SCENE 46: -
(Raymond na Angelina wapo nyumbani kwa Raymond)
Raymond:(anacheka)
yaani huwezi amini ila nakupenda kwa mambo mengi sana…napenda una heshima sana,
unajua kupika, unajua kupanga bajeti vizuri, na Zaidi unaonekana unanipenda
sana…
Angelina:(anamuangalia
kisha anatabasamu)
Raymond: mi nimechoka kusimama twende sebuleni
(Wanaenda sebuleni)
Raymond :( anampakata)
Angelina :( anajisemea
moyoni) yaani huyu amesahau mambo mengi…nashangaa hajasahau kuwa mimi nay
eye tunapendana sana
Raymond: mbona huongei…?
Angelina: wala sina usemi mimi nakusikiliza wewe
Raymond: unajua mwenzio sijui ninakuwaje yaani
nimesahau kila kitu…hivi nimeshakutolea mahari eeh
Angelina: hapana bado…
Raymond: inabidi nimwambie baba ili twende tukatoe
mahari mpenzi wangu yaani natamani nikuoe haraka uwe mke wangu
Angelina; unajua kabisa kuwa hata mimi natamani
kuwa mkeo mpenzi
Raymond: twende tukaoane tutoroke(anacheka)
Angelina:(anacheka) tutauliwa
Raymond:ni kweli…sasa naomba nimpigie simu Edmond
aje sasa hivi…
Angelina: unakumbuka kuwa Edmond ni rafiki yako?
Raymond:(anacheka)
jamani Edmond ni rafiki yangu tangu tuna miaka 20…mpaka leo nina miaka 30
Angelina:(anajisemea
moyoni) kasahau kuwa ana miaka 32…karudi miaka miwili nyuma
Raymond:(anamshika
Angelina kidevu) yaani nakupenda wewe…ona ulivyo mzuri jamani
Angelina:(anacheka)
asante hata mimi nakupenda sana na unajua hilo
(wanabusiana)
Raymond: ngoja nimpigie simu Edmond…aje (anapiga simu)
(simu inaita)
Edmond:(anapokea)
hello
Raymond: mwana mpotevu
Edmond: (anashangaa)
tangu lini mimi nikawa mwanampotevu?
Raymond: sijaongea na kukuona siku nyingi sana
Edmond: acha masihala…si tumeongea jana tu?
Raymond :(anashangaa
sana)
Edmond: (anabaki
anashangaa)
Raymond: anyway…tuachane na hayo…kuna dada mmoja
wazazi wangu wanasema kuwa nimemchagua mwenyewe ila ukweli ni kwamba mimi
sijamchagua yaani sikumbuki, ila Mond nampenda huyu dada uwiii yaani sijui
nikwambieje
Edmond:(anaguna)
inamaana umempenda demu mwingine mbali na Angelina?
Raymond: anaitwa Angelina
Edmond:(anashangaa
sana) unajua masihala yako mimi huwa siyapendi yaani unaleta masihala mpaka
kwenye mambo muhimu
Raymond: una maana gani nakutania Mond?
Edmond: huyo demu ni shemeji yangu na wewe
umempenda muda mrefu sana mara baada ya kuishi nae hapo kwako alikuja kama
housegirl
Raymond:(anashangaa)
hausigeli tena?
Edmond: ndio na ni mimi ndo nilikuletea (anacheka)yaani dokta Raymond bwana
kwahiyo unaniletea masihala mimi?
Raymond: dokta Raymond tena?
Edmond: ndio wewe dokta
Raymond: najua hiyo ni ndoto yangu ila bado sijawa
dokta…nitamaliza baada ya miaka miwili, nasoma bado kwanza nilitakiwa kuwa
india nashangaa nipo tanzania
Edmond: Raymond una nini?
Raymond: kwani vipi? nawashangaa wote mnanipeleka
mbele miaka miwili...mara wengine wananiita dokta…nimeenda kwenye ofisi Fulani
yaani kila mtu dokta…dokta yaani mnanichosha
Edmond:(anashangaa
sana) jamani
Raymond: anyway…tunatakiwa kupeleka mahari kwa
mchumba wangu
Edmond: tumeshapanga mimi, wewe na mama yako
Raymond: saa ngapi?
Edmond: ulifanyaje ulipoenda Serengeti?
Raymond: mimi sijawahi kwenda Serengeti ingawa
natamani sana kwenda kupumzika na mpenzi wangu yaani mwanamke nitakayemchagua
mwenyewe…kama Angelina, nitaenda na Angelina…by the way nimeshaachana na Christina
yaani nilipomuambia amekasirika ila nikamwambia mimi nimeamua kama ana hasira
sana basi agalegale
Edmond:(anacheka kidogo) unajua wewe uliachana na Christina
siku nyingi sana lakini sawa…nitakuja huko
Raymond: karibu…sana uje umuone Angelina
Edmond: namjua
Raymond: haina shida njoo umjue tena
Edmond:(anakata
simu) jamani
Catherine:(anamtengea chakula) nini? maana ulikuwa
unashangaa tu muda wote mnaongea na Raymond kuna nini?
Edmond: kuna tatizo
Catherine: lipi tena?
Edmond: Raymond hayuko sawa…
Catherine: kivipi? (anakaa)
Edmond: amepoteza kumbukumbu…yaani hakumbuki
kabisaaaa chochote kilichotokea hivi karibuni yaani akili yake imerudi miaka
kama miwili nyuma
Catherine: wewe Edmond inawezekana vipi hiyo?
Edmond: sijui…labda kuna sehemu amejigonga vibaya
kichwani
Catherine:(anashusha
pumzi) yaani Angel sijui itakuwaje
Edmond: cha kushangaza anampenda sana Angelina
Catherine: yaani hiyo inachanganya…
Edmond: aha!!kuna kitu nakumbuka juzi mama yake
aliniambia kuwa Raymond hayupo vizuri
Catherine: kwa mantiki hiyo wampeleke hospitali?
Edmond: ngoja kesho nitaenda ili nimuelewe vizuri
maana hata simuelewi kabisaa
Catherine; kwahiyo hakumbuki hata kwamba mlikuwa
marafiki
Edmond: tangu naanza urafiki na Raymond huu ni
mwaka wa 12 na yeye akili yake imerudi miaka miwili nyuma na wala simuelewi
Catherine:(anakula
chakula kidogo) yaani dunia ina mambo hii(anaguna)
Edmond:(anaguna) kuna nini hapo?
Catherine: sijui ndugu yangu atakuwa anaendeleaje huko?
na penzi lao ni la muda mfupi lakini limepitia mambo mengi
Edmond; sana…ila watavuka maana kuna upendo wa
dhati kati yao (anatafakari kitu)
0 Comments