SCENE 6: -
(Majira ya
saa moja na nusu usiku,Mr.Bembele na mkewe wanafika katika jumba la kifahari la
mtoto wao wa pekee na mpendwa Raymond,wanapiga honi na haraka mlinzi anafungua
geti hilo wanaingiza gari lao la
kifahari kisha wanaliegesha katika sehemu maalumu ya maegesho nyumbani
hapo,wanashuka kwenye gari,mama Raymond anamsalimia mlinzi huku Mr.Bembele
akionyesha kutojali uwepo wa mlinzi huyo,mara baada ya salamu ya mama Raymond
kwa mlinzi huyo wanaingia ndani ambako wanafunguliwa mlango na Raymond)
Mrs.Bembele: wow…mtoto wangu hujambo baba?
Raymond :(
huku anawaongoza kwenda ndani) sijambo mama shikamoo…
Mrs.Bembele: marahaba mziwanda wangu
Raymond :(
anacheka huku anamgeukia baba yake) shikamoo baba
Mr. Bembele: marahaba baba hujambo?
Raymond: sijambo, karibuni jamani (anaelekea jikoni baada ya sekunde kadhaa
anarudi akiwa amebeba juisi glasi tatu
kwenye trei) karibuni (anatenga juisi
hizo)
Mrs.Bembele: Asante baba (anatabasamu kidogo kisha anakunywa kidogo)
Mr. Bembele: hii nyumba inahitaji mwanamke, mwezi
wa sita si uje haraka uoe, umuoe mwanamke wako jamani au aje aishi hapa
Raymond: hapana
Mrs.Bembele: unahitaji msichana wa kukusaidia kazi
za hapa na pale
Mr. Bembele: wa kazi gani? Christina aje aishi hapa
hata kama hamjafunga ndoa
Raymond :( amekaa
pembeni ya mama yake) hata kama Christina akija kuishi hapa msichana wa
kazi ni lazima maana hajui chochote hajui kupika hata chai
Mr. Bembele: mvumilie tu si ndo kipenzi chako
Raymond: baba…mi wala simtaki tena Christina
Mrs.Bembele :(
anamkonyeza)
Mr. Bembele: baba unatania eeh
Raymond :( anajichekesha) natania dad… (Anamuangalia mama yake)
Mr. Bembele: kidogo nishangae unamkataa mwenzio
kisa hajui kupika huku hata wewe hujui kupika
Mrs.Bembele; hivi nani huwa anakupikia?
Raymond; rafiki yangu huwa akija ndo huwa
ananipikia lakini huwa ananifundisha pia
Mrs.Bembele :( anacheka)
sipatii picha mnavyojipikilisha kinatokaga kweli chakula cha kueleweka hapo
kweli
Raymond; we acha mama halafu mwenyewe huwa ana
mtindo wa kujisifia huyo
Mr. Bembele: mnamuongelea nani hapo?
Raymond: rafiki yangu Edmond
Mr. Bembele: huwa ni mtoto wa nani?
Raymond: wazazi wake walishafariki
Mr. Bembele: nay eye ana kazi gani?
Raymond: huwa ni mwalimu…wa shule ya msingi?
Mr. Bembele: na wewe ni nani?
Raymond: mimi ni dokta
Mr. Bembele: ilikuwaje ukawa na urafiki na mwalimu?
Raymond :( anaanza
kuchukia) dad
Mr. Bembele: sio dad…halafu nakumbuka kuwa
nilishakuambia kabisa kuwa sitaki uwe na urafiki na kijana ambae hana pesa,
anachokifata kwako mwanangu ni hizo pesa zako otherwise asingekuangalia na
kuanzisha urafiki na wewe, wanafata pesa mwanangu
Mrs.Bembele: baba Raymond...
Mr. Bembele: sio baba Raymond hapa, mwanangu
nimemlea kwa shida sana, halafu leo aje awe na urafiki na mwalimu wa shule ya
msingi yaani hamuendani hata kidogo na anachotaka yeye ni pesa zako
Raymond; enough dad...
Mrs.Bembele: tafadhali jamani msianze kugombana Kama
ilivyo kawaida yenu
Raymond: mama, mimi na dad hatuwezi hata siku moja
kupatana kutokana na kwamba mawazo yetu hayako sawa… (anamuangalia baba yake) nachukia dad unavyokuwa unawasumbua na
kuwasema vibaya maskini, utasema nao sio watu, inaniuma sana, maskini nao ni
watu dad tena watu walioumbwa na Mungu, hawakupenda kuwa hivyo…na pia dad
tuliumbwa ili tusaidiane ili Mungu ajitwalie utukufu wake, embu tafakari dad
kama wote yungeumMra matajiri nani angemsaidia mwenzie? Mungu katuumba hivyo
ili tuhudumiane
Mrs.Bembele :( anatikisa
kichwa kuonyesha kuwa anakubaliana na alilosema Raymond)
Mr. Bembele: umaskini ni dhambi na pia ni laana,
ndo maana hata maskini wanachukia laana hiyo na mwisho wa siku wanaona sasa
watumie watu wengine kujinufaisha
Raymond; siwezi kubishana na wewe maana hata hivyo
akili yako umeshailazimisha iamini kuwa sisi matajiri ni lazima tuchangamane na
matajiri wenzetu na maskini wafanye hivyo hivyo ya kwamba wachangamane na
maskini wenzao halafu mwisho wa siku Mungu atajitwaliaje utukufu wake?
Bembele: ongea yote Raymond ila tu elewa kuwa ni
lazima uachane na huyo sijiui nani
Raymond: siwezi dad...
Mr. Bembele :( Kwa
hasira huku anatoka nje) wewe naona unataka kunipanda kichwani yaani mimi
kama baba yako nakwambia ninayoyaona wewe unajifanya kidume huyo Edmond hajawaoana
walimu wenzake mpaka aje kwako?
Raymond: sasa dad…hiyo inakuwa sio vizuri ukifanya
hivyo hata yeye ni mtu baba nay eye anahitaji mapenzi ya kweli na si hivyo
tunavyofanya dad
Mr. Bembele: wewe mtoto Mimi nakupenda na
nimekuonyesha kila kitu kuonyesha hayo ila unaona haitoshi, nikupendeje?
Raymond: hapo dad…you are blackmailing me…unanifanyia
hivi vyote halafu mwisho wa siku niendeshe? Baba Mimi ni mwanao na sio mtumwa
wako, sio kwasababau umenipa nyumba nzuri na gari la kutembelea ndo unaweza
kunifanyia chochote nikanyamaza,
Mrs.Bembele: naomba muache ugomvi jamani angalau
nisikilizeni mimi
Mr. Bembele :( anamshika
mkewe mkono na kumvuta nje) twende mke wangu naona mtoto wetu tayari
keshachotwa akili na huyo rafiki yake
Raymond: sio kuchotwa akili dad…naongea uhalisia
Mr. Bembele :(
anaondoka yeye pamoja na mkewe)
Mrs.Bembele:(anajifanya
kuwa kasahau kitu hivyo anarudi ndani) mwanangu Raymond nakupenda baba na
ninakubaliana na wewe kwa kila kitu mtoto wangu, nachokuomba mimi kama mwanamke
niliyekuzaa baba usiwe unagombana na baba yako mwanangu
Raymond:mama,upo kama hukusikia maneno mabaya
aliyokuwa anaongea juu ya Rafiki yangu Edmond,mama siwezi na wala sitaki kusikia
mwanadamu yoyote anasemwa vibaya na yoyote atakayemsema vibaya mwanadamu
mwenzie mbele yangu basi ni lazima nimueleweshe,hata ikiwa baba yangu
mzazi,mama sisi ni mavumbi wote iwe tajiri iwe maskini sisi wote ni mavumbi,na
mavumbini tutarudi sasa sio kwamba Mungu ametusaidia tuna maisha mazuri ndo
tudharau na kuwatenga ambao wana maisha duni yaani hayo malezi siyawezi na wala
sikubaliani nayo
Mrs.Bembele: unajua hata Mimi baba siyakubali hayo
mawazo aliyo nayo baba yako, ila sasa ndo tutafanyaje ndo kichwa cha familia
yetu
Raymond: kwahiyo mama wewe unatakaje? Niachane na
Edmond?
Mrs.Bembele: hapana mwanangu
Mr. Bembele :( sauti
kutoka nje) hicho ulichosahau kimeota mabawa kimeruka au, embu twende
nyumbani
Mrs.Bembele :(
Kwa Raymond) nitakupigia simu baadae mwanangu nakupenda
Raymond: nakupenda pia mama
(Haraka anatoka nje alipo mume wake anapanda kwenye gari kisha Mr.
Bembele analiwasha gari na kwa mwendo wa kasi wanaondoka mahali hapo, huku
ndani alipo Raymond nae kuingia chumbani kwake ili apumzike)
Raymond:
mimi siwezi kubadilisha mawazo niliyowekewa na mama yangu tangu nipo mdogo kuwa
sisi sote ni ndugu maana tuliumbwa na Mungu mmoja…(anapanda kitandani anachukua rimoti anawasha runinga kisha anajilaza)nampenda
na kumheshimu mzee wangu ila siyaheshimu mawazo yake,halafu baba bwana kwahiyo
kanipa vyote hivi ili anaiendeshe,yaani nifanye anachotaka,kweli baba yangu ana
akili mbovu sana yaani hata mimi mwanae wa kuzaa anaonyesha ubabe?(anajigunia mwenyewe huku anaendelea kupekua chaneli kwenye runinga )
0 Comments