SCENE 14: -
(Liliana anatembea njiani na
anaonekana ana njaa na amechoka sana, Analia sana na anaonekana amekata tamaa
kabisa na maisha)
Liliana:
bora ningekufa tu (Analia)kuliko
kuteseka hivi bora nife tu
(Wakati Liliana analaani na
kutamani kifo kuna gari linamfuata kwa nyuma yake na linaenda kwa mwendo mdogo
sana na inaonekana huyo mtu kama anamvizia liliana)
Liliana:(anagundua gari nyuma yake anajaribu
kukimbia)
Mtu
kwenye gari:(anajaribu kumuita)
Liliana:(anasimama na kuangalia nyuma anagundua kuwa ni
mwanamke mrembo sana mwenye umri kati ya miaka 40 mpaka 45)
Mwanamke:
hata usiogope mwanangu…sitakudhuru nakuahidi hivyo
Liliana:(anaanza kulia) niue tu maana nimechoka
sana kuishi niue tu mama nigonge na gari yako nife mama
Mwanamke:
siwezi kukuua wala kukudhuru (anashuka
kwenye gari lake la kifahari) usijali…nimekuona muda mrefu sana unaonekana
una uchungu sana…mtoto mdogo sana wewe nini kinaweza kuwa kinakusumbua
mwanangu?
Liliana:ni
hadithi ndefu sana…mimi ni yatima sina mama wala baba
Mwanamke:na
ndugu je?
Liliana:(anaendelea kulia sana) ni hadithi ndefu
sana…
Mwanamke:
mimi naitwa Bianca…ni mfanyabiashara nina biashara nyingi sana sijaolewa na
wala sina mtoto…na ninatamani sana kuwa na mtoto wa kuishi nae
Liliana:(anaogopa sana)
Bianca:
twende nyumbani kwangu
Liliana:
hapana… (Anakataa na kujaribu kukimbia)
Bianca:
mimi nakuhakikishia kuwa sitakudhuru nataka mtoto tu…jamani wanaume wangu
wananikimbia maana sijawahi kumzalia yeyote hapo nimemuomba Mungu anipe mtoto…
Liliana:(anakimbia na kumuacha Bianca hapo)
Bianca:
jamani mi wala sina nia mbaya jamani ninatamani tu mtoto wa kuishi nae sina
mtoto nina wafanyakazi tu na sina Amani…nahisi mtoto atanipa Amani
nayotafuta…nimemuona huyu mtoto tangu jana…na nimewaza tu kuwa anahitaji
msaada…
Liliana:(anajikuta anarudi alipo Bianca)
Bianca:(anajiandaa kupanda gari lake ili aondoke)
Liliana:
mama…
Bianca:(anamgeukia) nambie mwanangu?
Liliana:
naumwa tumbo…
Bianca:
una njaa mwanangu...twende nyumbani…
Liliana:(anapanda kwenye gari ingawa anaonekana ana
wasiwasi sana)
Bianca:
usiogope nimekufatilia kama siku mbili hivi sio nimekurupuka…sina mtoto na nina
mali nyingi sana…ninaishi na wafanyakazi kuna mtunza bustani kuna dada wa usafi,
kuna mpishi kuna mlinzi wote hao hawanipi ile faraja nayotamani kupata…nahitaji
mtoto
Liliana
:( anamuangalia chinichini)
Bianca
:( anachukua biskuti na kumpa) kula
hizi biskuti kabla hatujafika nyumbani…
Liliana
:( kwakuwa ana njaa Sana anapokea na
kuanza kula)
(Wanaendelea na safari na baada
ya muda wanafika katika jumba safi la kifahari la Bianca.Bianca anapiga honi na
haraka mlinzi anafungua geti)
Mlinzi:
shikamoo anti
Bianca:
marahaba…funga geti…
Dada
wa usafi: shikamoo anti…
Bianca:
marahaba… (Anaegesha gari katika
maegesho)
Mpishi
:(anafungua buti na kutoa vitu) leo
naona umekuja na mgeni
Bianca:(anatabasamu)
ndio…ingawa mwenyewe hajiamini… anaogopa kweli yaani (kwa Liliana) karibu nyumbani mwanangu
Liliana:(anawasalimia wote)
(Wafanyakazi wote wa nyumba ile
kasoro mtunza bustani wanamuitikia)
Mtunza
bustani (ndo anafika) shikamoo anti…
Bianca:
marahaba (kwa Liliana) naomba
nikutambulishe mwanangu…huyu dada wa usafi anaitwa Husna
Husna:
karibu…
Bianca:
mpishi jina lake ni Siwema
Siwema:
karibu sana
Bianca:
mtunza bustani ni Mbise
Mbise:
karibu sana
Bianca:na
mlinzi anaitwa Lupemba
Lupemba:
karibu sana
Bianca:(kwa wafanya kazi wake) huyu anaitwa… (anamuangalia Liliana) jitambulishe
Liliana:
mimi naitwa Liliana
Siwema:
oh…jina zuri
Bianca:
kwanzia leo yeye ni mwanangu…nimemuona mtaani muda mrefu sana nikamuonea huruma
sana…leo nimemuona sana nikaona nisimuache. nimlete nyumbani yeye sasa ni binti
yangu nitamlea ingawa simjui alipotoka…karibu nyumbani Liliana
Liliana:(anatabasamu) asante…
Husna:(anaangalia angalia huku na huku) nguo
zake ziko wapi?
Liliana:
sina nguo…
Bianca:
twende nikakuonyeshe chumba chako upumzike…wakati huo Siwema andaa
chakula…nikimaliza kumuonyesha chumba chake aoge, ale kisha apumzike
Siwema:
chakula kipo anti…
Bianca:
sawa (kwa Liliana) twende ndani…
(Wanaingia ndani nyumba ni ya kifahari kweli
kweli na inapendeza sana kila kitu ni cha gharama, Bianca anamchukua Liliana na
kwenda nae chumba kimoja kizuri sana)
Bianca:
hiki chumba nilipanga kumpa mwanangu na kwakuwa Mungu hajanipa mtoto…basi wewe
ndo mmiliki wa chumba hiki…
Liliana:(bado ana wasiwasi) asante
Bianca:
niite mama…tafadhali…
Liliana:
asante mama
Bianca:
usijali…umekipenda?
Liliana:
ndio ni kizuri… (anakumbuka alivyokuwa
analala stoo) asante mama
Bianca:
usijali…basi oga…kisha uje tule Siwema atakuwa anatenga ili tule...
Liliana:
sawa…
Bianca:(anafungua mlango wa bafu la kifahari
lililopo chumbani humo) oga mwanangu au nikuogeshe
Liliana:
nitaoga tu mama ninajua kuoga
Bianca:
haya mwanangu…ukimaliza uje upate chakula kisha upumzike kidogo…nimeona una
vidonda vingi nitakupeleka hospitali
Liliana:
sawa mama
Bianca:(anatoka nje)
Liliana:(anaingia kuoga)
Bianca: asante Mungu nimepata
mtoto…Mungu mkubwa sana amenisikia maombi yangu
Husna: anti naomba hela nikanunue
hizo nguo maana humu ndani hakuna ngujo za mtoto hata moja
Bianca: sawa na sijui akitoka
kuoga atavaa nini (anatoa pesa na
kumkabidhi Husna)
0 Comments