SCENE 56: -
BAADA YA MIEZI MIWILI: -
HARUSI YA CHRISTINA NA PETER: -
(jioni iliyo njema machoni pa bwana, basi kama ilivyo kawaida ikimpendeza
bwana basi na wanadamu wanapendezwa nayo, hali ya hewa inavutia ili kuendelea
na shughuli yoyote ile. katika ukumbi mmoja wa kifahari watu wamekusanyika ili
kusherekea muungano wa Peter na Christina, wapenzi wa karibia miaka mitatu.
Watu mbalimbali wanaingia ukumbini, miongoni mwa watu hao ni wazazi wa Christina,
wazazi wa Raymond, Edmond na mkewe na hatimaye Raymond na mchumba wake)
Mama Christina:(anajifuta
machozi)
Shangazi: mwenzetu vipi mbona unalia?
Mama: nimefurahi sana…
Baba:(anacheka
sana) mwanao alishtuka mapema sana...
Mama: Mungu ni mwaminifu leo Christina amefunga
ndoa na yule yule mwanaume aliyekuwa anaona hamfai…mwisho wa siku mapenzi
yakashinda pesa na mali zote
Shangazi: hakika!!!
Mama: mwanangu leo alikuwa amependeza sana kanisani
Shangazi: sana
Baba:my princess is married (anafurahi sana)
(upande walipokaa Angelina na Raymond)
Angelina: nimependa sana kanisani wakati Christina
Analia
Raymond: yes…amelia sana maana yeye na huyo
mwanaume wamepitia mambo mengi sana hakuamini kama leo amekuwa wake wa milele
Angelina:(anaangaza angaza) wow ukumbi umependeza
Raymond:na mwalimu wako wa English course anafanya
kazi nzuri sana…
Angelina: kwanini?
Raymond: nazisikia hizo wow... (anacheka sana)
Angelina: bwana...niache, mimi nausifia ukumbi na
wewe unanitoa kwenye mood
Raymond: kazi ya sisi kamati… (anacheka kwa kujidai)
Angelina:(anaguna)
na unavyopenda kuwa mwenyekiti wa kamati sijui harusi yako nani atakuwa
mwenyekiti?
Raymond: hata wewe sawa tu
Angelina:(anashangaa)
mimi tena?
Raymond: ndio…(anacheka)
Angelina: huku mimi ni bibi harusi…
Raymond: wacha weeee
(kwa wazazi wa Raymond)
Mrs.Bembele: yaani ukumbi umependeza Sana
Mr. Bembele: kabisa
Mrs.Bembele: Christina kaolewa…nimefurahi Sana
kwanza kwasababu hii miezi michache iliyopita amejua kujirekebisha na
imependeza
Mr. Bembele: kweli kabisa (anajisemea moyoni) kikubwa nachomshukuru Christina ni kwamba
hakuwahi kusema ukweli wa mahusiano yetu kwa mke wangu ameniokolea ndoa sana
Mrs.Bembele: nakupenda mume wangu
Mr. Bembele: nakupenda pia Gloria wangu mpenzi
(wanacheka)
Mc: habari za jioni mabibi na mabwana…
Watu:(wanaitikia)
Mc: tupo nje ya muda kidogo wapendwa wangu na kwa
kutambua hilo, sasa naomba niwaruhusu ma brighter wasafishe njia ya maharusi
wetu… (Kwa dj) Dj
(Muziki mzuri unapigwa wakati huo mabrighter wanaingia wakicheza kwa
madaha yote, wanacheza wakielekea mbele ya ukumbi, wanacheza kwa muda na
hatimaye wanafika mbele)
Mc: barabara kabisa mara baada ya mabrighter wenu
wake Kwa waume sasa ni zamu ya matron na best man
(Edmond na Catherine kama matron na bestman wanaingia ukumbini hapo kwa
mbwembwe Zaidi ya zile walizoonyesha siku ya harusi yao, wanacheza huku kila
mmoja anawashangaalia sana, wakiwatiwa moyo na shangwe zile wanacheza mpaka
wanafika mbele ambapo mabrighter wamesimama)
Mc: wow…basi bila kupoteza muda kwa shangwe
hizohizo naomba tuwakaribishe maharusi wetu…bibi na bwana mbeikya…bwana harusi
mhaya huyu (anacheka kidogo) wahaya mpo
(Unapigwa
wimbo mmoja wa kihaya unaonawachangamsha Zaidi watu)
Mc: wwwwaaaah basi Dj imetosha Sana hiyo
(watu wanarudi kukaa kwa wale wote walioenda mbele kuyarudi mangoma ya
kihaya)
Mc: safi sana…sasa mabibi na mabwana nawaomba sasa
kwa heshima na taadhima tuwakaribishe maharusi wetu ambao wapo tayari kabisa
kwa ajili ya kuingia ukumbini hapa...kwa ajili ya sherehe nzuri tuliyowaandalia
siku ya leo…asante sana kamati kwa kufanya sherehe yetu ipendeze na
wakahakikisha tunakula tunakunywa tunavyotaka…shoutout kwa Raymond Bembele
mwenyekiti wa kamati ya harusi hii
(Watu
wanapiga makofi)
Mc: basi Dj niletee maharusi wangu…
(muziki mzuri
na wa amshaamsha unapigwa huku Christina na mumewe wakiingia kwa mbwembwe zote,
watu wanawashangilia na wa kufurahi wanafurahi wenye kupiga picha wanapiga kwa
kifupi kila kitu kipo sawa kama kilivyopangwa, wanacheza na kila mtu anavutiwa
na jinsi wanavyoingia, wanacheza kwa muda na hatimaye wanafika mbele walipo
matron na bestman)
Mc: asante Dj… (kwa
maharusi) mmependeza jamani…
(Ama hakika wamependeza, tena wamependezeana Peter ni mrefu kijana
mtanashati huku Christina ni mrefu kiasi na ni msichana mrembo sana)
Mc: wow…jamani maharusi mmependeza
Peter na Christina :( wanacheka) asante sana
Mc: tuendelee na ratiba nyingine maana nikianza
kuwasifu jamani sitamaliza…
(Watu wanacheka Sana)
Mc: utambulisho
(Bila kupoteza wakati Peter anaanza utambulisho akitambulisha ndugu zake
na kila akitambulisha ndugu wananyanyuka na kuwapungia watu mikono,
anatambulisha wote na mwisho anamtambulisha Christina)
Peter :(
anamshika bega mkewe Kama kumkumbatia hivi) na huyu ni kipenzi changu,
chaguo la moyo wangu, mahabuba wangu
(Watu wanashangilia)
Peter: mke wangu…anaitwa Mrs.Christina Peter
Mbeikya…
(Watu wanapiga makofi)
Mc: safi jamani bwana harusi yupo
romantic…(anatabasamu)haya na wewe bibi harusi onyesha makeke yako tuyaone
kwenye utambulisho…twende sasa
(Christina
anachukua kipaza sauti na kuanza kuwatambulisha ndugu zake wakiwemo wazazi wake,
shangazi yake na ndugu wengine, kila mara wakitambulishwa ndugu hao husimama na
kupungia watu mikono, anatambulisha mwisho anamalizia na mumewe)
Christina :( anacheka
kidogo huku anamshika mumewe begani) na huyu ni mume wangu mpenzi wa moyo
wangu, rafiki yangu na mshikaji wangu anaitwa Peter Renatus Mbeikya
(Watu
wanapiga makofi Sana)
Mc :( anaguna
kidogo) hapo kwenye mshikaji embu tufafanulie tafadhali)
Christina: si mshikaji tu
(Watu akiwemo mama yake wanacheka Sana)
Mc: kiaje
Christina: ki hivyohivyo…
(watu wanacheka)
Mc:(anaguna)
haya bwana umekataa kuniambia nasusa
(Vicheko)
Christina: ukisusa wenzio twala
Mc: heeeeeee! Bibi harusi huyu… (Anacheka)
Christina :( anacheka)
Mc: haya sina cha kuongezea, naomba nimtangaze bibi
harusi kuwa ndo mshindi wa mtanange huu
(Watu wanapiga vigelegele)
Mc: amekataa kuniambia kwanini anamuita mumewe
mshikaji
(Watu wanacheka)
Mc: basi sawa muda wa keki…
(Keki inakatwa, maharusi wanalishana, kisha wanawalisha wapambe wao na
baada ya zoezi la kulishana keki zinapelekwa kwa wazazi wa pande mbili na baada
ya zoezi la keki kuna zoezi la zawadi. watu mbalimbali wanatoa zawadi na
hatiamye kamati inayoongozwa na bwana Raymond Bembele)
Raymond:(Baada
ya kufika mbele) habari za jioni mabibi na mabwana, mbele yenu ni kamati ya
maandalizi ya sherehe hii, ili tusipoteze muda mwingi nijitambulishe kwa niaba
ya wote…mimi ninaitwa bw. Raymond Bembele ni mwenyekiti wa kamati hii mnayoiona
hapa mbele
(Watu wanapiga makofi)
Raymond: zawadi zetu kwa maharusi ni kiwanja na
vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba yao na watoto wao
(Shangwe za
kutosha zinaendelea mahali hapo)
Raymond: gari aina ya prado naona lipo hapo nje…tutawakabidhi,
tiketi za ndege kwenda south Africa kwa ajili ya fungate na mapumziko mafupi…
Watu: woooo…w
Raymond:na pesa taslimu milioni sita… (anawakabidhi cheki) asante na Mungu
awabariki
(DJ anaachia ngoma nzuri ya kuwarudisha kamati wakakae,
wanaenda kukaa sherehe inaendelea na watu wanacheza, wanakula wanakunywa na
kila kitu kinaonekana kipo shwari, maharusi wamefurahi, wageni waalikwa
wamefurahi na Zaidi kamati imefurahi. sherehe imefana sana, Christina na Peter
wanawashukuru sana wageni waalikwa na wazazi kwa ujumla)
0 Comments