SCENE 13: -
(Liliana anatembeatembea huku na
huku na anaonekana amechoka sana na kwakuwa ana njaa sana anaomba msaada watu
mbalimbali)
Liliana:
naomba unisaidie mama…nina njaa
Mwanamke:
embu toka hapa…kwani huna wazazi? Mnakimbia kwenu mnakuja kusumbua watu mitaani
(anamsukuma) embu toka hapa (Anaondoka zake)
Liliana:(anaanguka na anajikuta Analia sana) sina
mama wala baba na wala sina ndugu…nipo peke yangu kwenye hii dunia
Mwanamke:(anampuuzia na kuondoka zake)
Liliana:(Analia sana tena kwa uchungu sana) mama…uko
wapi? nateseka mimi…nimekimbia kutoka kwenye nyumba yangu kabisa…na sasa sina hata
sehemu ya kula wala kulala ...mama, baba kwanini mliniacha…napigwa nabakwa… (anapiga magoti) Mungu nimeumizwa sana
maishani mwangu kwanini usinichukue tu, nichukue tu na mimi niende kwa baba na
mama yangu nikapumzike sitaki kuishi tena nimechoka Mungu wangu
(Watu wanampita tu tena wengine
wanamuona kichaa)
Liliana:(anaendelea kulia sana kwa uchungu)
(Upande wa nyumbani kwao kina Liliana
walipo mjomba, shangazi na binamu zake)
Anna:(anaonekana hana raha kabisa)
Belle:
sasa kama aliamua kuondoka si tumuache?
Shangazi:
atajua mwenyewe bwana…mtoto kaanza umalaya akiwa bado mdogo atakuwa ameenda kwa
wanaume wake
Anna:
mtoto wa miiaka saba mama?
Shangazi:
anashindwa nini?
Anna:
sidhani na kwanini tusiende kutoa taarifa polisi
Shangazi:
embu niondokee na upuuzi wako hapa
Anna:
mama embu fikiria chukua mud ahata dakika moja mama tumia ubinadamu mama na
tumtafute Liliana kwanza tunakaa kwenye nyumba yao…ambayo ni nyumba yake…
Shangazi:
hivi huyo Liliana akija akadai hii nyumba unadhani utakuwa na sehemu ya kukaa?
Anna:
sidhani kama Liliana ana roho mbaya…
Shangazi
huna hata aibu mshenzi wewe kaa utulie hapo na unisikilize mimi…mimi ndo mama
yako na ndo mwenye maamuzi hapa nyumbani hata baba yenu hana usemi
Mjomba:(amekaa kimya hana usemi)
Shangazi:au
nadanganya (anamuangalia mumewe)
Mjomba:
hapana hudanganyi mke wangu wewe ndo mwenye maamuzi yote
Anna:(anashangaa sana) baba…wewe si ndo kichwa
cha familia yetu? na hii nyumba ni ya dada yako na mumewe…inakuwaje huna
maamuzi yoyote?
Shangazi:(anamnong’oneza) ukinigeuka tu nitaenda
polisi kusema ni kweli ulikuwa unambaka mpwa wako si unajua adhabu ya kubaka?
sio polisi tu hata jamii nzima itakuadhibu…kwahiyo kaa hapo utulie na
kunisikiliza maamuzi yangu yote
Mjomba:(kwa unyonge) sawa…usijali
Anna:
baba kuna nini?
Mjomba:
yaache tu mwanangu…na kama binamu yako amepotea basi hiyo ni kazi ya Mungu
kumtunza au kumrudisha sio jukumu letu
Anna:(anashangaa sana) baba
Mjomba:(ananyanyuka na kuingia chumbani kwake)
Shangazi:(anacheka kwa kejeli)
Anna:
baba kuna nini lakini?
Mjomba:(anaingia ndani na kufunga mlango)
Anna:
mama…
Shangazi:
embu usinsumbue na huyo sijui binamu yako…acha afie huko…hana faida
Anna:
mama
Shangazi:
kapike huku msichana wenu wa kazi kakimbia (anacheka
kama mazuri) kuanzia leo utakuwa unapika mpaka pale tutakapopata msichana
wa kazi
Anna:(anasikitika)
Shangazi:
fanya tu kazi mwanangu kesho tu nakuletea msichana wa kazi (anaingia ndani alipo mumewe)
Mjomba:
unachofanya sio kizuri kabisa mama Anna…
Shangazi:
nafanya nini?
Mjomba:
kila kitu…
Shangazi:
wewe je ulichofanya ndo kizuri?
Mjomba:
sio kizuri na ninajuta kumbaka mtoto wa marehemu dada yangu…na ninatamani
nimuone mpwa wangu na kumuomba msamaha na kumrudisha aishi hapa kama malkia wa
nyumba hii maana hii nyumba ni ya kwake
Shangazi:(anashikwa na hasira) nyamaza na
nikusikie tena unaongea kuhusu huyo mdudu kurudi kwenye nyumba yangu nzuri kama
(anaangalia huku na huku) hii wanangu
wanahitaji maisha haya na sio maisha tuliokuwa tunaishi
Mjomba:
hii nyumba na haya maisha sio yetu mama Anna haya maisha ni ya Liliana mtoto
uliyekuwa unampiga kama punda uliyekuwa unamlaza na panya stoo…
Shangazi:
maisha yake yalikufa pamoja na wazazi wake…na usinichanganye nitaongea siri
nyingi tu…usinichezee tena usinichezee kweli
(Wakati huo Anna anapita nje ya
chumba hicho, ila anajikuta anasimama kusikiliza maongezi ya wazazi wake)
Shangazi:
nitawaambia watoto na huyo panya unaetaka arudi…
Mjomba:
nimejuta maisha yangu yote na tangu dada yangu amekufa sina amani kabisa
Anna:(anajisemea moyoni) nini kinaendelea…
Shangazi:
unaweza ukaniona mimi ndo mtu mbaya ila wewe ndo mbaya Zaidi na hii roho
nilionayo sasa ni wewe ndo umenifundisha mara baada ya kuona unaweza kufanya
chochote hata kwa ndugu yako ili upate maisha mazuri…
Mjomba:
ongea taratibu mama Anna…
Shangazi:
ulimuua dada yako na shemeji yako na ukataka kumuua na mpwa wako ili upate
maisha mazuri…kwa bahati mbaya mtoto akapona…ilikuudhi sana hiyo hali ulikubali
kumlea mtoto ila ukapanga kumkomesha kwa kumtesa sana ili aondoke mwenyewe…sasa
leo unataka arudi ili iweje huku wewe mwenyewe ulipanga yote haya?
Anna:(anaziba mdomo kwa mshangao)
Mjomba:
ninajuta tena najuta sana kwa kusababisha ajali kwa kukata breki kwenye gari ya
dada yangu…
Shangazi:
sasa wewe unadhani…umenionjesha maisha mazuri halafu sasa hivi unataka kunifanyaje?
wewe tulia ameshaondoka na hicho tulichokuwa tunataka
Anna:(anasikitika sana) Mungu wangu…baba ndo
alisababisha ajali kwa wazazi wa Liliana? aisee (anaondoka na kukimbilia
chumbani kwake)
Mjomba:
lakini wewe ndo ulinishauri
Shangazi:
ulikuwa na uwezo wa kukataa nakusimamia kwenye msimamo wako…badala yake usiku
ule ulikuja hapa na kukata breki na kurudi nyumbani bila mtu yeyote
kukuona…kwahiyo kila mtu anajua kuwa ilikuwa ni ajali
Mjomba:(anasikitika sana) najuta kwa kila kitu
Shangazi:
pole (ananyanyuka na kuondoka zake)
Mjomba:(anabaki anasikitika na kujuta kwa kila kitu alichowahi kufanya kwa
kifupi moyo wake unauma kwa matokeo yaliyotokea kwa matendo yake)
Shangazi: (anamchungulia mume wake)
0 Comments