SCENE 57: -
(jioni nyingine wiki kadhaa mara baada ya harusi ya
Christina na Peter kupita, Edmond, Catherine, Raymond na Angelina wamekaa
katika bustani safi iliyopo nyumbani kwa Raymond, wanajadili kuhusu harusi
iliyopo mbele yao)
Edmond: hii harusi inatakiwa iwe bab’kubwa kama ya
mastaa kwenye picha(anacheka)picha
zenu mnazoangaliaga ITV
(Angelina na Catherine wanacheka)
Raymond: oh, finally naenda kumuoa kipenzi changu
imekuwa Zaidi ya mwaka tangu nimekuwa nae
Edmond: uzuri wako umekaa na mkeo mtarajiwa hata
kabla ya kumuoa
Raymond: ndo hivyo (anacheka kidogo)
(Christina na Peter wanakuja mahali pale)
Edmond: wow…wanandoa wapya kabisa mjini
Peter: eeh baba…mpo poa
Raymond na Edmond: poa
Christina :( anatabasamu) za hapa jamani
(Wanaitikia)
Edmond: za honeymoon?
Peter na Christina: nzuri tu
Raymond: wacha we… (Anamuangalia Christina) mbona Kama umenenepa
Edmond: na wewe (anampiga ngumi moja)
Raymond: utaniua unajua Mimi ndo bwana harusi pekee
niliyebaki
Edmond: hai au?
(Wanacheka)
Angelina :( Kwa
Christina na Peter) karibuni jamani niwaletee vinywaji gani?
Christina: chochote ukipendacho wewe
Angelina: eti ee… (Kwa Peter) Na wewe shemeji?
Peter: maji tu
Angelina: sawa (anaelekea
kwenda jikoni)
Raymond: enhe…naona mama mwenye nyumba kaenda
kuleta vinywaji sisi tuendelee na mazungumzo
Edmond: kabisa…
Christina: mlikuwa mnaongelea nini?
Catherine: harusi ya hawa ma staring
(Wanacheka)
Raymond: kwani muvi hii?
Catherine: Kwa mfano ingekuwa tamthilia mngekuwa ma
staring
Edmond :( anatikisa
kichwa) yaani wanawake bwana wao kila saa mnawaza tamthilia…tu…na wale
wakalimani wenu utasikia yoooo anakujaaaaa
(Wanacheka Sana)
Angelina :( anakuja amebeba glasi mbili za maji
kwenye trei)
Raymond: dear dada yuko wapi?
Angelina: yupo jikoni…
Raymond: si ungemwambia alete yeye?
Angelina: ana kazi nyingine...
Edmond: embu muache bana na wewe…
Angelina :( huku
anawapa maji Christina na mumewe) karibuni sana
Christina: hivi Angelina wadogo na mama yako
walishaondoka
Angelina: siku nyingi Sana watakuja kwenye harusi
lakini
Christina: aha!!!Kumbe sikujua ndo kidogo nikuulize
mbona sijawaona kwenye harusi?
Angelina: walishaondoka walikuja kusalimia tu
Christina: basi sawa… (kwa wengine) jamani tumekuja na habari hapa?
Raymond: ipi tena na wewe mbaya nzuri
Christina: eeh baba tuliza mzuka
Edmond: eti mbona unapanikigi sana wewe (anacheka)
Raymond: wewe, Mimi sasa hivi sitaki kukonda
Edmond: Na nini sasa
Raymond: Na mawazo…
Catherine: nyie hawa hawamalizi utani wao naomba tu
mama utuambie hiyo habari
Christina :(
anatabasamu) ah… (Anavuta pumzi ndefu) Mimi na mume wangu tunatarajia kuwa
wazazi maanake nina ujauzito… (Anatabasamu)
(Wanalipuka
na shangwe, vifijo na makofi kwa sana)
Edmond: kwahiyo habari za ujauzito zimefika mbili…
Christina: na nani tena? Angelina?
Angelina: hapana…
Edmond: mke wangu mpenzi Sana…Mrs.Catherine
Mutalemwa…
Christina: wow…hongereni Sana
Edmond: hongereni pia jamani…
Raymond: party…tutoke jamani jioni tukajirushe
Edmond: wazo zuri…
(Wanafurahi Sana)
Edmond: bado Angelina
Angelina: baada ya ndoa... (Anafunika macho yake kwa mikono miwili ishara ya kuona aibu)
Raymond :(
anaguna)
Catherine: eeh hiyo ndo vizuri maana wenzio hapa
tumekuwa wajawazito baada ya ndoa (Kwa Raymond)
sasa Shem unaguna nini?
Raymond: Mimi nataka sasa hivi
Edmond: embu kwenda huko…hili lisukuma vipi hili…
Raymond: mi nataka tu mtoto
Edmond :(
anamtania Kwa kumsukuma kidogo) embu tupishe huko
Christina :( anacheka)
yaani hawa…
Peter :(
anacheka)
Raymond: hongereni Sana…
Peter: tunashukuru mwenyekiti
Raymond :( anacheka)
nyie hilo jina (anaguna)
Angelina :( Kwa
Peter na Christina) hongereni sana jamani
Christina: Asante katotoooo
Raymond: katoto…kazae hivyo hivyo
(Wanacheka Sana, wanaendelea kuongea na
kufurahi na kupanga mipango mingi ya harusi ya Angelina na Raymond)
0 Comments