SCENE 45: -
(Asubuhi ya siku kama ya tatu baada ya Christina na Mr. Bembele kukutana
ofisini, Raymond anafika nyumbani kwa kina Christina, kama kawaida
anakaribishwa na mama yake Christina ambae mara nyingi sana anapenda kukaa
sebuleni akiangalia runinga)
Mama: karibu mwanangu
Raymond: asante mama, shikamoo
Mama: marahaba baba
Raymond: sijakuona siku nyingi kweli jamani
umepotelea wapi?
Mama:(anaguna)
Ray baba siku nyingi kama muda gani?
Raymond: mwaka na kitu hivi
Mama:(anacheka) masihala hayo baba…sisi tumeonana
mara ya mwisho juzi tu hapa…
Raymond:(anaguna)
(shangazi anakuja mahali hapo)
Shangazi:( kwa
Raymond) hujambo baba…
Raymond: sijambo mama shikamoo…(anamshangaa)yaani na wewe umepotea kweli
shangazi
Mama:(anashangaa)
yaani sijui kawaje huyu jamani…eti anasema mimi hajaniona mwaka
Shangazi:(anacheka)
utamuweza huyu kwa vituko (anajisemea moyoni) kumbe kweli Christina kamfanyia
vibaya mtoto wa watu(anaguna)
Raymond: yaani mimi ndo siwaelewi…lakini sawa Christina
yuko wapi?
Mama: chumbani kwake…wewe muone tu
Raymond:(anaelekea
chumbani kwa Christina cha kushangaza anaenda chumba alichokuwa anatumia Christina
zamani)
Shangazi:(anamfuata)
sio huko baba (anamuonyesha Christina
alipo)
Raymond: amehama?
Shangazi:(anatabasamu)
ndio amehama
Raymond:(anaingia
chumbani kwa Christina)
Christina:(amekaa
kitandani akiwa katika pozi la mitego) karibu mpenzi
Raymond: asante Christina…
Christina:(ananyanyuka
na kumfuata aliposimama na kumkumbatia)
Raymond:(harudishi
badala yake anamtoa kwa upole) Christina sikia kuna kitu nataka kukuambia
Christina: utaniambia baadae...kwa sasa nipe nafasi
mpenzi wangu nikuonyeshe mambo mazuri
Raymond: No... (anamsukuma
kidogo) kuna kitu nataka nikuambie please nipe nafasi...niongee
Christina: najua unataka kuniambia ni jinsi gani
unavyonipenda baby…najua
Raymond: hapana Christina sitaki kukuambia hivyo
Christina: ila?
Raymond: sikia (anashusha
pumzi) najua tumetoka mbali sana katika penzi letu…
Christina: ndio najua…
Raymond:na tambua kuwa sio kila penzi huishia
kwenye ndoa
Christina: una maana gani?
Raymond: wazazi wangu wamenichagulia mchumba
wananiambia kuwa nilimvalisha pete ya uchumba na kwamba mimi ndo nilimchagua mwenyewe…ukweli
ni kwamba mimi sikumbuki chochote Christina
Christina: kama hukumbuki chochote basi
hukumvalisha pete wanakudanganya hao…wazazi wako
Raymond: hiyo sijui…ninachojua mimi ni kwamba
nampenda huyo binti sana…nisamehe tu Christina yaani nampenda kupita kiasi,
yaani sijui nikuambieje...nampenda sana yaani ananivutia sana
Christina:(anakasirika
sana)
Raymond: nielewe Christina najua sipaswi kukuambia
hivi wewe ni mpenzi wangu wa siku nyingi sana…lakini kwa mapenzi nayoyahisi juu
ya huyo binti haki ya Mungu tena nimejitoa mhanga itakavyokuwa naiwe tu
Christina: that is not fair Raymond mimi ni mpenzi
wako kwanini unaniambia maneno hayo?
Raymond: ndo maana nimekuomba msamaha kwanza jamani
nisamehe mwenzio...
Christina: get out
Raymond: usikasirike Christina...nampenda sana Angelina
na nipo tayari kumuoa…
Christina: toka nje
Raymond:(anatoka) nielewe
(anafika sebuleni)
Mama: baba mbona mnagombana na mwenzio?
Raymond: mama kwani ni kosa kumpenda mtu?
Mama: sio kosa baba kwani nini?
Raymond: anyway, tuyaache hayo mama… (anaondoka zake)
Shangazi:(anaenda alipo Christina) imekuwaje?
Christina:(akiwa
anatokwa machozi) wewe mwanamke ni mchawi
Shangazi: una maana gani?
Christina:(Analia)
Shangazi: kwanini unaniita mchawi?
Christina: umefanya nini?
Shangazi: nimefanya nini kwani?
Christina: umeenda kuipindua dawa yangu
Shangazi:(anacheka
kidogo) imegoma?
Christina:(anamuangalia
shangazi yake kwa hasira)
Shangazi:shoga yangu haijagoma…wewe huoni Raymond anakumbuka tu vitu vilivyotokea
miaka miwili iliyopita,miaka miwili iliyopita mlikuwa katika mapenzi
motomoto,miaka miwili iliyopita hakumuona mama yako kama mwaka mzima na ndo alichomuambia hapo…mpaka mama yako
ameshangaa..hiyo dawa uliyoitengeneza kurudisha matukio nyuma kwa Raymond wala
haijadunda ila…moyo wa Raymond umempenda Angelina kupita kiasi yaani
anachotumia Raymond kwa sasa ni moyo…najua Angelina anashangaa haelewi nini
kinaendelea anamuona mtu hakumbuki hiki wala kile ila anampenda…ni moyo
mama…pole sana tangu mwanzo wewe na Raymond hamkuwa wala hamkupangiwa kuwa ni
sisi t undo tulikuwa tunapanga ila kwa sasa Mungu ameona imetosha
Christina: nimemlipa pesa nyingi sana huyo mganga
nilijua Raymond leo kaja turudishe penzi letu…nilipanga leo akija nitabeba
mimba yake
Shangazi: pole mipango yako haijatimia ila huo ndo
ukweli wa mambo na ni jukumu letu sote kulikubali na kulitii
Christina: nitamfanyia kitu mbaya angelina…mpaka
atajuta
Shangazi: hata iweje Christina huwezi
kuwatenganisha wale watu
Christina: naweza…ninaweza (kwa ukali Zaidi) nimesema naweza mimi ndo Christina sishindwi kitu
Shangazi: hushindwi kitu umekuwa Mungu wewe?
Christina :( anamuangalia
shangazi yake kwa hasira) toka nje
Shangazi :( anatoka)
Christina :( Analia kwa hasira sana) yaani Raymond
anakuja kuniambia kuwa hanitaki tena? pamoja na kufanya yote yale…(anafyonza)ngoja nimpigie yule mganga (anachukua
simu kisha anapiga)
(simu inaita)
Mganga:(anapokea) hallo…
Christina: rudisha pesa yangu…wewe mwizi dawa
haijafanya kazi
Mganga: labda ulikosea masharti (anakata simu)
(Christina anabaki amekasirika na Analia
Sana)
0 Comments