SCENE 17:
(asubuhi na mapema siku moja baada ya yule
mwanamke kumuona Liliana, anafika nyumbani kwa shangazi na mjomba wa Liliana)
Mwanamke:(anagonga mlango) hodi jamani?
Anna:(anafungua mlango) karibu (kwa heshima) shikamoo
Mwanamke:
marahaba mama hujambo?
Anna:
sijambo
Mwanamke:
mama yako yuko wapi?
Anna:
ndani… (anaufungua mlango kumruhusu
kuingia ndani)
Mwanamke:(anaingia ndani anakuta sebule iko wazi
anashangaa sana) jamani samahani kwa kuingilia mambo yenu kwani nini tatizo?
mbona sebuleni hakuna kitu?
Anna:
vitu vilianza kuuzwa kimoja baada ya kingine
Mwanamke:
Kisa?
Anna:
madeni mama kwenye vicoba
Mwanamke:
aisee?
Anna:
ndio…sasa sijui utakaa wapi maana hatuna hata kiti, labda nikuletee kigoda
Mwanamke:
niletee mwanangu
Anna:(anaelekea jikoni na baada ya muda anarudi
akiwa na kigoda anampa yule mwanamke kisha yeye anakaa chini)
Mwanamke:
sasa na wewe mbona shule huendi?
Anna:(anaguna) yaani tangu Liliana ameondoka
hapa kaondoka na kila kitu hela ya kula tu hapa ni matatizo…tu
Mwanamke:
aisee? na baba yako?
Anna:
yupo tu
Mwanamke:
aisee
(Shangazi anatokea chumbani
kwake)
Shangazi:
vipi na wewe asubuhi yote hii kwa watu unataka nini?
Anna:
mama?
Mwanamke:
pole kwa matatizo
Shangazi:(kwa jazba) matatizo gani?
Mwanamke:
ya kuuza kila kitu cha ndani
Shangazi:
(anachukia sana) hayakuhusu
Anna:
mama…
Shangazi:(kwa Anna) na wewe…nini? embu toka nenda
zako huko sitaki hata kukuona
Mwanamke:
yaani una gubu kama mama mkwe, yaani Yesu anisaidie nisikujibu vibaya
Zaidi…hata hivyo sikuja kukuona nimekuja tu kutangaza ushindi
Shangazi:
wa nani na sisi unatuhusu nini huo ushindi?
Mwanamke:
unawahusu maana unamhusu Liliana
Anna:
kafanyaje binamu yangu?
Mwanamke:
kawa mzuri jamani…ana maisha mazuri
Bella:(anaingilia maongezi akitokea jikoni)
kivipi
Mwanamke:
njia za Mungu hazichunguziki…nachojua tu sasa ni mtu ambae ni tajiri kwa kweli
mrembo ana furaha
Anna:
maskini binamu yangu…
Shangazi:(anabaki ameganda tu kama sanamu)
Mwanamke:
ndo hivyo
Anna:
ama kweli malipo ni hapa hapa duniani, alikosa hata maji ya kunywa hata kama
alikuwa ndani ya nyumba ya wazazi wake leo hii sis indo tunakosa mpaka maji ya
kwendea chooni tunaomba au tunanunua maji ya mia tano duh!!
Shangazi:
anapatikana wapi?
Anna:
ili ukamuharibie Amani yake?
Shangazi:
namuulizia tu…
Mwanamke:
kwa kuibia nimempiga picha… (anawaonyesha
picha ya Liliana)
(Wote wanabaki midomo wazi)
Bella:
aisee
Anna:
huyo ndo binamu yangu Liliana
Mwanamke:(kwa Anna) halafu alikuulizia
Bella:
mimi ee’
Mwanamke:
hapana alimuulizia Anna
Anna:
maskini kumbe bado ananikumbuka, kwahiyo hamukuongea maneno mengi
Mwanamke:
hapana mama yake mkali huyo tena anaweza hata akakupiga anampenda sana Liliana
Anna:
jamani…
Mwanamke:
ndo hivyo
Bella:(anaguna) mimi nampenda binamu yangu Liliana
Mwanamke:
mara baada ya kumuona kawa mzuri?
Anna:(anacheka sana) kweli anayepanga riziki
ni Mungu…na kama amepanga kuwa utaishi vizuri utaishi vizuri tu…binamu yangu
alizaliwa katika utajiri hivi vyote vilikuwa vyao lakini mama na baba wakafanya
wanayoyajua akaishi vibaya sana na nina uhakika alitamani hata kufa, ila Mungu
akamwambia usilie mwanangu mimi ni baba wa yatima nitakuvusha
Mwanamke:
oh, haleluya jina la bwana lihimidiwe
Shangazi:(amekasirika kupita kiasi)
Anna:
sasa anaishi vizuri akiwa na mama ambae
Mwanamke:(anadakia) si mama yake ila anamlea kama
mwanae
Anna:
We Mungu
Shangazi:si
umwambie na mimi anitendee kama alivyofanya kwa huyo Liliana
Mwanamke:(anacheka sana) nimecheka si kwa
kukudharau ila nimecheka Kukuonyesha kuwa Mungu hadhihakiwi mama…tubu dhambi
zako atakusamehe yeye ni mwingi wa rehema na fadhili zake ni za milele
Shangazi:
hayo mahubiri yako peleka huko…mimi uniache na wanangu
Mwanamke:(anasikitika) kwani kuna mtu kakushika
wewe na wanao? tunakushauri tu
Shangazi:
hatutaki ushauri wako unaweza kwenda tu na wala sitaki kukuona unanitia kiwingu
tu halafu huwa sikupendi kweli yaani lione na sura lake lilivyo baya
Mwanamke:
maskini mama Anna
Shangazi:
toka hapa muone kazi kufuatilia mambo ya watu
Mwanamke:
najua unaugua moyoni kwa habari niliyokuletea ya Liliana pole…ona watoto wako
hawaendi shule kama Liliana alivyokuwa haendi shule, dunia duara unachomtendea
mwenzio siku moja itakurudia iwe nzuri au mbaya
Shangazi:
nimekuambia ondoka zako bwana usiniletee kiwingu hapa
Mwanamke:
naondoka mpenzi (anaondoka zake)
Shangazi:
huyu mwanamke mjinga sana anakuja kuleta umbea hapa yaani ndo maana watanzania
hata hatuendelei maana kila wakati badala ya kufanya yanayotuhusu tunakalia
yasiyo wahusu
Anna:
umeumia sana kusikia habari za Liliana? ulidhani atakufa? uliposema tusimtafute
ulijua kabisa kuwa lazima atakufa huku kwa njaa
Shangazi:na
wewe usiniletee habari zako hapa kwanza nina mawazo mengi mume wangu sijui
anaumwa nini jamani yaani anaumwa na nyie hamuendi shule maisha yamekuwa magumu
kitu tulichonacho hapa ni nyumba tu hatuna vitanda, masofa wala vyombo sina
biashara ya aina yoyote, maisha yamekuwa magumu…Leo hii wanangu mnauza karanga
na matunda barabarani huku mliishi maisha mazuri
Anna:
Maisha mazuri yamerudi kwa mwenyewe
0 Comments