SCENE 58: -
BAADA YA
MWEZI MMOJA NA NUSU
HARUSI YA ANGELINA
NA RAYMOND
(KANISANI)
(Hayawi
hayawi mbona yamekuwa wamesema haolewi mbona anaolewa, asubuhi iliyo tulivu
kabisa machoni pa kila kiumbe chenye uhai na kisicho na uhai, siku hii
imebarikiwa na bwana maana kuna hali nzuri kabisa ya hewa, kaubaridi kwa mbali
na upepo mwanana unavuma na hali inavutia sana, ndugu jamaa na marafiki wa Angelina
na Raymond wamekusanyika katika kanisa kubwa la T.A.G wakisubiri muungano kati
ya Angelina na Raymond)
Christina :( Kwa
mama yake) ah…hatimaye Raymond anamuoa mwanamke aliyempenda Kwa dhati
Mama: ndio mwanangu kila kitu kinakaa jinsi Mungu
anavyotaka kikae unaweza kupanga hivi yeye akapanga hivi
Christina: Nina furaha Sana siku hizi mama…
Mama: nashukuru kusikia furaha yako mwanangu
(Raymond anafika akiwa na Edmond, Raymond amependeza kwelikweli suti
yake inaonekana ni ya gharama sana)
Christina: bwana harusi huyo
Mama: kapendeza…kweli
Mrs.Bembele :(
anamfuata mwanae) mwanangu…kipenzi changu (anambusu kwenye paji la uso)
Raymond :(
anatabasamu) naam mama
Mrs.Bembele: umependeza Sana
Mr. Bembele :( anawajia) wow…Mr. Bembele junior umewaka
(Anatabasamu huku anamshika bega)
Raymond: Asante baba…Asante kwa kila kitu…asante
hata kwa kukubali penzi langu na mke wangu mtarajiwa…nakupenda sana baba
Mrs.Bembele :( anafuta
machozi) nakumbuka zamani mlikuwa kila mkikutana mnagombana…ona Leo
mnavyofurahia maisha pamoja, sifa na utukufu tumrudishie yeye aliyeziumba
mbingu na dunia
Raymond: usiyakumbuke ya kale mama…tena Zaidi siku
ya Leo sio ya kukumbuka mabaya yote yaliyowahi kutokea maana tutaiharibu bure
siku hii
Mr. Bembele:(kwa
Edmond) asante kwa kuwa rafiki mzuri kwa mwanangu…leo wewe ni bestman wake,
inanipa Amani sana
Edmond :(
anatabasamu) usijali baba tupo pamoja…
Mchungaji :( anakuja
akitokea ndani ya kanisa) jamani bwana yesu asifiwe…
Watu: amina…
Mchungaji: Kwa utaratibu uliowekwa, naomba bwana
harusi na bestman wake waje ndani ili tuwasubiri bibi harusi na matron wake…
(Watu
wanafuata utaratibu)
Raymond :( anaenda
mbele kabisa)
Edmond :( anamfuata
nyuma)
Mchungaji: asanteni…sasa naomba utulivu wakati
msafara wa bibi harusi unajiandaa kuingia kanisani
Mama Angelina :(
anatabasamu wakati wote)
Raymond :( analengwa
na machozi anajitahidi kuyazuia)
(Watoto wa
kike tofauti wakiwemo wadogo zake Angelina wanapita mbele wakiwa wamebeba maua,
wanapita kwa zamu mpaka wanaisha, baada ya tukio hilo anapita Catherine ambae anasimama
kama matron wa Angelina)
Mrs.Bembele:(kwa
mumewe) wow…harusi inapendeza kweli
Mr. Bembele: saaaana mke wangu
Mrs.Bembele: ona mtoto wetu kule mbele
alivyopendeza
Mr. Bembele: Mungu alitupendelea mwenzangu alitupa
mtoto… (Anaguna) sio kwa uzuri huo (anatabasamu huku anamuangalia mwanae aliyeko
mbele anasubiri kumpokea mpenzi wake)
(Wakati huo wanaingia watoto wadogo kati ya miaka mitani na sita
wanaingia huku wanamwaga maua yenye rangi nyeupe na nyekundu)
Watu: wow…
(Mlango
unafungwa)
Mchungaji :(
Kwa watu) sasa Kwa heshima kabisa tunaombwa kusimama Ili kumkaribisha bibi
harusi...
Watu :( wanasimama)
(Lango linafunguliwa, Oh Yes!!!malkia amesimama akiwa amevalia gauni
lenye mkia mrefu sana, veili lake ni refu limemfunika mwili mzima, nay eye
anaonekana kwa mbali sana kupitia veili hilo lililonakshiwa kwa urembo mwingi.Angelina
anatabasamu mara baada ya lango hilo kufunguliwa, wapiga picha mbalimbali
wanampiga picha .akisindikizwa altareni na mdogo wake wa kiume (Angello) pamoja
wanaanza kupiga hatua taratibu sana kuelekea altareni alipo Raymond na
Edmond.Wakiwa njiani kuelekea altareni watu wanakuwa katika hisia
tofautitofauti kuna watu wanalia,kuna watu wanafurahi tu,kuna watu wanashangaa
aina ya shela alilovaa bibi harusi huyo,miongoni mwa watu wanaotoa machozi ya
furaha ni mama mzazi wa Angelina na mume wake mtarajiwa.Angelina anatabasamu
sana na mara zote anawaangalia watu waliosimama kwa heshima ya kumpokea yeye
malkia wa siku hiyo.baada ya hatua kadhaa hatimaye yeye na mdogo wake wanafika
altareni,Angello anamkabidhi dada yake kwa shemeji yake kisha yeye anaenda
kukaa walipo mama na wadogo wengine,wakati huku nyuma Raymond anamshika mkono
mpenzi wake na kupanda nae altareni,anamuangalia sana.Watu wanakaa mara baada
ya Angelina na Raymond kupanda altareni)
Mchungaji :( anacheka
kidogo) eeeh ni yeye au sio yeye
Raymond :(
anacheka)
Mchungaji: embu mfunue tumuone…na wewe umuone
Raymond :( anamfunua)
wow…wewe ni mrembo sana (kwa mchungaji) ni yeye
(Watu
wanaangua kicheko)
Mchungaji: Ni yeye ee…
Raymond: kabisa
Mchungaji: hawajakubadilishia?
Raymond: hapana
Angelina :( anatabasamu
vizuri)
Raymond:(anamuangalia Angelina) jamani Mungu kajua
kuumba…tangu siku ya kwanza nakuona kama mwaka na miezi imepita…nafsi yangu
ilikiri kuwa nakutaka wewe kuwa mama wa familia yangu sio uzuri wa sura na umbo
bali uzuri wa moyo na tabia yako…ni mwanamke mchapakazi, mwenye upendo, mwenye heshima,
mwenye kujali, nakupenda sana Angelina, namshukuru Mungu kwa kuruhusu leo hii
iwe
Mchungaji :( Kwa
watu) mpigieni bwana makofi mengi
(Watu wanapiga makofi na vigelegele)
Mchungaji: ndoa takatifu ya watakatifu na iwe takatifu
(anawaangalia Angelina na Raymond)
kaeni wanangu niwafundishe jambo kabla Mungu hajawaunga kuwa wamoja…
(Angelina na Raymond wanakaa)
Mchungaji: ni jambo la kuhuzunisha kabisa kuona mke
na mume wanagombana na kuivunja ndoa, unajua ni mpango wa Mungu kwetu sisi
wanadamu kuwa pamoja yaani mwanamke na mwanaume kuwa pamoja katika ndoa
takatifu,mmeishi muda mrefu katika uchumba,mmejuana sasa ni jukumu lenu
kuchukuliana nyinyi ni binadamu na haimpendezi Mungu hata wazazi kuona watoto
wao wanaachana na kuvunja ndoa…vumilianeni,mkikosana ombaneni msamaha muwe
wasiri sio mnagombana kila siku dada anajua,mama anajua jamii nzima inajua kuwa
,leo Raymond amegombana na mkewe..
Raymond :(
anawaangalia Catherine na Edmond kisha anacheka)
Mchungaji: basi kwa kusema haya machache naomba tuanze
taratibu za kufungisha ndoa hii... (kwa watu)
je kuna yeyote mwenye pingamizi ya ndoa hii isifungwe?
(Kimya)
Mchungaji: basi Kwa maana hiyo naruhusiwa kufungisha
ndoa hii kati Raymond Desmond Bembele na Angelina Deus…
(Mchungaji anawafungisha ndoa wawili hao huku watu wanashuhudia matukio
hayo ya kheri. baada ya kufanya hatua zote zinazotakiwa hatimaye mchungaji
anawatangaza Angelina Na Raymond kuwa mume na mke)
Mchungaji: alichokiunga Mungu binadamu hawezi
kukipangua Nina watangaza Angelina Na Raymond kuwa mke na mume na ikawe Kheri
kwenu na uzao wenu
(Vifijo, nderemo na vigelegele vingi vinaendelea katika kanisa hilo,
Angelina na Raymond wanakumbatiana na kuukubali umoja wao wa kuwa mume na mke,
watu wanapita mbele kuwapongeza wawili hao)
Mr. Bembele: hongereni Sana jamani…ikawe Kheri
kwenu
Mrs.Bembele: mmependeza, hongereni Sana
Angelina Na Raymond :( wanatabasamu) asanteni Sana
Mama Angelina: hongereni Sana wanangu, Mungu
awatunze
Angelina Na Raymond: amina mama
Christina: hongereni Sana mmependeza
Raymond: Asante mama katumbo…mbona huna tumbo?
Christina: bado ndo kwanza miezi miwili
Raymond: sawa. Tunasubiri kubeba katoto
Christina: usijali (anacheka kisha anaondoka)
Peter: hongereni Sana bibi na bwana Bembele
Raymond :( anawanyooshea
kidole wazazi wake) wale pale
Peter: nyie Ni Mr & Mrs.Bembele junior
(Angelina, Raymond na Peter wanacheka sana)
(Watu wanaendelea kuwapongeza)
Mchungaji: sawa, vyeti vya ndoa vipo tayari Kwa
ajili ya kusainiwa
Angelina na Raymond :( wanaenda kusaini vyeti vyao)
(mashahidi yaani Edmond na Catherine nao wanasaini vyeti hivyo. Baada ya
zoezi la kusaini vyeti wanaruhusiwa kutoka nje na kwendelea na ratiba nyingine,
nao pamoja na ndugu na jamaa wote wanatoka nje na ratiba nyingine zinaendelea.
Wanapongezana, wanafurahi pamoja kisha wanapanda kwenye magari maalumu kwa
ajili ya kwenda sehemu maalum kwa ajili ya kupiga picha za ukumbusho wa ndoa ya
Angelina na Raymond)
Raymond :( akiwa
kwenye gari yeye na mkewe) Mrs.Bembele…
Angelina :( anatabasamu)
abeee
Raymond: umefurahi
Angelina: Sana… (Anataka kulia)
Raymond: usilie... (anamfuta machozi)
(Wanaendelea
na safari huku kila mmoja wao ana furaha nyingi moyoni)
Angelina
na Raymond: (wanapungia watu mikono)
0 Comments