SCENE 16
(Liliana na Bianca wanashuka
kwenye gari moja matata kwa lugha nyingine gari la kifahari, Liliana amependeza
kuliko kawaida na nuru ya uso wake ni ang’avu sana, amenenepa na pia anaonekana
ana furaha mno, wanaongozana na kuingia katika duka moja la nguo la kifahari
sana)
Bianca:(anafika mapokezi) habari yako…
Dada
mapokezi: salama shikamoo
Bianca:
marahaba…natafuta nguo nzuri za mtoto wangu hapa
Dada:
okay karibu piteni mchague
(Liliana na Bianca wanapita na
kuanza kuchagua nguo)
Liliana:(anashangaa shangaa ila anajikuta
anawakumbuka wazazi wake)
Bianca:(anamuona) mama ni nini mwanangu pita
uangalie nguo unayopenda
Liliana:(anatabasamu) sawa mama…
Bianca:
sipendi kukuona unalia wala kuhuzunika…yaache ya nyuma mwanangu…achana na
mawazo mimi ni mama yako na ninakuhakikishia kuwa utaishi maisha uliyopangiwa
na Mungu…Mungu alikupangia uishi maisha mazuri na ndo maana ukazaliiwa kwa
wazazi wenye uwezo ni ndugu tu ndo walikuharibia ila Mungu hakukata tamaa na
wewe na ndo maana upo hapa na mimi …nitakulea vizuri maana Mungu hakunipa mtoto
wangu mwenyewe ila kanipa mtoto nitakutunza mwanangu mzuri sawa mama ee…
Liliana:
ndio mama…
Bianca:
ukitoka hapa twende tukale icecream au unaonaje?
Liliana:
sawa mama
(Wanaendelea kuchagua nguo)
Bianca:(anapokea simu aliyopigiwa)
(Wakati huo kuna mtu anaingia,
anaangaza ghafla anamuona Liliana, anapigwa butwaa)
Mwanamke:
Liliana??
Liliana:(anageuka na kumuangalia mwanamke aliyemuita)
shikamoo
Mwanamke:
marahaba…unanikumbuka?
Liliana:
hapana…
Mwanamke:
mimi mama Joyce nilikuwa jirani yenu
Liliana:(anajaribu kuvuta picha)
Mwanamke:
mara ya mwisho nilikuwa ni mmoja wa watu waliokuja kukuokoa wakati unapigwa na
shangazi yako
Liliana:
ah…sawa sema sikuwa naangalia
Mwanamke:
usijali…yaani umenenepa…umekuwa mzuri kweli yaani
Liliana:
asante…dada Anna hajambo?
Mwanamke:
hajambo jamani
Mwanamke:
uko wapi siku hizi mwanangu jamani mungu mkubwa kweli
Bianca:(anakuja alipo Liliana na yule mwanamke)
mama…vipi? uko sawa??(kwa mwanamke)
habari yako dada?
Mwanamke:
salama dada kwema?
Bianca:
kwema (kwa Liliana) vipi…mbona
huchagui nguo
Mwanamke:(anamuangalia Bianca kuanzia viatu alivyovaa,
mkufu wa dhahabu, pete za dhahabu, simu ya gharama) Duh!!huyu mwanamke
anaonekana ana pesa jamani
Bianca:
abeee…unaniongelesha?
Mwanamke:
hapana dada
Bianca:(anamshika mkono Liliana na kuondoka nae)
Liliana:(anamvuta Bianca nyuma)
Bianca:
nini mwanangu
Liliana:(kwa
mwanamke) huyu ni mama yangu anaitwa mama Liliana
Bianca:(anafurahi kusikia hivyo)
Mwanamke:
mama yako?????!!!!
Liliana:
ndio (kwa Bianca) mama, huyu alikuwa
jirani yetu nyumbani
Bianca:
okay…haina shida mwanangu (anamuangalia mwanamke) nashukuru kukufahamu…upite
kwetu ututembelee au unaonaje?
Mwanamke:
sawa, ni wapi?
Bianca:
uzunguni…
Mwanamke:
wow…
(Liliana na Bianca wanaendelea
kuchagua nguo)
Liliana:(anapata nguo na kujaribisha)
Mwanamke:(anabaki mdomo wazi) njia za Mungu
hazichunguziki…leo nimemuona Mungu na anapendeza jamani yaani sijamuona Liliana
nimemuona Mungu kupitia Liliana, mtoto aliyekuwa analala stoo, anakula makombo
nyumbani kwao, aliyekuwa anafagia uwanja wote peke yake leo anang’aa hivi…jina
la bwana lihimidiwe…ninakusifu wewe Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, Mungu wa
Mussa, Mungu wa Eliya ama hakika wewe ni mtu wan ne katika maisha yetu…nitaenda
kumsimulia shangazi yake Liliana matendo makuu ya mungu
Bianca:(anageuka kumuangalia yule mwanamke anagundua
kuwa bado anawaangalia sana) child, huyo mama ana shida gani kwani
Liliana:
hana shida mama
Bianca:
mbona haachi kutuangalia…asije akawa jambazi bure
Liliana:
hapana mama yeye sio jambazi ni mtu mzuri tu
Bianca:
okay
Mwanamke:(anaamua kuendelea na kazi zake zilizomleta
hapo)
Liliana:(anatabasamu kuona nguo nyingi na nzuri)
mama zote zangu
Mwanamke:(amesimama pembeni yao anatabasamu)
Bianca:(anapata wasiwasi) mwanangu huyu mama
isije ikawa katumwa na shangazi yako aje akuharibie Amani yako
Liliana:
mama usijali jamani
Bianca:
haya mwanangu…mimi nakusikiliza wewe
Mwanamke:(anafika alipo Liliana) mwanangu
ilikuwaje mpaka ukafika hapa?
Bianca:(anadakia) wewe dada kwani vipi nimekuona
muda mrefu sana unamfuatilia mwanangu tatizo nini?
Mwanamke:
sio ugomvi…mimi nimeokoka na ninampenda Yesu sina cha kukutishia mdogo wangu
kuwa na Amani
Bianca:(anatulia)
Liliana:
nilikuwa natembea mtaani ndo nikakutana na mama yangu
Mwanamke:
usisahau kumtolea Mungu sadaka…nawakaribisha kanisani siku moja mje mjumuike
nasi
Bianca:
tutakuja (anamshika mkono Liliana na
kuondoka)
Liliana:
mama, wala sio mtu mbaya,
Bianca:
we huyaoni macho yake…jamani Mungu amenipa mtoto kwa njia zake za pekee halafu
nimuachie mtu aje akuchukue ghafla tu?
Liliana:
hakuna atakayekuja kunichukua mama mimi nipo na wewe mpaka mwisho wa dunia
Bianca:(anacheka) wewe mwisho wa dunia unaujua?
Liliana:ee
(Wanacheka kisha wanatoa mizigo
yao nje na kulipa kisha wanaondoka)
Mwanamke:
nitamsimulia kila mtu matendo makuu ya Mungu…haleluya…ee mungu ulisikia kilio
cha huyu mtoto muda mrefu, umempa kicheko, umemfuta dhiki na kilio, unastahili
sifa na utukufu
(Bianca anawasha gari kisha
wanaondoka huku Liliana anaendelea kuonyesha furaha isiyo na kifani)
Liliana: mama asante sana
Bianca: usijali mwanangu
(yule mwanamke nae anamaliza
kuchagua nguo analipa kisha anaondoka zake huku akiendelea kumsifu Mungu, watu
wanamshangaa yeye wala hajali)
Mwanamke: Mungu anaishi jamani
0 Comments