SCENE 10: -
(Ni Jumamosi nyingine ya kawaida
kabisa kama jumamosi nyingine, siku moja baada ya Liliana kupokea kipigo cha
mbwa kutoka kwa shangazi yake ambae pia ni mlezi wake, Anna na Bella wapo
nyumbani kwani hawaendi shule siku hiyo, Liliana anaugulia maumivu ya kipigo
cha jana)
Shangazi:
na ufue hizo nguo
Anna:
mama naomba simu yako…
Shangazi:
ya nini?
Anna:
kuna rafiki yangu nataka kumpigia aje tusome
Shangazi:(anatoa simu yake na kumpa Anna) fanya
haraka
Anna:(anaipokea kisha anaenda pembeni na
kuzungumza kitu Fulani ambacho hakisikikin kwa walipo hapo maana anaongea kwa
sauti ndogo sana)
Shangazi:(anatoa nguo nyingi sana chafu na kumtupia Liliana)
fua zote hizi acha kujidekeza unadhani mama yako yupo hapa?
Liliana:(Analia sana) shangazi naumwa sana
Shangazi:(anamzaba kofi kubwa sana) pumbavu
nimekuambia fua nguo ukimaliza pika chakula kitakachotufurahisha wote hapa mbwa
wewe mama yako hayupo hapa
Anna:
mama…
Shangazi:(kwa Anna) kelele (anarudi kwa Liliana) unasubiri nini umesahau kile kipigo cha jana?
Liliana:(anabeba nguo na kutoka nazo nje lakini kabla
hajatoka)
(maafisa wale waliokuja jana yake
wanaingia)
Shangazi:(anapigwa butwaa)
Elizabeth:
tulijua tu…kuwa unamtesa huyu mtoto…
Julieth:(anamuangalia Anna) asante sana kwa
ushirikiano wako
Anna:(kimya huku akimuangalia mama yake)
Edson:
mama unashtakiwa kwa kosa la kumnyanyasa mtoto mdogo na kumnyima haki zake za
msingi
Shangazi:(anashangaa sana) lakini huyu si mwanangu
Edson:
hatujaona kama unamlea kama mwanao
Julieth:(kwa maafisa wenzie) niliwaambia mimi
nilimuona mtoto ana vidonda vingi mwilini mwake na pia hana raha wala nini
nikajua hapa lazima ile taarifa tuliyopewa ni ukweli
Shangazi:(anashangaa sana)
Julieth:(kwa shangazi) ndo nikapata wazo la
kukukamata mara moja natamani hilo wazo ningeliwaza mapema Zaidi ila
hakijaaharibika kitu
FLASHBACK
(Inaanzia jana yake maafisa
walipoaga na kuondoka zao, nje kukawa na mazungumzo baina yao)
Julieth:
kuna kitu hapa…hizi taarifa tulizopata zina ukweli mtupu ndani yake mtoto ni
kweli kabisa anafanyishwa kazi na kupigwa sana na hiyo inaonyesha hata jinsi
anavyotuangalia anahitaji msaada wetu
Elizabeth:
nini kifanyike?
Julieth:
naomba namba ya mwalimu Monica
Elizabeth:(anampa) unataka kufanya nini Julieth?
Julieth:(anaichukua huku anawaongoza wenzie)
twendeni
(pamoja wanapanda gari walilokuja
nalo na kuliondoa mara moja)
Elizabeth:
bado hujanijibu…unataka kufanya nini?
Julieth:tunatakiwa
tumkamate shangazi akiwa anamfanyia unyama mtoto huyu
Elizabeth:
tutafanyaje?
Julieth:(anaipiga namba ya mwalimu Monica inaita
mwisho inapokelewa) Eliza...embu ongea kwanza atajua mara moja kuwa anaongea
na nani
Elizabeth:(anaipokea na kuiweka sikioni) eeh...Monica
mambo vipi shoga yangu
Mwl.Monica:
poa shoga kheri?
Elizabeth:
kheri mami…embu ongea na mwenzangu kuhusu ile inshu ya yule mtoto aliyekuwa
anateseka
Monica:
aaah!!!sawa mi niliambiwa na mwanafunzi wangu je mlienda?
Elizabeth:
ndio tulikuwepo hapa muda si mrefu ila hatujapata ushahidi
Julieth:(anampokonya simu) dada habari yako?
Monica:
salama vipi?
Julieth:
unaweza kuniunganisha na huyo mtoto aliyekuambia taarifa hizi?
Monica:
bila shaka kabisa...
Julieth:
sawa…sasa nitawakuta wapi?
Monica:
Njooni hapa shuleni bado yupo darasani nitamuita tu mara moja
Julieth:
sawa…tunakuja hapo sasa hivi
Monica:
sawa karibuni…
Elizabeth:
wewe noma…unadhani mtoto ataongea…
Julieth:
kitendo cha kumwambia mwalimu wake ni kwamba tayari amechoka na anamhurumia
sana mwenzie kwahiyo atafanya kila kitu amsaidie mwenzie
Elizabeth:
good plan
(Gari linaendelea kwenda
wanaendesha na baada ya dakika kadhaa wanafika shuleni hapo, haraka wanampigia
mwalimu monica na bila kupoteza muda mwalimu Monica anakuja kuwapokea)
Monica:
karibuni sana
Edson:
hatujaja rasmi…
Monica:
naelewa nitasema tu nyinyi ni ndugu zangu…
Julieth:
haya muite mtoto…
Monica:
tayari yupo ofisini kwangu maana mliposemaa hivyo nimemuandaa…
Elizabeth:mi
naona umuite tusimame nae pale chini ya mti tuwe kama vile tunapiga stori
Monica:
sawa (anaondoka kuelekea ofisini kwake na
baada ya muda anaruddi akiwa amemshika mkono Anna)
Julieth:
oh…binti mzuri mzuri hujambo?
Anna:
sijambo…shikamoo (kwa heshima
anawasalimia wote)
Maafisa:(wanaitikia pamoja)
Julieth:
haya...tuambie ulichomuambia mwalimu…kuhusu mtoto kuteseka
Anna:
huyo mtoto ni binamu yangu…ni mtoto wa shangazi yangu…wazazi wake walifariki
kwa ajali walipofariki wazazi wanguwakapewa jukumu la kumlea…sasa halelewi
inavyotaakiwa anapigwa, anafanya kazi zote na mbaya Zaidi baba yangu ambae ni
mjomba wake anambaka kila usiku…namhurumia sana na ni mtoto mdogo sana
Elizabeth:
sana jamani tutamsaidia…
Julieth:
sasa cha kufanya hapa ni kitu kimoja cha akili sana…nitakupa namba yangu...na
tutakuwa tumekaa sehemu standby akianza tu…mambo yake nipigie
Anna:
sina simu…
Edson:
unaweza kuchukua simu ya mama yako bila yeye kujua na ukafanya tulichokuambia
bila yeye kujua sawa ee
Anna:
sawa...
Elizabeth:
tunashukuru kwa msaada wako tunakutegemea sana…
Anna:
haina shida
Julieth:
poa basi tusipoteze muda sana mwanangu ni bora tukuache ili uendelee na masomo
(maafisa wanaondoka huku Anna na
mwalimu Monica wanaenda kuendelea na kazi zao)
END
OF FLASHBACK
Julieth:(kwa shangazi) sijui kama unaelewa kuwa unachofanya
ni kibaya mpaka mwanao anachukia hiyo hali kwahiyo huna cha kujitetea na tayari
polisi wapo nje hapo kukusindikiza rumande tunakufungulia mashtaka
(polisi wanakuja na kumshikilia
shangazi na kuondoka nae)
Shangazi:(anamuangalia Anna vibaya sana mithili ya
simba kaona swala na anataka kumla)
Anna:(wala hajali)
Bella:(Analia)
mama
Anna:(kimya huku kamkumbatia Liliana)
Bella:(kwa Anna) yaani sababu ya huu uchafu (anamnyooshea kidole Liliana) umemfanya
mama yetu kaenda jela
Anna:
wewe koma na tena ukome zaidi huyu sio hausigeli wenu ni mwenye nyumba hii
Bella:
nampigia baba sasa hivi…
Anna:
fanya haraka kabisa…mpigie huyo baba yako…huyo mbwa anayebaka…watoto wadogo na
bado yeye…tunatafuta ushahidi tu na yeye awekwe nguvuni
Bella:
una roho mbaya sana... (Anaingia ndani kwa
hasira)
Anna:(kwa Liliana) basi mdogo wangu…yameisha
mama na baba watalipakwa yale yote waliyokutendea usijali mama umesikia?
Liliana:
sawa…dada nashukuru kwa kunisaidia mama angekuwepo angekupa zawadi dada yangu (machozi yanamlenga) maskini wazazi wangu
wangekuwepo leo…ningekuwa shule nzuri mimi na sio shule hizi
Anna:
hapana usiseme hivyo mdogo wangu mimi nipo hapa kwa ajili yako na ninakupenda
sana na nitakuwa kama mama yako nitakupigania kama mama yako usijali
Liliana:
Asante dada Anna
Anna:
usijali
(Wanakumbatiana huku kila mmoja wao anaonekana ana furaha)
0 Comments