SCENE 11: -
(Ni asubuhi na mapema kumepambazuka vyema,
kwa kuwa ni siku ya jumapili watu wanaanza kwenda kwenye nyumba za ibada ili
kumshukuru Mungu, katika nyumba ya Liliana anapoishi kama mtumwa nao
wanajiandaa kwenda kanisani, Anna anampa Liliana gauni zuri ili nae aende
kumtukuza Mungu wake, wanajiandaa kutoka lakini kabla hawajatoka, shangazi
yaani mama yao Anna na Bella anaingia)
Bella:(kwa furaha isiyo ya kifani) mama… (anamkimbilia na kumkumbatia) shikamoo
mama…
Shangazi:
marahaba mwanangu (anamgeukia Anna)
hujafurahi kuniona
Anna:(anaonyesha hasira wazi) shikamoo mama
Liliana:(kwa sauti ya unyonge) shikamoo shangazi
Shangazi:(kwa jazba) pumbavu sana wewe yatima
usiyekuwa na wazazi wala ndugu
Anna:(anapandwa na hasira) mama…
Shangazi:(anaendelea kuongea kwa jazba) hivi kwa
mawazo yako ulidhani nitafungwa? mimi jeshi kubwa ndugu yangu na hakuna
atakaenishinda…umeelewa sio hao maafisa wala mapolisi wote nimewaweka kiganjani
mwangu
(Mjomba anaingia akitokea nje)
Shangazi:
mume wangu mpenzi amekuja leo asubuhi sana kunifanyia mpango nitoke
(Bella, shangazi na mjomba
wanacheka kwa dharau)
Anna:(anawaangalia kwa hasira sana)
Shangazi:(kwa Liliana) sasa nitakachokufanyia
hautaamini…yaani umenichokoza vibaya sana wewe ni wakunilia timing mimi?
Liliana:
sio mimi shangazi mimi nitawezaje kupigana na wewe shangazi?
Anna:(anasikia uchungu sana) mama ni mimi ndo
nilimwambia mwalimu na wale maafisa wakaja nyumbani kwetu siku ile sorry sio
nyumbani kwetu nyumbani kwa Liliana
Shangazi:(anacheka kwa dharau) eti nyumbani kwa
kina Liliana…. yeye hana chake hapa mama yangu na nikikumbuka ulivyokuwaga
unadeka tukija hapa ndo tunakuwa wafanya kazi wako ni muda wetu sasa wa kutesa
hiyo inaitwa kutesa kwa zamu
Anna:
unatesea kwenye nyumba ya watu? mama Liliana alifanya fadhila kukubali sisi ndo
tumlee alipokubali tuje tuishi nae…inakuwa sio vizuri wala sio busara
tunachofanya kumbuka tulipokuwa na leo hii tunaishi pazuri
Mjomba:(anaingilia) kimya wewe mtoto usiyekuwa
na heshima hata kidogo kwa wazazi wako…wewe unajua nini?
Anna:
sijui chochote Zaidi ya kumuonea huruma binamu yangu…
Shangazi:
eti binamu…yaani undugu ulikufa siku wazazi wake walipokufa
Anna:
hapo ndipo mnapokosea wazazi wangu na ndio maana basi baba anambaka binamu kwa
kisingizio kuwa undugu umekwisha…
Mjomba:(anashikwa na kigugumizi) nani…alikuambia?
Anna:
nilikuona jana usiku kwa macho yangu, ulimtoa Liliana chumbani kwetu na
kumpeleka stoo… (anatokwa na machozi)
baba…Liliana bado mtoto sana bora hata angekuwa mkubwa kidogo jamani…maskini
hawezi hata kujisimaia hawezi hata kupiga kelele kwahofu yakwamba utamuua
Mjomba:(anainamisha kichwa)
Shangazi:
utakuwa ulikuwa unaota mwanangu
Anna:
nilimuona kwa macho yangu mawili na wala sio ndoto mama…ila tu nilishindwa
kufanya lolote kwa aibu niliyopata sikutaka kuamini kuwa baba yangu mzazi
anaweza kumfanyia haya mpwa wake…
Shangazi:
acha kumshuhudia uongo baba yako Anna
Bella:(amekaa kimya huku anakumbuka kuwa hata yeye
alimuona baba yake akimchukua Liliana na kwenda nae nje)
Anna:
sisemi uongo mama sasa niseme uongo inisaidie nini mimi?
Shangazi:
mume wangu hawezi kufanya kitu cha kipuuzi kama hicho…
Anna:(machozi yanamtoka) najuta na ninajionea
aibu kwamba huyu baba ni baba yangu mzazi
Shangazi:
acha kuongea upumbavu wewe mtoto usiye na akili vizuri
Liliana:
dada acha tu msije mkagombana…na wazazi wako
Anna:
naishangaa hii serikali hivi polisi inashindwa kutetea haki za watoto mpaka
watu wanapata nafasi ya kupata dhamana hata baada ya kuwepo kwa ushahidi wa
kutosha?
Shangazi:(anacheka kwa dharau) ushahidi haukuwepo
ndo maana nilipatiwa dhamana… hakuna atakayeniweza kwa hili
Anna:
pengine uko sawa au pengine hauko sawa kila kitu kipo mikononi mwa Mungu
Shangazi:
Mungu??/Mungu gani unayemzungumzia wewe
Anna:
aliyeziumba mbingu na dunia na kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana…ni
kweli leo umetoka kwa dhamana na ni kweli baba unajifanya hujui nachozungumzia
ila amini nakwambia ipo siku Mungu atakuadhibu kwa jinsi anavyojua Mungu huyu
sio kipofu wala kiziwi hata asione wala asisikie yeye ni mkuu na yeye peke yake
ndo atawaadhibu… (anamshika mkono Liliana)
twende mdogo wangu…
Shangazi:
unadhani kuna sehemu ataenda huyu mbwa? haendi popote…nimerudi unadhani ni nani
atanitengea maji ya kuoga na kunipikia chakula
Anna:
mama, Liliana bado mtoto mdogo anahitaji kuishi maisha yake kama mtoto mdogo
Shangazi:
nitakutandika…wewe unajua nini? hujui lolote mshenzi wewe unajifanya kubishana
na mimi unadhani utanishinda? bora uwe mpole na kufata nayokuambia…mimi ndo
mkuu na malkia wa nyumba hii na nitabakikuwa hivyo hata wazazi wa huyu mbwa
wakifufuka hakuna atakayenishinda
Anna:
mama mbona uko hivi jamani mama yangu?
Shangazi:(anamvuta Liliana kwa nguvu) embu njoo
huku jikoni
Anna:(anajaribu kumsaidia Liliana)
Shangazi:(kwa Anna) acha kujifanya una huruma
mshenzi wewe, wewe ni mwanangu na ni lazima uwe kama mimi na si vinginevyo (anamsukumiza Liliana kwa nguvu) nenda
jikoni haraka mshenzi wewe… nipikie chai na uniandalie maji ya kuoga…
Liliana:(anatembea taratibu)
Shangazi:(anamfuata na kumpiga vibaya sana kisha
anamsukuma)
Liliana:(anaanguka chini) shangazi
Shangazi:
ninakutuma kitu naomba uelewe...kwamba nikimtuma mtu kitu nataka afanye haraka na
si kujivuta
Liliana:
samahani shangazi…nisamehe shangazi
Shangazi:
leo hautakula chakula chochote…unaniletea mimi madeko nimekuwa mama yako?
mfuate kaburini…na sijui ilikuwaje tu wakazikwa kwenye uwanja huu nitaenda
kuwafukua nitupe mifupa yao huko nje
Liliana:(Analia sana)
Anna:(anajikuta anatokwa na machozi)
Liliana:
shangazi nimeumia…
Shangazi:
kwahiyo kama umeumia mimi itanisaidia nini? au inanihusu nini? nitakuadhibu kwa
kunifanya mjinga mwenzio na kwenda kuwaita hao wajinga wenzio hapa eti
wanikamate
Anna:
nimesema mimi ndo niliwaita hapa
Shangazi:
sijali, hasira zangu zote zipo kwa huyu mbwa.,.
Anna:
nitakutengea maji na kanisani siendi tena…nakupikia chai Liliana ameumia
Shangazi:
nataka afanye hivyohivyo asilete uzuri hapa
(Liliana
anaenda jikoni huku Anna anamfuata nyuma, wanawasha jiko kwa kusaidiana
wanafanya kila kitu anachotaka shangazi ambae kwa sasa anajiita malkia wa
nyumba ile ya kifahari. wakati Anna na Liliana wanafanya kazi Bella, shangazi
na mjomba wamekaa sebuleni kama mabosi Fulani.Liliana na Anna wanaendelea na
shughuli zao bila kipingamizi)
Anna: Vumilia binamu yangu
Liliana: nimewakumbuka sana
wazazi wangu
Anna: jikaze binamu jamani
Liliana: natamani kujikaza lakini
siwezi nimechoka natamani kufa Anna
Anna; usiseme hivyo sasa ukifa
mimi nitabaki na nani
Liliana: na Bella
Anna: (anaguna kidogo)
Liliana: mbona unaguna?
Anna: acha tu binamu (anaendelea na kazi za hapa na pale)
0 Comments