SCENE 55: -
(Siku kadhaa mara baada ya sherehe ya kutolewa kwa mahari kwa Angelina kupita,
wadogo zake Angelina pamoja na mama yao wamekaa katika sebule kubwa nay a
kifahari ya Raymond mume mtarajiwa wa Angelina, wanashangaa uzuri wa kila kitu
ndani humo)
Clara :( Kwa
mama yake) mama ona li TV likubwa
Mama: naliona mama
Monalisa: mama ona palivyo pazuri…
Mama: Sana
Angello: mama shemeji tajiri si eti eeh
Mama: ndio mwanangu Mungu hamtupi mja wake ona
mwanangu anapoenda kuolewa yaani nafurahi Mimi…asante Mungu wangu
(Wakati huu Angelina amesimama nje ya dirisha moja linaloelekea sebuleni
anawasikiliza na kila mara anatabasamu)
Angelina: hata mimi namshukuru Mungu kwa haya yote…sikutegemea
kama Raymond alikuwa ananiambia ukweli tangu mwanzo kuwa anataka
kunioa…sikudhani kama alikuwa ananiambia kweli pamoja na misukosuko yote ya
maisha bado Raymond alionyesha kunipenda Zaidi na Zaidi
(Raymond anakuja Kwa nyuma yake na kumkumbatia)
Raymond: mbona unaongea peke yako…
Angelina :( Analia
huku anacheka) Asante sana Raymond
Raymond: machozi tena? (anamgeuza ili amuangalie vizuri)
Angelina:(anacheka)
ona wadogo zangu walivyo na furaha…nimekuwa nikifanya kila kitu kuona tabasamu
kama linavyoonekana sasa hivi…Mungu ni mwaminifu…
Raymond:(anamshika
mkono huku anamuongoza kuelekea bustanini) twende mke wangu mtarajiwa
twende mahali mapenzi yetu yalipoanzia…
(Wanafika
palepale Raymond alipopamba kwa ajili ya kumwambia hisia zake kwa mara ya
kwanza)
Raymond: hapa nilipachagua sababu ya utulivu wake,
nilipapamba kwa mara ya kwanza na kukuambia hisia zangu kuwa ninakupenda sana
mpenzi wangu…kabla sijakuambia nilikuwa naogopa watu, Edmond, Catherine.baba.
mama na Zaidi Christina ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni mchumba wangu…
Angelina :(
anamuangalia sana)
Raymond: siku ile niliweka pembeni uoga na
kukutamkia hisia zangu nashukuru ukazipokea…
Angelina:(anatabasamu)
Raymond:baada ya penzi letu kujulikana…ulipata tabu
sana mara uambiwe nina mtoto….(anacheka)ukabeba
mizigo yako ukaondoka nikakufata huku nikiwa naogopa sana pengine labda ndo
mara yetu ya mwisho na kwamba penzi letu litaishia hapo…nilikuambia ukakubali
kurudi na mimi nyumbani…baada ya muda ukatekwa na kupigwa vibaya ila
ulipotibiwa ukasahau yote na kuruhusu penzi letu kuendelea…hilo
likapita,nikarudishwa akili nyuma lakini bado ukasimama na mimi hukuniacha
mpaka siku nikawa vizuri na penzi letu likazidi kuota mizizi
Angelina :( anatabasamu)
Raymond: Asante sana Angelina kwa kunipenda
kunijali na kuniheshimu…asante kwa kumheshimu baba yangu pamoja na kwamba
alikuwa anakutukana sana na kukusema vibaya ila hukuacha kumheshimu kama baba
yako mzazi… (Anamuangalia kidogo)
wewe mwanamke ni bora sana nataka nikupe zawadi sijui kama itatosha kwa furaha
uliyo nipa katika maisha yangu…siku namwambia Edmond anitafutie msichana wa
kazi za ndani sikuwa na wazo kama msichana huyo atakuwa mke wangu na mama wa
watoto wangu
Angelina :(
anacheka)
Raymond: I fell in love with my housegirl…I AM
IN LOVE WITH MY HOUSEGIRL (anacheka)
Angelina :( anacheka
pia)
Raymond: umeelewa?
Angelina: nimeelewa kidogo…sana, si unajua nimeanza
kusoma kiingereza naelewa
Raymond: nimesemaje?
Angelina: love maana yake kupenda na housegirl
maana yake msichana wa kazi za nyumbani sasa hapo lazima itakuwa labda nampenda
msichana wangu wa kazi za nyumbani
Raymond: umepatia (anamnyanyua kidogo)
Angelina :( anambusu)
Raymond: wakati wote tupo kwenye mahusiano kwanza
kama kaka na dada, baadae wapenzi na baadae wachumba nilikuwa nakujengea nyumba
kama zawadi…yaani sasa hiyo ni ya kwako hata ikitokea leo nimekufa ni yako wewe
Angelina
Angelina: baby usiongelee kufa bwana...
Raymond :( anamuonyesha
picha kwenye simu) hi indo nyumba yako
(Nyumba nzuri hatari)
Angelina: Mungu wangu nyumba nzuri sana...Jamani
asante mume wangu (anamkumbatia)
asante sana sana tena sana...Wow...Jamani (anambusu
mfululizo)
Raymond: ninafurahi kwamba umefurahi sana, wadogo
zako utawasomesha…sio kwa mshahara wa udada wa nyumbani bali…nimekufungulia
kampuni ya wadada wa kazi za nyumbani yaani housegirl utakuwa unawatoa mikoa
mbalimbali unawaleta huku unawafundisha labda na wenyewe watapata bahati kama
yako(anacheka)kisha unawasambaza watu
wana uhitaji wa mabinti wa kazi…
Angelina :(
anafurahi Sana)
Raymond: nyumba ya kijijini kwa mama yako
imeshaanza kurekebishwa na kila kitu kinaendelea vizuri
Angelina:(Analia
kwa furaha) Mungu nikurudishie nini jamani… (kwa Raymond) asante mume wangu mpenzi…
Raymond: lakini mbali na kampuni ya wadada wa kazi
kuna saluni ya kike ya kisasa nimeifungua kwa ajili yako yaani sitahusika labda
ukitaka kunikopesha
(wanacheka)
Angelina: yaani wewe
Raymond: nini tena?
Angelina: I love you
Raymond:(anashangilia)
Angelina kajua kiingereza
Angelina: nilimuuliza mwalimu akaniambia ni
hivyo…nimeitaja vizuri
Raymond: sana (anamuangalia
kwa umakini) halafu mimi mchumba wangu ni mrembo jamani yaani watoto
watakaotoka hapo ni visu…wakifanana na wewe lakini
Angelina: mimi nataka wafanane na wewe…
Raymond: mama yangu na sura baya hili?
Angelina: sio mbaya na mashavu ya kubonyea ni noma
Raymond: yanabonyea kama ya Gloria Bembele
Angelina: enhe…halafu unafanana kweli na mama
kuliko baba
Raymond: eti ee… (anaangaza angaza) yaani huyu mdada wa kazi hajui kazi sijui yuko
wapi?
Angelina:(anacheka) huna lolote unataka kunituma kitu,
naenda kukuchukulia hiyo juisi unayopenda (anacheka
huku ananyanyuka kuelekea ndani)
Ramadhani:(ambae
amesimama anawaangalia muda mrefu) jamani haya maisha acheni yaitwe maisha
na Mungu ndo muweza wa yote akipanga, amepanga…hata waje na waganga lori zima
Mungu atabaki kuwa mkuu…ona sasa hawa, kulikuwa na kina Christina kina Mz. Bembele
leo hii wamenawa mikono wanachekelea tu (anacheka)
sema nini Raymond Angelina amekufaa mwaya…mimi nilikuwa nakula hela bure za Christina
ila hata mimi nilikuwa naona hamuendani (anacheka
huku anarudi getini) mmependezeana bwana
Angelina :( anarudi
alipo mchumba wake na juisi glasi mbili) yaani wadogo zangu wanapenda Tv
wanachelea tu (anampa glasi moja Raymond
huku moja anabaki nayo)
Raymond: waache wafurahie jamani Kwa shemeji...
Angelina: wanatakiwa warudi shule
Raymond: we nae (anakunywa juisi kidogo) ila kwenye harusi watakuwepo?
Angelina: watakuja
(Wanaendelea kupunga upepo safi huku wanapata juisi
zao baridi huku wanazungumza mambo mbalimbali)
0 Comments