SCENE 8: -
(Asubuhi ya siku ya pili, Raymond yupo chumbani kwake akijiandaa na siku,
wakati anaendele kujiandaa anakumbuka kuwa ana miadi na Edmond, hivyo anampigia
simu)
(simu inaita kwa muda mwisho inapokelewa)
Raymond: za asubuhi kaka
Edmond: poa mambo, ndo naingia getini kwako hapa,
na uhakikishe kuna chai
Raymond :( anacheka
kidogo) upo na binti?
Edmond: ndo hivyo… (Anaingia ndani) mambo Ramadhani
Ramadhani: poa mambo…
Raymond: wewe mbona sikuelewi mambo Ramadhani tena?
(Anacheka)
Edmond: kwahiyo nilivyokuambia kuwa nipo getini uliona
nakudanganya?
Raymond: ngoja niwapokee… (Anatoka nje ya chumba chake kuelekea sebuleni)
Edmond :( anaingia
ndani akiwa na binti)
Raymond :( anapigwa butwaa baada ya kumuona binti)
wow…umeniletea binti eeh
Edmond: ndio kama nilivyokuambia
Raymond: (Anajisemea
moyoni) wazazi wangu walijitahidi kunipeleka nchi mbalimbali ila kote huko
sikuwahi kuona mwanamke mzuri hivi…dah!!Haya si majaribu
Edmond: wewe…mbona huongei?
Raymond :(
anamuangalia binti kisha anatabasamu)
Binti :( nae
anatabasamu)
Raymond: dada…unaitwa nani…na je wewe ni mtu wa
Ngara?
Binti: mi naitwa Angelina, ndio kaka mi ni mtu wa
Ngara
Raymond: sawa…watu wa Ngara warembo sana
Edmond: tena?
Raymond :( anajishtukia) ah hata Shem mzuri yule
yaani Sana tu, wewe humuoni?
Edmond: ah…kumbe…sawa…haya bwana huyu ndo dada wa
kazi uliyeniagiza
Raymond: karibu dada (anajisemea moyoni) is it love at first sight…. Yaani nimemuona tu
najihisi kumpenda
Edmond: we leo vipi yaani unakuwa kama una mawazo au
(anamsogeza pembeni) hujafurahia?
Raymond: we Edmond umemtoa wapi binti mzuri hivi?
Edmond: Ngara…acha ujinga wako sio uje uanze
kumbaka mtoto wa watu…yaani huko kijijini kwao wanampenda sana maana mtoto
anajituma hana tabia za wanaume...
Raymond: anajituma ee
Edmond: Sana…yaani Catherine alinipa stori zake
mpaka nikamfurahia so kaa na mtoto wa watu vizuri…
Raymond: bila shaka kabisa, nimekuelewa kaka
Edmond…
Edmond: poa (anarudi
kwa Angelina) haya mama umefika sasa ukae vizuri, heshima ni kitu cha
muhimu sana mdogo wangu
Raymond :(
bado anamuangalia Sana) una umri gani Angelina?
Angelina: ishirini na mbili…
Raymond: Mimi Nina thelathini na mbili
Edmond: kuna mtu kakuuliza umri wako (anacheka)
Raymond :( anatoka
nje kumuita Ramadhani) Ramadhani…naomba uje mara moja (kisha anaingia ndani)
Ramadhani :( anaenda
ndani) naam boss…
Raymond: jamani si nishakuambia kuwa sipendi unite boss.
Usiniite boss bwana
Ramadhani: sawa nisamehe...
Raymond: usijali…sawa…sasa unamuona huyu ni dada wa
kazi hapa…naomba ukae nae mpaka nitakaporudi toka kazini jioni
Ramadhani: sawa hamna shida (Kwa Angelina) binti Mrembo…Mrembo nambie…unaitwa nani
Raymond :(
anaingiwa na wivu wa ajabu) sio sasa umeona kabinti ndo uanze
kutongozatongoza kuwa makini saana…humu ndani ni kazi tu
Edmond :( anashangaa Sana) we vipi
Raymond: kwani nimesemaje?
(Wote
wanacheka)
Edmond: hicho kibesi sijakielewa kabisa…kwahiyo mtu
akisifiwa kwako kosa (Kwa Ramadhani)
basi fanya kitu kimoja msifie yeye
Ramadhani:
basi poa...Dah!!Raymond we handsome, wewe Mnyarwanda au Msomali? (anacheka sana)
Raymond :( anacheka)
ah!!Nyie nikianza kukuwasikiliza hapa sitoki…mi naenda jamani baadae
Edmond: lifti basi
Raymond: twende nikupe ofa mpaka ofisini kwako…
Edmond: poa
Raymond :( Kwa
Angelina) sasa dada tupikie basi jioni nitakuja kula
Angelina: sawa kaka…
Raymond: halafu sijakuonyesha chumba chako?
Angelina: ndio kaka
Raymond :(
anafungua chumba kimoja) haya chumba chako hiki hapa
Angelina :(
anaingia huku kabeba mfuko wabluu wenye nguo Kama mbili hivi na viatu
vilivyokatika) asante kaka…pazuri kweli jamani
Raymond: Asante sawa wewe kaa…hapa
Angelina: sawa kaka
Raymond :( anatoka
humo chumbani) we Edmond…twende
(Wanatoka nje
wanapanda gari kisha wanaondoka…wakiwa kwenye gari kuna machache wanayoongea)
Edmond: vipi unamuonaje huyu dada?
Raymond: wife material
Edmond: unasemaje?
Raymond: yuko vizuri Sana
Edmod: mdogo wangu stress zitakuua we kila ukimuona
mtu wife material
Raymond: najisikia kumpenda sana Angelina
Edmond: Raymond…tuchungane basi…usije kumpa mimba mtoto
wa watu
Raymond: nakutania…sasa nitampendaje Angelina hata
baba hatoniruhusu, tulia kuwa na Amani kaka yangu handsome mume halali wa
catherine
Edmond :( anacheka)
umeanza (anaacha kucheka) poa Kama
unasema hivyo haina shida mtu wangu
Raymond: muone umeshtuka Sana nilipokuambia
nampenda…eeeh
Edmond: sasa utampendaje mtu ndo kwanza umemuona Leo
Raymond: huamini kuwa wengine wakimuona tu mtu
hapohapo nafsi inakubali kuwa imeridhika…Angelina ni Mrembo sana hiyo haina
ubishi
Edmond: sawa sina neno…
Raymond: she is so beautiful walahi jamani
Edmond: dogo kuwa makini bwana sitaki kesi na
shemeji yako
Raymond: basi siongei tena (anaendelea kuendesha gari)
Edmond: ila utampenda huyu dada yuko vizuri (anacheka)
0 Comments