SCENE 47: -
(Mchana mwingine wa siku nyingine tena tulivu sana, kuna jua la kawaida
na hali ya hewa iko sawa kabisa, muda ni majira ya saa saba, Christina
anaegesha gari lake mbali kidogo na nyumba ya Raymond, hatoki ndani la gari
badala yake anayaangalia mazingira yale kwa mbali)
Christina:yaani nimejisumbua nimeenda mpaka kwa
mganga ili kumpoteza akili Raymond akumbuke tu mapenzi tuliyokuwa nayo badala
yake karudi palepale kumpenda huyo kijakazi mnuka mikojo…mimi ni mzuri kuliko
huyo Angelina…tena ni mzuri mbali sana mimi nafaa kuolewa na Ray kwanza
tunaendana(anafyonza)huyu mjinga kaja
kuniharibia ndoto zangu..mimi niliumbiwa kuishi maisha mazuri na mwisho wa siku
natakiwa kuishi hayo maisha na hakuna mwenye mamlaka ya kuishi maisha
niliyoyaota…ni kweli nampenda sana Peter ila Raymond ndo mwanaume pekee
atakayenipa maisha nayoyataka
(Angelina anapita akiwa anatokea sokoni)
Christina: ona anavyojifanya wife material…(anafyonza)namkanyaga namtoa utumbo leo
mshenzi huyu… (anawasha gari na kwa
mwendo kasi analiondoa gari na kumfuata Angelina)
Angelina:(analiona gari linakuja kwa kasi sana
anapiga kelele) mama…
Raymond:(amesimama
karibu na geti anatoka anakimbia) nini?
Christina:(anakanyaga
breki na kulisimamisha gari ghafla)
Angelina:(anaogopa
sana)
Christina: shenzi sana…nitakuua una bahati sana
huyo bwana wako ametoka kwa wakati ningekutoa utumbo…(analirudisha gari nyuma kisha anaondoka)shit!!!Raymond anampendea
nini huyu mshenzi (anafyonza)yaani
anataka kumuoa halafu mimi ameniacha pamoja na juhudi zote nazofanya ili
kumfanya awe mume wangu lakini ameona aniache(anaendesha gari kwa hasira)lakini mimi ndo Christina…nisipoolewa na
Raymond nitaolewa na Desmond yaani hawa baba na mwana nina usongo nao hawa
hawajui tu…na siwaachii hivihivi nitamroga Desmond kama nilivyomroga Raymond
lakini dah Raymond nimemroga imebuma yaani ana mizimu mikali huyu(anaendelea na safari)
(upande wa Raymond na Angelina)
Raymond: nini wewe mbona huongei?
Angelina: lile gari lililoondoka hapa lilitaka kunigonga
Raymond:ni la nani unamjua?
Angelina: hapana simfahamu…
Raymond: sasa mbona alitaka kukugonga kama ana
uadui na wewe?
Angelina: mimi sijui dear…
Raymond:(kwa Ramadhani)
wewe kaka…umeliona hili gari na labda unalijua?
Ramadhani: gari gani boss?
Raymond: halafu usiniite boss bwana
Ramadhani: mi nimeona umesahau ndo maana nikaanza
kufanya Kama nilivyokuwa nafanya zamani
Raymond: kufanya nini?
Ramadhani: kukuita boss
Raymond: naomba usiniite boss…yaani sipendi Sana
Ramadhani: najua hupendi…
Raymond: umejuaje
Ramadhani: ndivyo ulivyo siku zote boss
Raymond: anyway sawa…by the way umeliona hilo gari?
Ramadhani: gari gani boss
Raymond: lililotaka kumgonga mke wangu?
Ramadhani :( analikumbuka)
lile (anajisemea moyoni) si la Christina
lile na aliyekuwa anaendesha ni Christina
Raymond: mbona hunijibu, Rama?
Ramadhani: sasa boss wangu mimi nitajuaje huku wote
tulikuwa ndani tumetoka tu mara baada ya kumsikia Angelina anapiga kelele
Raymond: nina uhakika ulimuona hata kwa mbali…maana
hata mimi nimemuona ila sijamtambua
Ramadhani: sasa wewe boss hujamuona vizuri mimi ndo
naanzaje kumuona vizuri…
Raymonda: anyway, tuachane na haya…kikubwa kwamba
wife hajaumia…ungeumia na mimi ningeumia sana… (Kwa Angelina) twende ndani mpenzi
Ramadhani: wacha we…
Raymond: naomba unitafutie msichana wa kazi huyu
anatakiwa apumzike awe wa kukaa ndani…
Ramadhani: usijali boss ake…nitakuletea msichana
nitamtoa kijijini kwetu
Raymond: sawa utakuwa umenisaidia sana… (Kwa Angelina) kabla hajaja huyo binti
nitakuwa nakupeleka mimi na kukurudisha kila unapotaka kwenda popote mpenzi
maisha yako hayako salama kabisa mpenzi
Angelina: unatakiwa uwe unaenda kazini
Raymond: sawa...Najua mama na baba wameniambia
niende hospitali ila mimi sio dokta…bado
Angelina: dear…wewe ni daktari tayari mbona muda sana
tangu umekuwa dokta
Raymond: Kama unaniambia wewe labda naweza kuwa ni
daktari kweli
Angelina: wewe ni daktari na ni mchumba wangu
Raymond: nafurahi kuwa mchumba wako baby
Raymond: wow…Nina bahati Sana kuwa na mchumba mzuri
kama wewe
Angelina: Asante dear
Ramadhani :( anaguna)
mapenzi shatashata… (Anaguna tena)
Raymond: twende ndani… (kwa Ramadhani) usisahau na dereva maana mimi nitakuwa naenda
kazini sitaki ataembee kwa miguu utasema sio mke wa Raymond Desmond Bembele
Ramadhani: sawa boss…nitawatafuta
Raymond: nikupe siku ngapi…maana nataka kuanza
kufanya kazi mwenzio…
Ramadhani: mfanyakazi hata ukinipa hela leo kesho
anakuja
Raymond: poa muite basi…aje na awe ana tabia nzuri
Ramadhani: sawa boss wangu
Raymond: niite Raymond
Ramadhani: sawa Raymond
Raymond :( anacheka)
haya endelea na kazi zako sasa
Ramadhani: sawa Raymond…
(Raymond na Angelina wanaingia ndani)
Angelina:(anaingia
ndani huku anajisemea moyoni) Raymond anajitahidi kunipoteza mawazo ya mimi
kunusurika kifo ila ukweli ni kwamba siwezi kusahau na ni nani alitaka kuniua
leo kwa kunigonga gari? je ni Christina labda kwasababu ya wivu au ni nani? (anaguna)hii nalo ni janga na ninatakiwa
kuwa makini sana
Raymond :( amemshika
mkono Angelina) vipi mbona umepoa?
Angelina: wala, mi mbona nipo sawa tu?
Raymond: nakupenda Sana Angelina natamani nikuoe
hata sasa hivi
Angelina :( anacheka)
hata mimi natamani hata sasa hivi niwe mkeo
Raymond: nitaenda kutoa mahari mpenzi, sijawahi
kupenda mwanamke Kama navyokupenda wewe, sijui umenipa nini
Angelina: (anacheka)
Raymond bwana, sawa ILA familia yangu itakukaribisha kwa mikono miwili na pia
hata mimi sijawahi kupenda mwanaume kama navyokupenda wewe
Raymond: eti ee
(Wanacheka kisha wanaingia ndani)
Ramadhani:
maisha haya…hausigeli anatafutiwa hausigeli… (Anaguna) kimasihara Angelina kampiku Christina (anacheka sana) sasa hausigeli kawa ‘mazahausi’ duh!!!dunia ina
mambo hii…ila Raymond kama kachanganyikiwa
0 Comments