SCENE 15: -
(Mchana Bianca anafika nyumbani
akiwa na daktari wake binafsi anayemtibu pindi anapokuwa anaumwa, baada ya
kusalimiana na mlinzi na wafanyakazi wake anaingia ndani na anamkuta Liliana
amekaa anaangalia runinga, Liliana sasa ni mtoto mrembo muonekano wake ule wa
uchakavu umebadilika na amekuwa ni mtoto mrembo na uso wake una nuru mpya na ya
matumaini)
Liliana:
shikamoo mama
Bianca:(anatabasamu)
safi sana...niite hivyohivyo mama…marahaba mwanangu hujambo?
Liliana:(anaachia tabasamu) sijambo
Bianca:
msalimie anko...
Liliana:
shikamoo anko…
Daktari:
marahaba
Bianca:(anatabasamu) dokta huyu ni
mwanangu…Mungu amenipa mara baada ya kumuomba kwa muda mrefu
Daktari:
hongera sana umemu adapt au inakuwaje?
Bianca:
nimemu adapt…
Daktari:
kwahiyo unamjua vizuri…
Bianca:
doctor she is my daughter and I love her, anyway nimemuona ana vidonda
vingi…mwilini mwake nataka umpe dawa ya kuvikausha na pia mpime magonjwa mengi
na kama yanatibika naomba tumtibu nataka aanze maisha upya…anaonekana amepitia
mengi…
Daktari:
unaonekana humjui vizuri sana
Bianca:
nitamjua tu…she is so beautiful na pia anaonekana ni mtulivu anafaa kuwa binti
yangu
Daktari:
umelilia mtoto sana… I hope umepata
mtoto uliyekuwa unamtaka siku zote….
Bianca:
kabisa…
Daktari:
ana umri gani?
Bianca:
saba…
Daktari:
bado mdogo kumbe
Bianca:
nataka nimpeleke shule…international school na akitaka kukaa boarding au day ni
yeye tu…
Liliana:(anaonyesha kufurahia habari ile) asante
mama nataka kusoma
Bianca:
utasoma tu mwanangu nitakusomesha katika shule nzuri mpaka wewe mwenyewe
utafurahi mwanangu umesikia ee
Liliana:
ndio mama(anatabasamu)
Daktari:(anaanza kumpima vipimo mbalimbali) wewe
ni mtoto mzuri eeh…usiogope sindano ee (anamchoma
sindano na kuchukua damu kwa ajili ya vipimo mbalimbali) good girl … (kwa Bianca) basi sawa nitakuletea majibu
baadae mimi ngoja niende…
Bianca:
sawa dokta tutawasiliana...
Daktari:
poa(anatoka)
Bianca:(kwa Liliana) umekula mama?
Liliana:
ndio nimekula…
Bianca:
umekula nini?
Liliana:
ugali...na nyama
Bianca:
unapenda mwanangu?
Liliana:
ndio…
Bianca:
safi sana mama…yaani naahidi kukutunza vizuri ila tu hujaniambia pale ulikuwa
unafanya nini maana nilikupita kama mara mbili nikakuonea huruma sana…
Liliana:
mimi ni mtoto yatima mama na baba yangu walikufa kwenye ajali, baada ya kifo
chao nikaenda kuishi na mjomba pamoja na mke na watoto wake…shangazi na mjomba
walikuwa wananitesa sana, wananifanyisha kazi ngumungumu na kunipiga, sikuenda
shule nzuri ingawa ile nyumba na mali zote ni za kwangu
Bianca:
maskini mwanangu…enhe embu endelea
Liliana:
mjomba akawa ananibaka usiku
Bianca:
Mungu wangu…jamani mbona kuna wanadamu wengine hawana huruma?
Liliana:
acha tu, nikawa sipati chakula cha kutosha…nalala stoo utasema sio nyumba yangu
Bianca:
aisee…kwahiyo ikawaje mpaka ukaishia mitaani?
Liliana:
kuna siku shangazi alinipiga sana jamani mpaka nikaona nitakufa ndo nikakimbia
na kwenda mitaani
Bianca:(anashusha pumzi) aisee…dah!!!Mungu nae
ana mitihani yake lakini usijali kabisa mama hapa umefika hautapata mateso wala
nini…Mungu alituumba ili tuhudumiane…mimi mpaka unavyoniona hivi ni mtu mzima
ila sina mtoto na wala sina mume…ila hilo la mume wala halikunipa wasiwasi,
linalonipa tabu mimi ni kutokuwa na mtoto nina mali nyingi nina mabiashara,
nina majumba lakini sina mtoto hata leo nikifa nitamuachia nani
Liliana:
ndugu zako...
Bianca:
hawapo hapa wapo nchi za nje hukona wana maisha yao na pesa zao unajua sisi
wazazi wetu walikuwa na pesa sana wakaturithisha yaani hatuna hata shida...sana
Liliana:(anatabasamu)
Bianca:
ndo hivyo kuwa na Amani hapa nitakulea kama mwanangu kabisa na wala hautakuwa
na shida yoyote sawa mama?
Liliana:
ndio mama…
Bianca:(anaita) Siwema, Husna
(Wanakuja na kusimama mbele ya
Bianca na Liliana kwa heshima)
Bianca:
Husna naomba unisafishie kile chumba cha midoli nilichokifunga miaka mingi
nikiamini ipo siku na mimi Mungu atanisikia na nitakuwa na mtoto wa kucheza
kwenye hicho chumba
Husna:
sawa anti
Bianca:
Siwema nenda ukapike mlo mzuri sana wa jioni nitakaa mezani na mwanangu na
kufurahia chakula hicho
Siwema:
sawa anti(anaondoka)
Liliana:(anakumbuka maisha yalivyokuwa akiwa na
shangazi yake na mjomba wake, jinsi alivyokuwa anakula makombo kama mbwa na
alipokuwa analala)
Bianca:(anamshtua)
Liliana:(anashtuka)
Bianca: unawaza wapi?
Liliana:(anatabasamu)
Bianca:
sipendi kukuona unawaza mwanangu…
Liliana:
sawa mama…
Bianca:
Husna alienda kukununulia nguo za kuanzia kwahiyo nimeona wala sio nzuri sana kesho
nitakupeleka dukani ukachague upendavyo sawa ee
Liliana:
sawa mama…nitafurahi
Bianca:
usijali (anachukua rimoti) mbona
huwashi TV mwanangu
Liliana:(anakumbuka alivyokuwa anajaribu kuwasha TV
alivyokuwa anapigwa)
Bianca:
washa bwana…hii ni TV yako mwanangu…
Liliana:
sawa mama, asante mama nashukuru kwa upendo nilikuwa nimekumbuka kupendwa hivi
Bianca:(anatabasamu) usijali nitakupenda kweli (kimya kidogo) unapenda katuni naweza
kuweka katuni na kuangalia na wewe hata siku nzima…
Liliana:
napenda sana marehemu mama yangu alikuwa ananiwekea sana
Bianca:
usiwakumbuke bwana mimi nipo hapa niangalie mimi
Liliana:
asante mama
Bianca:
usijali (anabadilisha chaneli) sasa katuni sijui zipo namba ngapi
Liliana:
hata sijui
Husna:
yaani anti ni namba 302
Bianca: kumbee
(Wote
wanacheka huku Bianca akiweka katuni ili waangalie pamoja, wanaonekana kufurahi
sana maana kuna vicheko vingi sana)
0 Comments