SCENE 7: -
(Raymond amekaa ofisini kwake ila anaonekana amechoka sana sio chini ya
mara kadhaa anapiga miayo, ambayo inamshangaza sekretari wake ambaye yupo hapo
akipanga mafaili)
Sekretari: kaka…unaonekana una uchovu kweli
Raymond: yaani acha tu dada Glory…yaani ni
matatizo…naamka saa kumi na moja nasafisha nyumba yangu, naosha vyombo
nilivyolia jana yake usiku…nahakikisha kila kitu kipo sawa ndo nakuja kazini na
huku natakiwa saa kumi na mbili na nusu ili saa moja kamili niingie kwenye
kikao cha bodi yaani we acha tu
Glory: pole mdogo wangu, si utafute msichana wa
kazi? Awe anakusaidia?
Raymond: Hilo nalo neno…nitafutie basi dada yangu
Glory :( anaguna)
yaani kaka siwezi kukudanganya naweza kupata msichana ila wengi wao wanaweza
wakawa si waaminifu…ukaja kunilaumu bure
Raymond: ndo ubaya, sasa nifanyeje dada je niedelee
kuwa nafika kazini nalala au nifanyeje?
Glory: ila si nasikia una mchumba wewe?
Raymond: tena hata usinikumbushe hiyo mada
Glory: kwanini mdogo wangu
Raymond: mwanamke hajui hata kupika hata chai
Glory :( anashangaa)
Hee!!!Kwanini?
Raymond: hata sijui…huyo sasa ndo mke wangu…wa maisha…si
nitaumbuka mimi?
Glory :( anacheka)
acha kukata tamaa mdogo wangu Mungu atakusaidia anaweza hata akamfanya
abadilike
Raymond: ni ngumu kwa huyo mwanamke
Glory: pole mdogo wangu nakuombea yaliyo mema
Raymond: unasali wapi?
Glory: Lutheran
Raymond: Mimi nasali T.A.G ILA wazazi wangu wote ni
wa katoliki
Glory: kwanini sasa wewe ukaamua kuwa mlokole
Raymond: maamuzi tu…
Glory: hongera kaka kwa maamuzi hayo mema nay a
kupendeza (anacheka)
Raymond: (anacheka
kidogo) kwahiyo umekataa kunisaidia dada…msichana?
Glory: nitajaribu
Raymond; au nisikuchoshe…ngoja (anampigia Edmond)
(simu inaita)
Raymond: hello brother, nambie
Edmond: poa my brother uko poa…?
Raymond: nalala tu mwenzio…Nina uchovu kweli yaani
Edmond: pole…oa… (Anacheka Sana)
Raymond: ah!!!Mpaka nije nipate wa kumuoa si
nitakuwa nimekufa jamani
Edmond: kwahiyo nikusaidieje?
Raymond: nisaidie kaka…unaeza kunitafutia binti wa
kazi anisaidie kazi mwenzenu
Edmond: mama mtu mzima au binti
Raymond: vyovyote bwana
Edmond: una bahati wewe kuna ndugu yake Catherine
katoka Ngara juzi wanakaa nae hapo kwake, anatafuta kazi yoyote… hata za ndani
tena nilitaka kukuambia sijui nikasahau vipi...yupo kwa Catherine
Raymond: Safi sana nan do maana nilikufikiria maana
nilijua tu nitapata nachokitafuta kwako…embu mlete nitamlipa vizuri
Edmond: Kwa Leo haitawezekana maana nina kazi Fulani
imenitinga labda tufanye kesho asubuhi kabla hujaenda kazini
Raymond: Ni mwaminifu?
Edmond: anaonekana ingawa simjui vizuri kwakweli
Raymond: umesema ni ndugu yake shemeji eeh
Edmond: ndio…
Raymond: we si ulisema shemeji yuko peke yake kwao?
Edmond: huyo ni mtoto wa mama yake mdogo
Raymond: sawa kaka…nashukuru Sana…maana
dah…nahangaika Sana mwenzio
Edmond: naelewa Sana tu…ndugu yangu hivi (anaanza kucheka) huwa unadeki kweli
jamani au ndo kupitisha ufagio tu halafu kwaheri mpaka kesho kutwa tena (anacheka)
Raymond: kwahiyo unanicheka mwenzio jamani
Edmond: sikucheki…nakuhurumia mdogo wangu
Raymond: haya fanya kuleta huyo mwanamke
Edmond: nitakuletea
Raymond: poa (anatabasamu kisha anakata simu)
0 Comments