SCENE 48: -
(Edmond
pamoja na Catherine wanafika nyumbani kwa Raymond wakiwa na shauku ya kujua
yaliyomkuta Raymond kuhusu yeye kupoteza kumbukumbu na mambo mengine)
Edmond:(anagonga
hodi)
Angelina:(anafungua)
karibuni (huku anapiga magoti)
shikamoo shemeji…
Edmond: marahaba…shem hujambo
Angelina: sijambo (kwa Catherine) shikamoo dada
Catherine: marahaba hujambo
Angelina: sijambo…karibuni (anawaongoza njia) karibuni
Edmond: asante…simuoni Mond….
Angelina: yupo sebuleni…
Edmond:(anaelekea
sebuleni)
Raymond:(amelala)
Edmond:(anamuamsha)
wewe vipi unaumwa…
Raymond:(anashtuka)
ah…(anakaa)nambie
Edmond: wewe umekuwaje? mbona hata kazini huendi?
Raymond:mi bado mwanafunzi bwana…yaani Angelina
ameshinda siku nzima ananiambia kwamba mimi ni daktari na inanipasa niende kazini
yaani simuelewi unajua
Edmond: una shida gani Raymond kwanini kama akili
yako imebaki nyuma sana...kuna mambo mengi sana yametokea…wewe tayari
umeshamaliza elimu yako na tayari wewe ni daktari…baba yako kakupa ofisi wewe
ndo daktari mkuu, na pia umepewa nyumba gari ina maana hukumbuki vyote hivyo?
Raymond: sina kumbukumbu
(Angelina na Catherine wanafika mahali hapo)
Edmond: nini kilikutokea wakati upo Serengeti?
Raymond:(anamuangalia
usoni) Serengeti nilienda lini?
Angelina:(anasikitika)
Edmond:(kwa Angelina)
nini kilitokea wakati mpo Serengeti?
Angelina: hamna kitu shem…tulikaa huko tukafurahia
maisha na wala hakuna ambacho kilikuwa kimeharibika wala kuonekana
kuharibika…tatizo lilianza kesho yake mara baada ya sisi kurudi ndo nikawa
nikimpigia simu hakumbuki mimi ni nani na pia dada pendo na Rachel na wao
wakasema hawamuelewi asubuhi alienda vizuri ila mchana eti akawasahau
Edmond:au kachezewa maana kama hakujigonga sehemu...na
kama ingekuwa hivyo angeumwa kichwa
Catherine: atakuwa amerogwa
Edmond:na nani lakini?
Catherine: inaweza ikawa mtu labda anayetaka
akumbuke mambo ya nyuma ili labda awe karibu nae
Edmond: Duh hii mpya na hatari kwa mantiki hiyo mtu
pekee ambae anaweza kumfanyia hivyo Mond ni Christina ndo ambae anatamani kuwa
na Raymond na yuko tayari kufanya chochote ili ndoa iliyokuwa ikisubiri
itimie…yes ni Christina inaleta maana…
Catherine: cha kushangaza sasa pamoja na yote mbona
Raymond anataka kumuoa Angelina?
Edmond: moyo…kilichotumika ni moyo
Raymond; yaani hata siwaelewi mnajua…
Catherine: tumuite mchungaji...amuombee huyu mtu la
si hivyo atakuwa kichaa mnaonaje?
Angelina:ni kweli
Edmond:ni kweli ni mchungaji pekee ndo ataweza
kutatua hili au tumpeleke kwanza hospitali
Angelina: wazazi wake walitaka wampeleke hospitali
ila sijui ikawaje
Edmond: labda na wao wameona kuwa itakuwa ni nguvu
za giza ndo zimefanyika hapa
Catherine: labda
Raymond: Mond…bora umekuja ndugu yangu tunaenda
lini kwa ndugu zake huyu mrembo nimuoe mimi fasta
(Catherine, Edmond na Angelina wanaangaliana)
Edmond: tutaenda tu Mond
Raymond: haya mimi nalala bana… (ananyanyuka na kwenda zake ndani)
Edmond:au anajifanyisha
Catherine: ili iweje? huyu kweli amepoteza maana
hata alivyo hayupo kawaida kabisaaa
Angelina: yaani mimi nimeshachanganyikiwa
Edmond: wala hata usijali Mungu yupo…
Catherine: Christina nae ni king’ang’anizi yote
kamuharibu mtoto wa watu ilia pate hiyo ndoa jamani hajui kuwa ukiachwa inabidi
uachike?
Edmond: yaani hachoki ameshawahi kusingizia mpaka
mimba ili ampate Raymond sasa Raymond mwenyewe alivyo mtata (anaguna)
(Wanacheka)
Catherine: atakuwa poa tu siku sio nyingi…
Angelina: unajua yaani inashangaza mtu mlikuwa nae
vizuri tu jana yake eti leo hakumbuki kitu kabisa…yaani mara ya kwanza alienda
kwao akalala, akarudi kesho yake yaani akawa hata anikumbuki
Catherine: ila akawa anakupenda
Angelina:ee…yaani mpaka nikashangaa
Edmond: moyo…mama yaani na amekupenda…pamoja na
kwamba kichwa chake hakikukumbuki ila moyo wake unakumbuka kuwa uliwahi
kukupenda na bado anakupenda
Catherine: una bahati binamu
Angelina:(anacheka)
Edmond:(kwa Catherine)
kama ninavyokupenda wewe
Catherine:(anacheka)
Edmond: kabla hamjafunga ndoa wewe na Raymond mimi
na Catherine tutafunga ndoa…kila kitu tayari mpaka siku ya ndoa imeshapangwa…
Angelina:(kwa
Catherine) hongera binamu
Catherine: asante…(anatabasamu)
Edmond: sema ndo hivyo mshenga wangu ndo
kachanganyikiwa hana hata kumbukumbu na suala la kukutolea mahari wewe Angelina
lilikuwa limepangwa kimyakimya
Catherine: dah…Christina katuharibia kweli maana ungeshangaa
send off tu, yaani kila mtu alikuwa amejipanga mahali pake sio baba yake Raymond
na ukali wake ule na sio mama Raymond na ule upole wake
Angelina:(anacheka)
jamani
Catherine: ila usijali kila kitu kitakaa sawa wewe
shukuru tu kuwa bado upon ae basi mengine mkabidhi Mungu atakutendea
Angelina:(anatabasamu)
amina
Catherine: wewe nae tumekaa hapa muda wote jamani hata
maji…Loh!!
Angelina: jamani nimesahau
Edmond:(anacheka)
anamuawaza baby…baby mwenyewe sasa kulala…utasema kalogewa hapo
Catherine: anapenda kulala ee
Angelina: vibaya sana (anaenda jikoni na baada ya sekunde kadhaa anakuja amebeba glasi za
juisi na maji anawapa Catherine na Edmond kisha nay eye anachukua moja)
Edmond: atakaa vizuri tu usijali
(Wanakunywa vinywaji huku wanaendelea na maongezi
ya hapa na pale)
Catherine:
Muamini Mungu mdogo wangu
0 Comments