SCENE 49: -
(Majira ya
saa saba usiku Christina anafika nyumbani kwa mganga aliyemtengenezea dawa ya
kumpoteza kumbukumbu Raymond)
Christina:(anagonga
kibandani) uncle
Mganga:(anaamka)
naam… (anafungua mlango) wewe nini
usiku huu
Christina: nina mazungumzo na wewe
Mganga:(anatoka)
sasa ndo uje usiku? (anatoa kiti nje)
haya karibu uketi (anapiga miayo) ah
yaani ni usiku kweli
Christina:(anakaa)
Mganga: enhe niambie
Christina: ah…sina mengi ya kukuambia
Mganga:(anamsikiliza
kwa makini)
Christina: naomba ile dawa uitengue
Mganga:(anamuangalia
usoni) kwanini?
Christina: ah haijafanya kazi kama nilivyo tegemea
Mganga: kivipi?
Christina: yaani hata hanipendi kama ilivyokuwa
bado anampenda yule dada niliyekuambia
Mganga:(anacheka
kidogo) ila mimi si nilikuambia?
Christina:(kimya
huku anaangalia chini)
Mganga: yeye na yule dada wanapendana kweli…na hata
tukifanyaje wataishia pamoja
Christina:(anaangalia
chini) yaani nimepoteza muda…na mimi nimegundua kuwa wanapendana ingawa
inaniuma sina budi kukubaliana nalo...na mimi naogopa kuishia vibaya anko
Mganga: ndo hivyo…usije ukaishia vibaya mwanangu...
Christina:(anavuta
pumzi ndefu) mimi na Raymond tumetokea mbali sana
Mganga: najua…na mara nyingi ulikuwa ukigombana nae
unakuja nakutengezea mnapatana
Christina: ila sasa huyu msichana wake wa kazi
amekuja kupoteza kabisa uwezekano wa mimi nay eye kuwa pamoja isije ikawa kesi
naomba tu uitengue…najua inauma kumkosa Raymond
Mganga: kwani unampenda sana?
Christina: hapana...nimemzoea tu
Mganga: basi mpe nafasi aishi maisha yake maana
hata yeye anajua kabisa kuwa wewe humpendi hata kidogo nan do maana mara nyingi
alikuwa anakukwepa na alipopata nafasi ya kupenda amependa kwa moyo wake wote
na akili yake yote inamfikiria huyu mwanamke
Christina: naelewa anko kuwa anampenda sana
msichana wake wa kazi
Mganga: ngoja tuitengue dawa (anaingia kibandani mwake na baada ya dakika kama kumi anatoka akiwa na
vifaa vyake kama vibuyu n.k) sasa tuanze kazi…kwanza zile nywele
tulizochimbia tuzifukue…tuzichome moto
Christina: sawa
Mganga: fanya wewe maana hata mara ya kwanza
ulifanya wewe
Christina:(anachukua
jembe lililopo pembeni yake na kufukua nywele za Raymond)
Mganga:(anaongea
maneno Fulani kwa sauti ya kunong’oneza)
Christina:(anachukua
nywele za Raymond na kuzitupa mbali)
Mganga :( anaongea
lugha za kiganga huku anataja jina la Raymond)
Christina:(amesimama
kinyonge)
Mganga:(anamalizia
kwa kuvunja chungu alichopikia dawa na kumwaga dawa waliyompulizia Raymond siku
wanampoteza kumbukumbu)
(upande wa Raymond,
amelala kitanda kimoja na mpenzi wake lakini ghafla anasisimuka mwili na kupiga
kelele ya ajabu, inayomshtua Angelina)
Angelina:(anakemea
kwa jina la Yesu kristu wa Nazareth)
Raymond:(jasho
linatiririka)
Angelina: asante bwana Yesu (kwa Raymond) ni nini?
Raymond:(anatulia)
sijui…(anamkumbatia)malaika
Angelina:(anakumbuka
kuwa ni jina alilokuwa anapenda kumuita) hili jina si alikuwa ananiita
kabla hajapoteza kumbukumbu
Raymond:(anacheka)
kwani bado tupo Serengeti?
Angelina: kwanini?
Raymond: tumelala wote
Angelina: asante bwana Yesu amekumbuka…
Raymond: nini?
Angelina: hapana tumesharudi nyumbani
Raymond: nakupenda Sana Angelina
Angelina: nami nakupenda Sana Raymond…hatimaye umekumbuka
Raymond: kwani nilikuwa nimesahau?
Angelina: acha tu…tulale nitakusimulia kesho
asubuhi
Raymond: yaani nimetoka jasho utasema nilikuwa
nalima
Angelina: pole Mungu wetu hashindwi
Raymond: hakika…
(wanajifunika kisha wanalala)
Raymond: bwana nimekuambia nasikia joto
Angelina: pole (anamfunua)
Raymond:(anasinzia)
Angelina: lala…
(upande wa Christina na mganga)
Mganga: basi kwa kufanya hivi huko alipo anaweza
akawa amesharudisha akili na kumbukumbu zake
Christina: asante sana
Mganga: kwa mara ya kwanza tangu nimejua kufanya
dawa sijawahi kuona mwanamke mwenye busara kama wewe
Christina: kwanini?
Mganga: hii dawa ni kali sana, siku ingebuma
ungekuwa chizi
Christina: nimshukuru shangazi yangu ambae yeye ndo
alinikaribisha katika ulimwengu wa dawa lakini yeye ndo amekuwa chachu ya mimi
kujitoa kwenye huu ulimwengu…aliniambia hasara za kung’ang’ania ambapo hakuna
mapenzi nilitafakari sana nikaona ni kweli ndo maana unaona leo nimekuja
kutengua dawa na kumuacha huru. Raymond alipenda sana pamoja na kwamba
tumeachana basi tuwe marafiki ila mimi nikaona itakuwa hasara kwangu Raymond
akiwa rafiki tu
Mganga: umefanya jambo jema
Christina: Asante sana anko
Mganga: haya safari njema
Christina: unanifukuza?
Mganga: hapana
(wanacheka
kisha wanaagana)
Mganga: haya mama uwe unanikumbuka
Christina:(huku
anaanza kuondoka) usijali… (anaondoka
zake)
Mganga:(anaingia
ndani)
0 Comments