SCENE 53: -
BAADA YA MWEZI MMOJA
HARUSI YA EDMOND NA CATHERINE
(usiku mwingine wa furaha sana kwa Edmond na Catherine maana ni usiku
ambao wanasherekea muungano wao mara baada ya kuunganishwa mbele ya Mungu na
wanadamu,kabla ya maharusi kuingia wanaanza kuingia watu ambao ni karibu sana
na maharusi hao.Miongoni mwao ni wazazi wa Catherine na baada ya wazazi wa
Catherine wanaingia Mr.Bembele na Mrs.Bembele,na kwa mara ya kwanza baada ya
kuchumbiwa Christina anaingia na mchumba wake,wamependeza sio mchezo,na baada
yao ni Raymond na Angelina wanaingia,wamependeza sana Raymond amevaa suti yenye
upindo wa zambarau na Angelina amevaa gauni refu linalomshika umbo vyema nay
eye ni rangi ya zambarau.)
Raymond :(
anamuona Christina na Peter) baby...Twende tukawasalimie…kina Christina
Angelina :(
akiwa amejipamba amepambika anamfuata nyuma mchumba wake)
Raymond :(
anawafikia) mambo zenu
Christina: nzuri mwenyekiti wa kamati
Raymond: acha tu ndugu yangu
Peter:(anacheka)
mambo vipi? (anampa mkono)
Christina:(anamuona
Angelina) wow…jamani katoto kamependeza
Angelina :( anatabasamu
kidogo) shikamoo (anapiga magoti)
Christina: marahaba mama hujambo?
Angelina: sijambo (Kwa Peter) shikamoo
Peter: marahaba hujambo
Angelina: sijambo…
Christina: wow…mmependeza Sana
Raymond: hata nyie…
Christina: by the way…unamjua mchumba wangu (anamshika Peter)
Raymond: yeah…tunajuana
Christina: mlijuana wapi?
(Raymond na Peter
wanacheka)
Christina: mlijuana wapi?
Raymond: kitaa tu kwenye harakati za maisha
(Wote
wanacheka)
Raymond: mmefurahi…kweli kuwaona…Mimi namjua Peter
na Peter ananijua ila tu hamjui mchumba wangu
Angelina :( anatabasamu)
Raymond :( anamshika
bega Angelina) huyu ndo mke wangu mtarajiwa…anaitwa Angelina
Christina: tunamjua
Raymond: unamjua wewe…Peter hamjui
Peter: namjua…Christina alikuwa anapenda kumuongelea
(Wote
wanaangua kicheko)
Christina: yaani nyie maisha dah!!
Angelina :(
anatabasamu)
Raymond: Ni safari ndefu
(Wazazi wa Christina na wa Raymond wamekaa pamoja na wanawaangalia
watoto wao wanaoonekana kuwa katika wakati mzuri pamoja)
Raymond: njooni tukae tusije tukaanguka… (Anamuita mhudumu) tafadhali naomba
utuletee vinywaji
Christina: hongera umeipigania harusi ya rafiki
yako mpaka imekuwa bwana
Raymond: si unajua tena ananichukulia kama ndugu (anamuwekea Angelina nguo vizuri)
Christina: yaani kuanzia kanisani mambo yalikuwa
mambo na picha, vinywaji, chakula nyumbani kila kitu kipo safi…hongera sana
baba
Raymond: Asante (anatabasamu)
(Mhudumu anawaletea vinywaji)
Christina: sasa mbona sherehe haina pombe jamani
Peter: wewe pombe ya nini?
Raymond: harusi ya walokole hii…
Mc: habari za jioni mabibi na mabwana…
(Watu wanaitikia)
Mc: karibuni sote kwenye hafla ya kuwapongeza
Edmond na Catherine ambao leo mbele yetu na mbele za Mungu wameunganishwa na
Mungu na kuwa kitu kimoja yaani wanandoa...Anayewakaribisha ni mimi MC mazoea
karibuni sana… (Kimya kidogo) basi
baada ya utambulisho mfupi sasa tuwakaribishe maharusi waingie ukumbini
(Muziki mkubwa unapigwa)
Mc: karibuni…Dj fanya yako
(Ma-brighter wa kiume na kike wanaingia wakiwa wanacheza kwa mbwembwe
zote huku watu wakiwashangilia kwa shangwe nyingi)
Christina :( anamuangalia
Angelina aliyekaa pembeni yake) unaonekana unapenda sherehe
Raymond :( anadakia)
anawaza nyama tu…anapenda nyama huyu anafurahi maana anajua kuna nyama mwisho
wa yote anajua lazima tukale vyuku (anacheka)
Angelina: anakudanganya…
(Wanacheka)
Mc: baada ya mabrighter sasa matron na best man
wanaingia...Dj
(Matron na
best man wanaingia kwa mbwembwe zote huku watu wakiwashangilia, wanacheza kwa
muda kisha wanafika mbele ya kadamnasi)
Mc: sasa…mabibi na mabwana tukae tayari kabisa kwa
ajili ya kuwaruhusu malkia na mfalme wa usiku huu…Edmond na Catherine
(Watu
wanapiga makofi na meza inayoonekana ina shangwe kuliko zote ni meza waliokaa
kina Raymond tena ya mbele kabisa)
Mc: Dj…niletee maharusi wetu
(Watu
wanasimama huku Catherine anaingia akiwa amependeza sana gauni lake lenye mkia
mrefu limebana vyema umbo lake, anaingia akiwa anacheza kwa madoido na kuringa
na anaonekana kutambua kuwa ile ni siku yake na sio siku ya mtu mwingine...Baada
ya muda mumewe akiwa na furaha sasa kumzidi mke anaingia kuungana na mkewe na
wanacheza kwa madoido na watu wanafurahishwa sana na mpangilio huo wa uingiaji)
Edmond :( anaangaza
macho huku macho yake yanamtafuta Raymond na anapofanikiwa kumpata anamuonyeshea
ishara ya kumshukuru kwa yote)
Raymond :(
Kwa sauti ya kunong’oneza) usijali
(Maharusi hao
wanacheza Kwa furaha nyingi wakielekea mbele walipo matron na best man, baada
ya hatua chache hatimaye wanafika mbele kabisa, wanapofika mbele mziki unazimwa
ghafla)
Mc: Asante Sana... (Kwa maharusi) wow…mmependeza na mmeingia kwa mbwembwe
(Watu
wanacheka)
Mc: nimependa…anyway… (Kwa watu) makofi tena na vigelegele kwa maharusi wetu jamani
(Watu wanashangilia)
Mc: utambulisho…sasa Kama bibi harusi una aibu
tuambie mapemaaaaa
Catherine :( anachukua
kipaza sauti) sina aibu
Mc: kweli…
Edmond :(
anacheka)
Mc: haya Anza kutambulisha…
Catherine :( Kwa ujasiri) asanteni wote…naomba
kwanza niwasalimu kwa jina la Bwana
(Watu wanaitikia)
Catherine: napenda kuwatambulisha wazazi wangu baba
na mama…naomba wasimame na muwapungie watu mikono
(Wazazi wanasimama)
Catherine: kaka zangu na mawifi zangu
(Makaka na ma wifi wanasimama na kuwapungia mikono)
Catherine: wadogo zangu wote tuliozaliwa tumbo moja,
watoto wa baba zangu wakubwa, wadogo naomba msimame muwapungie watu mikono
(Wadogo zake ambao ndo wengi wao akiwemo Angelina wanasimama na kupungia
watu mikono)
Catherine: mwisho kabisa ninamtambulisha mume wangu,
ubavu wangu, chaguo la moyo wangu na namshukuru kwa kunichagua mimi kuwa mkewe
na mama wa watoto wake
(Watu
wanashangilia)
Catherine: Mr. Edmond Mutalemwa…
Edmond :( anamkumbatia
mkewe)
Mc: safi kumbe kweli bibi harusi huogopi haya zamu
yako sasa bwana harusi…utaweza
Edmond: naweza…
Mc: haya muombe mkeo kipaza sauti sio unampokonya
kibabe…ichukue taratibu halafu tutambulishe
Edmond :( anafanya
kama alivyoambiwa na Mc) asanteni bwana Yesu asifiwe…
(Wanaitikia)
Edmond: asalama le kum
(Wanaitikia)
Edmond: tumsifu yesu kristu
(Wanaitikia)
Edmond: kwanza kabisa … (anajisikia uchungu ghafla)
Catherine :(
anamshika bega kumpa moyo)
Edmond: natamani kuwatambulisha wazazi wangu lakini
kwa bahati mbaya wametangulia mbele za haki
Watu: oh maskini…
Edmond: lakini ninao wazazi walionisimamia mpaka
Leo hii nimefanikisha kumuoa mwanamke wa ndoto zangu Mr na Mrs.Bembele nyinyi
ni wazazi wangu naomba msimame muwapungie mikono
Raymond :(
anafanya utundu Kwa kumzomea mama yake)
(Mr & Mrs.Bembele wanasimama na kuwapungia watu mikono)
Edmond: asanteni Sana…kaka zangu na mashemeji zangu
wote…naomba msimame muwapungie watu mikono
(Makaka
pamoja na mashemeji wanasimama na kuwapungia watu mikono)
Edmond: wadogo zangu…Mimi kwetu ndo wa mwisho ila
nina mdogo wangu wa nguvu…Mr. Raymond Bembele naomba usimame uwapungie watu
mikono
Raymond :( akiwa
anatabasamu anasimama na anapungia watu mikono)
(Shangwe nyingi zinatawala ukumbini hapo ishara ya kuonyesha kuwa Raymond
ni mtu wa watu)
Edmond :( anacheka)
nimefurahi ukumbi umelipuka Kwa shangwe
(Shangwe zinalipuka tena)
Raymond :(
anacheka)
Edmond: mwisho kabisa napenda kumtambulisha mke
wangu mpenzi…. wa ubavu, asali wa moyo wangu, panado yangu
Catherine :( anacheka)
panado
Edmond: Mrs. Catherine Edmond Mutalemwa
(Shangwe zinalipuka)
Mc: Asante Sana…Kwa utambulisho
(Sherehe inaendelea huku matukio yanaenda jinsi yalivyopangwa, watu wanaserebuka,
wahudumu nao wanajitahidi kugawa chakula na vitafunwa mbalimbali, muziki
unapigwa na kuna burudani mbalimbali zinaendelea, sherehe imefana sana na kila
mtu anaonekana kufurahi sana kwa usiku huo. muda wa zawadi unafika na watu
tofautitofauti wanatoa zawadi, zawadi ni nyingi sana, kamati ikiongozwa na Raymond
wanatoa zawadi yao)
Raymond:(anachukua
kipaza sauti) asanteni sana, habari za jioni mabibi na mabwana mbele yenu
ni wana kamati walioweka nguvu zao katika kufanikisha sherehe hii…kutokana na
muda wala sitawambulisha ila nitajitambulisha kwa niaba ya wote…mimi naitwa Dk.
Raymond Desmond Bembele ni mwenyekiti wa kamati
(Makofi na
vigelegele vinasikika mahali hapo)
Raymond: Kama kamati ile nyumba uliyoianza…sisi
tutaimalizia na kila kitu kimeshanunuliwa (anamkabidhi
risiti)
Edmond: thank you so much brother…
Raymond: sambamba na hivyo vitu vya ndani…interior
zote ni juu yetu...na baada ya hapo tunakukabidhi milioni 30 ya kuanzia maisha
(watu wanashangilia sana, baada ya makabidhiano ya
zawadi kamati inarudi kukaa na sherehe inaendelea huku kila mmoja anafurahia
sherehe hiyo)
0 Comments