anatabasamu)
Mr. Bembele: ila hatujui atakuwa hivyo kwa muda
gani…au atakuwa anatudanganya
Christina:(anajisemea
moyoni) hajifanyishi nimemtengeneza na nimehakikisha anakumbuka penzi letu
na sio penzi la huyo housegirl
Mr. Bembele: umekuja kufanya nini Christina?
Christina: nataka turudiane
Mr. Bembele:au sio (anacheka) unataka yaani lazima? kwanini? ili iweje?
Christina: nakupenda…sana baby
Mr. Bembele:(anacheka
sana) sikiliza Christina…it was a mistake my dear mimi wala sitaki kesi
mimi na familia yangu tuko vizuri na sitaruhusu yeyote aharibu yote hayo,
sitaki na wala sijisikii kurudiana na wewe nampenda sana mke wangu
Christina:(anatoa
simu yenye meseji na picha walizokuwa wakipiga wakati wana mahusiano)
nitamuonyesha mkeo kila kitu
Mr. Bembele:(anamuangalia
kwa muda) are you blackmailing me?
Christina: nah baby nah (anamsogelea)…iam warning you…
Mr. Bembele:(anasikitika
sana) maskini unahangaika…kweli…vipi huna hela?
Christina:(anapandwa
na hasira)
Mr. Bembele: nakuuliza huna hela?
Christina: nataka kurudiana na wewe
Mr. Bembele: haiwezekani…na nipo serious…siwezi
kumsaliti tena mke wangu hasa na wewe
Christina: naenda kumuonyesha hizi picha
Mr. Bembele: sitakuruhusu unichezee akili yangu
kama unataka kumuonyesha mke wangu picha hizo sitakuzuia…unaweza kwenda tu
ukamuonyesha
Christina:(anamshangaa)
Mr. Bembele: unatoa macho…nenda ukamuonyeshe hizo
meseji…huna video ambazo zinaonyesha mimi na wewe tukiwa pamoja kitandani? kama
unazo pia kamuonyeshe…
Christina:(anabaki
anashangaa)
Mr. Bembele: sitakuruhusu Christina unipeleke kama
ulivyokuwa unanipeleka sijui ulikuwa unatumia dawa…sijui nini (anakaa kimya kidogo) embu subiri
kidogo…au ni wewe ndo umecheza na akili ya mwanangu…
Christina: hamna
Mr.Bembele:anyway…fanya utakavyo ila sitakuruhusu
utuingilie mimi na familia yangu…tena,mke wangu ni mzee ndio ila nampenda sana
mke wangu na kuhusu hizo picha kama unahisi hizo picha na meseji zitanivunjia
ndoa umechemsha…nitamwambia kila kitu Glory wangu nitamuomba msamaha najua
atakasirika siku mbili tatu ila hataniacha,yataisha ndo maana nimekuambia nenda
peleka tena upeleke zote usipeleke nusu nusu kusanya zote ili kama unaenda
kumwambia Glory umwambie ili nikikaa kumuomba msamaha iwe moja kwa moja na sio
kila saa na kesi mpya
Christina :(
kimya)
Mr. Bembele: nakuelewa Christina kuwa hutaki
kupoteza zile raha tulizokuwa tunakupa Mimi na Raymond, najua tulikuwa tunakupa
pesa unakula raha utakavyo, ila sasa maisha yanabadilika sana Christina…mimi ni
wa Glory na Raymond ni wa Angelina
Christina:(anakumbuka
maneno ya shangazi yake) Mhhh (anakumbukia
maneno ya shangazi yake) Raymond ni wa Angelina na Bembele ni wa Glory
waache mwanangu…wewe ni wa Peter… (anashusha pumzi)
Mr. Bembele: wewe uliwahi kuwa mtu wetu wa karibu
sana ukiwa unaomba pesa tutakuwa tunakupatia tu
Christina:(anajisemea moyoni) siwezi kushindwa
hivihivi…mimi sio wa kushindwa, nawataka wote wawili, nitafanya kila kitu mpaka
muwe wangu tu
Mr. Bembele: wewe ni binti mzuri sana
unajua…kwanini usitafute kijana tu mzuri akuoe
Christina:(machozi
yanamlenga huku anamuangalia Mr. Bembele kwa hasira sana)
Mr. Bembele: now if you don’t mind naomba uondoke
nina kazi nyingi nina kikao muda si mrefu
Christina: huwezi kuniacha hivihvi Desmond
Mr. Bembele: wow leo umeniita jina langu
kabisaaaaa…halafu mbona kama unani command?
Christina: yaani umenichezea weee halafu unakuja
kuniacha solemba?
Mr. Bembele: ndio kwani wewe ulijua mimi nitakuoa?
ulidhani mimi Desmond baba yake Raymond naweza kumuacha Gloria mama yake Raymond
na kukuoa wewe?
Christina:(anamuangalia) sio vizuri lakini
Mr. Bembele: sasa wewe sisi tukufanyeje?
nimekuambia sisi hatutakuacha kila mara ukitaka msaada tuambie ila sasa naona
huelewi unanilazimisha nikurudie yaani niachane na mke wangu nikurudie wewe
embu acha zako hizo, halafu naomba uende bwana mimi nina kazi zangu na pia mke
wangu atakuja muda si mrefu na pia tambua mwanaume yeyote hawezi kumuacha mkewe
na kumuoa hawara my dear…sisi kutembea nje ya ndoa huwa tu ni tamaa zinatutesa
and nothing more
Christina: nataka nimuone mkeo Desmond nataka
kumwambia kila kitu
Mr. Bembele:(huku
anacheka) karibu sana…keti msubiri Glory anakuja sawa ee
Christina:(anashangaa)
Mr. Bembele: kaa mbona bado umesimama
Christina:(anajisemea
moyoni) mbona haogopi?
Mr. Bembele: najua unajiuliza sana ila ukweli ni
kwamba yaani sikuogopi hata kidogo fanya utakavyo...sio mimi sio Raymond huwezi
kutupata Christina nenda kwa waganga, walete hata kama umejaza lori zima mama
hatutakuwa na wewe mama yangu…nilikuwa na wewe tu kama tamaa zangu mwenyewe na
sio kwamba mke wangu ana kasoro yoyote hapana…kwanza mke wangu pamoja na uzee
wote ule bado humfikii uzuri…unadhani au ulidhani naweza kabisa kumuacha mke
wangu na nikakuoa wewe?
Christina:(anakasirika sana)
Mr. Bembele: nenda karoge…mama nenda mpaka kanisani
ukaombewe…yaani kama umekosa mwanaume wa kukuoa basi piga maombi sana acha
kunisumbua mimi na mwanangu…hatukutaki…(anafyonza)unakuja
kunionyesha picha na kunitishia mimi ili nikutetemekee umechemsha wewe kama una
shida sema usaidiwe lakini sio kuforce…na nina wasiwasi hata mwanangu ni wewe
ndo umemfanyia hayo yote ili akukumbuke wewe tu…jiandae kwa mshangao mama (anacheka sana) get ready christina mdada
mrembo usiyejua kujishughulisha kazi kuvizia wanaume za watu wanawake sasa hivi
hawako tena huko chez ahata upatu basi ujikwamue uache kuhangaika na waume za
watu.embu nenda zako bwana
Christina:(anatoka
nje kwa hasira)
Mr. Bembele: njoo umsubiri Glory yupo njiani anakuja
(anacheka sana)
Christina:(anatoka
nje na kuelekea alipoegesha gari lake) shit!!!mbona nimefeli mimi…sijaweza
kumshawishi huyu mzee arudiane na mimi… (anashusha
pumzi) lakini hapana nisikate tamaa bado nina Raymond (anacheka)maskini basi kajua ameniweza…nina Raymond baada ya muda Raymond
atakuja kunioa (anacheka)mali zote za
huyu mzee zitakuwa zangu...(anacheka)
(Gari la Mrs.
Bembele linakuja, linaegesha karibu na gari la Christina, kisha Mrs. Bembele
anashuka akiwa amependeza kwelikweli, ama hakika mama yake Raymond ni mrembo bwana
na anastahili sifa zote)
Christina: kile kibibi kizee(anafyonza)kibayaaa!!(anapanda
gari kisha analiondoa kwa mwendo wa kasi sana)
0 Comments