SCENE 9: -
(asubuhi ya siku nyingine tena
Liliana akiwa anaendelea na kazi zake za kila siku kama mfanyakazi wa nyumba hiyo,
ghafla mlango wa sebuleni unagongwa, kwa kujivuta shangazi yake anaufungua
mlango na kukutana na watu ambao hawafahamu)
Shangazi:
karibuni
Watu:
asante sana…
Mwanamke
1: habari za hapa?
Shangazi:
salama…
Mwanaume:
tunaomba uturuhusu tuingie sisi ni maafisa kutoka taasisi ya haki za
watoto…tunaomba tuzungumze mawili matatu...
Shangazi:(anasita kidogo) kuna nini? mbona
siwaelewi?
Mwnamke
2: turuhusu tuingie tutakujuza usijali
Shangazi:(anawaruhusu kishingo upande)
(Maafisa wanaingia ndani na
kuketi)
Shangazi:
niwahudumie nini? chai, kahawa, juisi au nini?
Mwanaume:
usijali tupo sawa kabisa…asante kwa kujali
Shangazi;(anakaa kimya na amepooza kama kuku kamwagiwa
maji)
Mwanamke1:
ndio kwanza tujitambulishe labda kwa majina yetu…mimi naitwa Elizabeth Kapera
Mwanamke
2: mimi naitwa Julieth Julius
Mwanaume:na
mimi naitwa Edson Edward…
Elizabeth:na
sisi ni maafisa wa haki za watoto…tunaangalia haki za watoto majumbani na
mashuleni
Shangazi:
sawa…kwahiyo niwasaidie nini?
Elizabeth:
kuna watoto wangapi hapa?
Shangazi:
wawili…wanangu…Anna na Bella
(Liliana anapita akiwa anaelekea
chumba cha kina Anna)
Julieth:na
huyo?
Shangazi:
oh(anajichekesha)uzee nao mzigo si
nilimsahau…ndio na yeye ni mtoto anakaa hapa…
Elizabeth:
okay (anajisemea moyoni) okay sasa
huyu mtoto anaweza kuwa ndo huyo mtoto…
Julieth:
kuna mtu kweli anaweza kusahau idadi ya watoto wanaoishi nao?
Shangazi:(anajichekesha)
Elizabeth:
hao watoto wawili uliowataja wako wapi?
Shangazi:
wapo shuleni
Julieth:
huyu yeye haendi?
Shangazi:(anajichekesha)
Edson:
unajua…sisi tumepata habari nyingi sana kuhusu huyu mtoto…
Shangazi:(anaanza kutetemeka) habari gani?
Elizabeth:
huyo mtoto anaitwa Liliana…ni mtoto wa marehemu wifi yako…hii nyumba ni yake
yaani ya wazazi wake lakini anaishi kama mtumwa, mnamnyanyasa sana mpaka
kimwili
Shangazi:
hapana hiyo sio kweli…
Elizabeth:
anabakwa huyu mtoto…
Shangazi:
tumuite tumuulize habari hizo…
(maafisa
wanaangaliana)
Elizabeth:
muite…
Shangazi
:(ananyanyuka kisha anaenda alipo Liliana
na kumnong’oneza jambo Fulani) wakikuuliza chochote usiseme ukweli na
ukisema ukweli nitakumaliza umeelewa?
Liliana;(kwa unyonge anaitikia) sawa shangazi
Shangazi:(anarudi sebuleni huku anajichekesha)
mtoto anapenda kazi huyu
Elizabeth:
anapenda kazi au unamlazimisha azipende
Shangazi:si
anakuja mumuulize…
Elizabeth:(anaguna)
Liliana:(anakuja huku akiwa amenyong’onyea sana)
Julieth:
maskini…halafu mtoto mdogo sana…mbona kama huna raha (anamvuta na kumpakata) eti mama mbona huna raha hivyo? Unateswa?
Liliana:(anatikisa kichwa kuashiria kukataa)
Elizabeth:(anamuita) haya njoo uniambie mimi
mwanangu
Liliana:(anaenda kwa Elizabeth huku anamuangalia
shangazi yake)
Elizabeth:
nambie shangazi huwa anakupiga? je huwa unapika na kufanya kazi zote? mjomba
je…huwa anakufanyaje usiku?
Liliana:(anajikuta anatokwa na machozi)
Shangazi:(anaanza kuingiwa wasiwasi)
Edson:
usimuangalie shangazi
Liliana:(yupo kama vile kuna kitu anawaza)
Elizabeth:
niambie…mwanangu hakuna atakayekupiga…sisi tupo…
Shangazi:
labda hataki kusema jamani mbona hivyo?
Elizabeth:
nadhani mama ungetuacha na mtoto…tumuulize maswali mawili matatu…
Shangazi:
muulizeni na mimi ni mlezi wake nina haki ya kuwepo hapa
Edson:
mtoto anaonekana hana raha na wewe…kabisa jamani
Shangazi:
ndo alivyo huyu akiona watu mbona tukiwepo peke yetu hafanyi hivi?
Julieth:(anamuangalia shangazi kwa muda)
Shangazi:(anaonyesha jazba)
Julieth:
twendeni…jamani haya mambo ya familia
Shangazi:
wewe una akili mwaya…eti mnanifukuza kwangu
Elizabeth:
nisamehe mama
(wanaondoka kuelekea nje)
Julieth:
kuna kitu hapa taarifa tulizopata ni za kweli kabisa na mtoto anaonekana kabisa
kuwa anateseka anapigwa na kufanya kazi na anaumia sana…we fikiria kitendo cha
kumuuliza tu mtoto mdogo kama yule machozi yanamtoka yenyewe yaani ndo muone
kuwa ana uchungu wa muda mrefu
Elizabeth:
nini kifanyike?
Julieth:
nitawaambia wala msijali huyu mtoto lazima tumtoe kwenye mateso haya makali…
Elizabeth:
una mpango gani?
Julieth:
naomba namba ya mwalimu Monica kama hautajali
Elizabeth:(anachukua simu kisha anampa namba za mwalimu
Monica)
Julieth:(anazichukua na kuziandika katika simu yake)
okay asante sana…twendeni…
(Kwa pamoja wanaondoka mahali pale)
(Huku ndani walipo Liliana na
shangazi yake kipigo kwa Liliana kinaendelea, mtoto anapigwa kama mbwa)
Liliana:(kwa uchungu) nisamehee shangazi
Shangazi:
wewe ulishindwa kuonyesha uso wa furaha? kwani huli humu ndani?
Liliana:(huku Analia kwa uchungu) nisamehe
shangazi sitarudia tena
Shangazi:(anampiga na mikanda mara kadhaa tena kwa
nguvu na bila huruma) kufa mshenzi wewe
Liliana:(anazimia)
Shangazi: mshenzi Sana...KUFAAA!!!
(Anaingia ndani akimuacha hapo bila
msaada wowote)
0 Comments