SCENE 54: -
BAADA YA WIKI MBILI: -
MAHARI YA ANGELINA: -
(majira ya saa nane mchana, Mr. Bembele, Mrs.Bembele, Edmond, Peter na Raymond
wanafika nyumbani kwa kina Angelina ambapo wanapokelewa kwa shangwe nyingi sana
na wanafamilia na ndugu mbali mbali wa Angelina, sebuleni wamekaa wazee wa Angelina
yaani wajomba na jikoni kina mama mbalimbali wanamalizia kupika, nyumba ni ya
kawaida sana sakafu haina simenti n.k, huku Angelina, Catherine na Christina
wamekaa chumbani wakimuandaa Angelina)
Catherine :(
anachungulia kupitia dirisha dogo linaloelekea sebuleni) wamewahi?
Christina: ni bora walivyoamua kuja jana wakalala
hotelini mjini (anaguna) yaani
wangesema waje leo tungekesha
Angelina :( anavuta
pumzi) wameshakuja kwani?
Catherine: ndo wanaingia, wapo mzee mwenyewe,
shemeji Raymond, shemeji Peter na mume wangu
Christina: tufanyeni haraka si watatuita muda si
mrefu
Catherine: bado Sana ndo kwanza wanaingia
(Vinasikika vigelegele nje)
Angelina: Mungu wangu pamekucha…
Catherine: hata usiogope ukishatolewa mahari
unakuwa na uhakika Fulani hivi…najua huwa inakupa presha…si eti Christina?
Christina: Sana…
Angelina :(
Kwa Christina) shemeji ameshakutolea mahari?
Christina: muda mrefu mbona…
Catherine: ndoa lini?
Christina: baada ya miezi miwili
Catherine :(
anamuangalia Angelina) maisha bwana nakumbuka Angelina alikuwa anamuogopa Raymond
anamuita kaka mara sijui nini Leo mume
(Wanacheka)
Christina: ndo hivyo haya maisha hakuna anayejua
Mungu kampangia nini
Catherine :(macho
yake yanaangalia sebuleni) ni kweli
Christina :( anacheka)
yaani wewe macho yako yapo sebuleni una utani
Catherine: acha tu
(Huku
sebuleni, wajomba wanawakaribisha wageni wao vizuri huku shangwe zinatawala Kwa
wachache waliopo hapo)
Mjomba: karibuni Sana ndugu zangu…nyie ni wenyeji
wa wapi?
Mr. Bembele :(
anakohoa kidogo) sisi Kwa uenyeji tumetoka Dar ila Kwa kabila sisi ni
wasukuma wa Mwanza
Mjomba 2: aha…Safi Sana...Sisi ni wahangaza na ni
wenyeji wa Ngara na ndo wahangaza hupatikana
Mr. Bembele: Asante Sana na tunafurahi na tushukuru
kufahamu hilo
Mjomba: ndio karibuni wageni wetu labda tuanze Kwa
kujitambulisha sisi kwa majina lakini baadae tutaendelea na ratiba nyingine…
Mr. Bembele: labda tusikie utambulisho kutoka kwenu
maana nyinyi ndo wenyeji zetu
Mjomba 2: yupo sawa kabisa… (Anatikia kwa kichwa) Kwa majina naitwa Caisalius Rogders ni kaka
kabisa wa mama yake Angelina….
Mjomba: nami naitwa Raymond…Rodgers ni mjomba wake Angelina
Mr. Bembele :(
anacheka) bwana Raymond una jina sawa kabisa na kijana wetu hapa… (Anamshika Raymond)
Raymond Rodgers: ndio Angelina alitudokeza
(Wanacheka)
Caisalius: sawa inapendeza Sana…tusikie kwenu
Mr. Bembele: mimi naitwa Bwana Bembele ni
mfanyabiashara jijini Dar es salaam, na huyu anayefata anaitwa Peter na yule
mwingine anaitwa Edmond na huyu hapa (anamgusa
Raymond) anaitwa Raymond...Bembele ni daktari nan do kijana aliyetuleta
hapa, ameona ua katika bustani yenu kimila na desturi za wa Tanzania ameona aje
aombe ridhaa yenu alichume…ni mwanangu
Caisalius: tunafurahi Sana kwake yeye kuchukua
ustaarabu wa kuomba nasi tunasema aombae hupewa
(Wanacheka)
Mr. Bembele: basi Kama ilivyo kawaida tukikubaliwa
tunatoa zawadi Kwa wale ambao wametupa ridhaa ya kuchuma ua
(Wajomba wanacheka)
Raymond Rodgers: wajina embu Kwa ustaarabu (anawageukia wanawake) leteni mabinti hao
ili kijana atuambie ni ua gani amelichagua
Raymond :(
anacheka)
(Wanawake wanawaleta wasichana waliovaa sare wakiwa wamejifunika khanga
na hawaonekani kirahisi)
Caisalius: wafunue tuwaone
(Wanawake
wanawafunua wasichana hao)
Raymond :(
anatabasamu)
Caisalius: haya baba Kwa upole kabisa embu kamata
ua unalotaka kulichuma
Raymond :( ananyanyuka
na kwenda moja kwa moja mpaka kwa Angelina) huyu hapa
(Vigelegele
vinalipuka)
Caisalius: sawa kabisa… (Kwa wasichana wengine) mnaweza mkaenda
(Wasichana wanaondoka)
Caisalius :(
Kwa Angelina) enhe mama tuambie kijana amekupenda na anataka kukuoa je
unamruhusu
Angelina :( anajibu
huku anapiga magoti mpaka chini kisha kwa heshima kabisa anainamisha kichwa)
ndio mjomba
(Vigelegele na shangwe vinatawala)
Raymond :( anafurahi
Sana)
Angelina :( anamuangalia
Raymond huku anatabasamu)
Raymond Rodgers: sawa wewe rudi tutakurudisha
baadae
Angelina :(
anarudi ndani)
Caisalius :( kwa
Raymond) kijana rudi ukakae ulipokuwa umekaa...
Raymond :(
anarudi)
Mr. Bembele: asanteni sana kwa kutupokea (anatoa zawadi nyingi ikiwemo vitenge, mashati,
mablanketi na pesa taslimu kama
milioni moja) hiyo ni zawadi ya kutupokea na kutukubalia
(Wajomba wanapokea na kuwapa wanawake mbalimbali)
Caisalius: tunawashukuru sana kwa zawadi hizi...Sasa
Ni wakati wa kuongelea mahari
Mr. Bembele: sawa tunawasikiliza
Caisalius: sisi mtoto wetu tumemlea Kwa shida Sana
na pia tumemlea katika maadili mazuri na anafaa kuwa mke na atakuwa mke bora
(Upande wa kina Raymond wanatikisa vichwa kukubaliana na kinachosemwa na
mjomba)
Mr. Bembele: sawa tunakubali kabisa…
(Wajomba wanajadili jambo)
Raymond Rodgers: sawa sisi mahari tumepanga iwe
milioni tano
(Upande wa kina Raymond wanajadili jambo)
Mr. Bembele: sawa tumekubali (anatoa kitita cha pesa)
(Mjomba anapokea Na kumuita mama yake Angelina)
Mama Angelina :(
anazipokea pesa Kwa heshima kabisa)
Caisalius: huyu ni mama mzazi wa Angelina
Mr. Bembele: wanafanana sana
Mama Angelina :(
anatabasamu)
Caisalius :(
Kwa mama Angelina) hii ni mahari binti yetu Angelina ameposwa anataka
kuolewa
Mama Angelina :(
anapiga vigelegele) karibuni Sana
Mr. Bembele: Asante Sana
(Mr. Bembele na mama Angelina wanashikana mikono)
Caisalius: Na kijana aliyemposa mwenetu Ni (anamshika bega Raymond)
Mama Angelina: Asante baba…wewe ndo huwa tunaongea
kwenye simu?
Raymond: ndio mama…
Mama Angelina: karibu baba (anamshika mkono huku anapiga vigelegele)
(Mrs.Bembele na mama Angelina wanakumbatiana ishara ya kukubaliana)
Raymond Rodgers: sasa zoezi la mahari tayari sasa
tuwakaribishe wageni wetu kushiriki chakula cha mchana kwa mara ya kwanza kama
ndugu
Mr. Bembele: haina shida kabisa…tunashukuru kwa
mapokezi mazuri mnaonekana ni wakarimu sana
Caisalius: kawaida ya waTanzania…halafu
Angelina ana wadogo zake watatu… (kwa
mwanamke mmoja) waiteni wageni wawaone
(Wadogo wa Angelina wanakuja kwa wageni na kila mtu anaonekana
kuwafurahia)
Mr. Bembele: jamani watoto wazuri hamjambo?
(Wadogo zake Angelina wanawasalimia wageni Kwa
heshima)
Mr. Bembele: mna heshima…
Caisalius :(
anadakia) Kama dada Yao (anatabasamu)
Mr. Bembele :( kwa
mkubwa inaonekana ndo anamfuata Angelina) unaitwa nani?
Mdogo: Angello...
Mwingine: Mimi naitwa monalisa
Mwingine: Mimi naitwa Clara
Mr. Bembele: majina mazuri Sana…tunaenda wote Dar
Monalisa: kule kwa dada?
Mr. Bembele: ndio kwa dada
Clara: ndio
(Wote wanacheka)
Mr. Bembele: haya jiandaeni twendeni sawa ee
Angello: sawa
(Wanarudi ndani wakiwa wana furaha Sana)
Raymond Rodgers: jamani chakula tayari tujongee
mezani
(Catherine, Christina
pamoja na Angelina wanakuja kuungana na wenzi wao kwenye chakula, Mr na Mrs.Bembele
wanakaa sehemu moja huku vijana sita yaani Edmond na Catherine, Peter na Christina
na Angelina na Raymond wanakaa sehemu moja)
Edmond: afadhali siku imeenda na kuisha vizuri
Raymond: kabisa
Peter :( Kwa Raymond)
official mume wa mtu mtarajiwa
Edmond: kwa mara ya ngapi sijui
Catherine: acha kumchokoza mwenzio muone
Christina :( anacheka
huku anakula chakula chake)
Angelina :(
anatabasamu)
Edmond: najiuliza zile kesi sijui zitaendelea…zile
za kubeba mabegi…
(Wanaangua vicheko, vinavyowashtua wazee waliokaa mbali nao)
Caisalius: mmefurahi ee
(Hawajibu kitu badala yake wanaangua vicheko tena)
Caisalius: vizuri kufurahi wanangu
(Mazungumzo yanaendelea baina ya watu)
Raymond :( anamshika
mkono Angelina) namshukuru Mungu kwa ajili ya leo mpenzi wangu sasa mipango
ya kujenga familia yetu
Angelina:ni kweli mume wangu mtarajiwa
Raymond: nakupenda Sana
(Wanaendelea kula, na kila mmoja wao anafurahia
siku hiyo, picha nyingi zinapigwa na mara nyingi mpiga picha anawalenga Angelina
na Raymond ambao ndo malkia na mfalme wa siku hiyo. sherehe ya mahari inaisha
vizuri bila shida kabisa na kila mtu anaonekana kuridhika na kila kitu
kinachoendelea)
0 Comments