SCENE 12
(Majira ya saa tatu usiku Liliana
anaingia chumbani kwake ambapo ni stoo, anaonekana amechoka sana na kazi za
siku ile, anajilaza lakini baada ya kama dakika tano shangazi yake anakuja
akiwa amefura kwa hasira)
Shangazi:
wewe Malaya mbwa…vile vyombo tulivyovitumia umemuachia nani? au kuna mama yako
hapa wa kuviosha?
Anna:(anakuja) mama Liliana amechoka sana na
anaonekana anaumwa sana
Shangazi:
haumwi huyu anajifanyisha tu mshenzi sana huyu mtoto…mvivu sana (anaanza kumpiga na fimbo kubwa aliyoiweka
stoo humo kwa ajili ya kumpigia Liliana kila mara amekutwa na kosa Fulani)
Anna:
mama…huyu mtoto anaumwa
Shangazi:
afe…mshenzi sana huyu anatudekeadekea hapa utasema sisi ni wazazi wake awafate
sasa ili na sisi tupumzike na kulea mtoto asiye na msaada wowote (anampiga sana) kufa (anaona haitoshi anamkaba shingo) kufa
Anna:
mama…jamani (anatoka na kukimbilia kwa majirani)
jamani majirani
(Baadhi ya majirani wanatoka)
Mama:
nini Anna?
Anna:
mama anampiga sana binamu yaani anamkaba kama anataka kumuua tafadhali
nisaidieni…
Jirani:
jamani…
(Majirani wanakimbilia nyumbani
kwa kina Anna na kumkuta kweli Liliana anapigwa vibaya sana)
Jirani
1: jamani wewe mwanamke mbona huna huruma
Shangazi:
inawahusu nini? huyu ni mwanangu nina mamlaka ya kumpia nitakavyo
Mama:
jamani mtoto analala na makorokoro kibao jamani…huyu ni mwanao kweli?
Liliana:(anapata nafasi na kukimbilia nje na
kutokomea kusikojulikana)
Jirani
2: usikimbie…
Mama:
keshakimbia na usiku huu sijui itakuwaje mi naona tuwapigie simu polisi
wamtafute sasa hivi ni usiku sana na hatutampata kirahisi
Anna:
twendeni sisi wenyewe tukamtafute binamu yanu ni mtoto mdogo tu yanaweza
kumkuta makubwa…huko
Jirani
1: hapana hatuwezi kumpata katuacha mbali sana na wala hatuwezi kujua ameelekea
wapi
Shangazi:(amesimama hapo kama sanamu akiwasikiliza
wanavyopanga mikakati ya kumpata mtoto Liliana)
Mama:(anasogea pembeni kidogo na kupiga simu)
Jirani1:
ila sio vizuri kumtesa huyu mtoto na kila siku tunasikia huyu mtoto Analia kwa
uchungu huwa tunaona ni masuala ya familia yao na hatuwezi kuingilia
Shangazi:(kwa kejeli) kilichowaleta leo ni nini?
Jirani1:
Anna amekuja kutuita…. ya leo ilikuwa kali mpaka umefika hatua ya kumkaba mtoto
mdogo kama yule loh…wewe mwanamke ulaaniwe ona sura lako lilivyo baya kama roho
yako loh…!!!
Mama:(anarudi) aisee polisi hawawezi
kutusaidia labda mpaka keho
Jirani
2: hawa polisi nao…
Anna:
naomba nikamtafute mwenyewe
Mama:
acha tu mwanangu…Mungu atamlinda usiku huu
(Majirani wanaondoka na kurudi
majumbani kwao)
Shangazi:(kwa Anna) haya haraka nenda kalale
kujifanya wewe ndo steringi wa muvi kusaidia watu
Anna:(anaenda kulala huku Analia sana)
(Upande wa Liliana anakimbia
kuelekea shuleni kwao, shule ya msingi ya kata na kujihifadhi huko)
Liliana:(analala pembeni kidogo ya geti huku anaongea
na kumuomba Mungu wake) Mungu kwanini uliwachukua wazazi wangu kwanini
usingenichukua mimi? nateseka sana sili chakula kizuri tangu wazazi wangu
walipofariki na wala sivai nguo nzuri…nguo zangu zote nzuri amepewa Bella mimi silali
pazuri…ile nyumba ni ya wazazi wangu lakini leo hii naishi kwa kufanyishwa kazi
siku nzima hata kusoma imekuwa ni mtihani kwangu…napigwa sana…silali nafanya
kazi kama punda jamani (Analia sana na
kwa uchungu sana)
Mlinzi
:( anakuja baada ya kusikia mtoto Analia)
nani huyo Analia?
Liliana:(anafuta machozi) shikamoo anko…
Mlinzi:
marahaba…mbona upo hapa?
Liliana:
nimetoroka nyumbani shangazi amenipiga sana na nina njaa sana…
Mlinzi:(anamuangalia kwa matamanio makubwa sana)
unataka chakula?
Liliana:
ndio anko naomba unisaidie chakula
Mlinzi:(anaangalia huku na huku) nisaidie kwanza
mimi kisha nitakusaidia au unaonaje?
Liliana:
mimi sina cha kukusaidia anko
Mlinzi:(anajichekesha kama mwenda wazimu) unacho
kizuri sana kuliko chakula nipe tu…nitakupa chakula maana bado hapa kuna baa
nyingine bado ziko wazi nitakununulia chipsi
Liliana:
sawa tu ilimradi tu mimi nipate chakula na sehemu ya kulala…
Mlinzi:
sawa (anaanza kumshikashika)
Liliana:(kwa kuhamaki kidogo) nini hiyo…?
Mlinzi:
huo msaada niliokuomba…nafanya tu kidogo halafu nakupa juisi na chipsi…
Liliana:(anajikuta anakubali)
Mlinzi
:( anamvua nguo huku anachekelea kama
mjinga huku anavaa mpira)
Liliana
:( Analia sana)
Mlinzi:
wewe nae sasa unalia nini?
(Bila huruma mlinzi yule anambaka
mtoto mdogo sana ambae hata bado hajapevuka tena mwenye umri mdogo wa miaka
saba tu, dhambi kubwa sana na unyama mkubwa)
Mlinzi:(anafanya kitendo hicho mpaka anatosheka
wakati huo Liliana Analia sana huku akimtaja mama yake aje amsaidie) safi
sana… (ananyanyuka na kuvaa suruali yake
huku anacheka kidogo) haya binti nyanyuka na uende zako…hakuna msaada
wowote hapa…
Liliana
:( anashikwa na bumbuwazi) si
uliniambia kuwa utanipa msaada nikikupa msaada
Mlinzi:
sasa unahisi...saa nne hii natoa wapi chakula na pia hapa utaniletea shida tu
wakikukuta umelala hapa…sitaki kesi…nina watoto nyumbani na mke na wanategemea
kazi yangu hii sina msaada na wewe ondoka
Liliana
:( Analia Sana) lakini mwenzio nina
njaa…
Mlinzi:
hainihusu hata kidogo kwakweli
Liliana:
nisaidie sijala tangu asubuhi na pia tumbo linaniuma
Mlinzi:
kafie mbele huko…toka
Liliana
:( Analia kwa uchungu) sasa mimi
nitaenda kula wapi
Mlinzi:
yaani Hilo swali unaniuliza Mimi…una akili kweli wewe?
Liliana
:( anashikwa hasira) ipo siku moja
nitakujeruhi vibaya Sana Zaidi na ulivyonifanyia leo
Mlinzi:si
ndo mpaka unipate… (anacheka sana)
kafie mbele huko…
Liliana
:( anaondoka huku Analia sana)
amenifanyia hivi…amenibaka kisha akaninyima chakula (Analia) sawa tu…
Mlinzi:
eti…atanijeruhi…lini sasa? ila nimeenjoi…kaatoto kadogo ila dah…kapo vizuri
sijui nikaite tena nikadanganye
Liliana:(anaondoka huku Analia sana) kuna watu
wabaya sana bora mjomba alikuwa ananibaka lakini ananipa chakula…huyu amenibaka
kanidanganya kuhusu chakula kisha akanicha solemba bila hata maji ya kunywa jamani…
Mlinzi:(bado anamcheka kwa kejeli na dharau)
chombo cha starehe… (anacheka sana)
Liliana:(anamgeukia kumuangalia vizuri) nataka
kuukariri uso wako ili siku nikikuona tena nisikusahau… (anaugulia tumbo) njaa sana…
(Kuna mama anapita na vitafunwa
na anaonekana anatoka kuuza maandazi kwa wanywa kahawa na tangawizi usiku)
Liliana:(anamkimbilia) mama…samahani naomba
andazi moja sijala toka asubuhi
Mama:(kwa huruma anatua mzigo wake anaosha kikombe
anamimina chai anatoa maandazi manne na kumpa ale) haya mwanangu wewe kula tu...mi
naenda
Liliana:na
vyombo je?
Mama:
tumia tu (anabeba mizigo yake na
kuondoka)
Liliana:(anakula harakaharaka) asante Mungu… (anakula mwisho anamaliza) nimeshiba… (anaenda kwenye mtaro na kujilaza hapo)
0 Comments