SCENE 18: -
(Ni asubuhi ya siku nyingine siku
kadhaa zimepita tangu familia ya shangazi na mjomba wake Liliana kujua kuwa
kuhusu maisha mapya ya Liliana, Anna yupo barabarani amebeba deli la vitumbua
anauza,anapita gari moja baada ya lingine akinadi biashara yake,kuna watu
wananunua na kuna wengine hawanunui wanamuacha apite aende zake kwa upande wa
pili yake na Bella mdogo wake Anna nae anauza vitumbua na kama ilivyo dada yake
nae ananadi bidhaa yake,watu wananunua na wengine hawanunui wanamuacha aende
zake)
Bella:
baba, vitumbua
Baba
:( anapita anampuuzia)
(Upande wa Anna yeye anaendelea
kuuza vitumbua kwa kasi, wakati anaendelea kuuza vitumbua anamuona Liliana kwa
mbali)
Anna:(anashangaa) Hee!!! Liliana?
(Bianca anaendelea kuendesha gari akimpita
Anna)
Anna:
Lilly…Lily
Liliana:(anasikia ile sauti ingawa kwa mbali sana)
Anna:(anazidi kuita na Zaidi anaona akimbilie gari)
Liliana
Liliana:(anaisikia sauti kwa uhakika Zaidi) mama
kuna mtu ananiita
Bianca:
nani tena?
Liliana:
sijui ila kama sauti naijua
Bianca:(anatafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari)
embu ngoja niegeshe gari hapa…(anaegesha)
(Bianca na Liliana wanashuka
kutoka kwenye gari la kifahari na kumuangalia huyo mtu aliyekuwa anamuita kama
kweli ni anna au lah)
Anna:(analifikia gari kwa kukimbia) Liliana
Liliana:(anamshangaa binamu yake huyo alivyo) Anna?
Anna:
Liliana (anajikuta Analia sana)
Liliana:(akiwa ndani ya sare za shule mpya
anamkimbilia binamu yake huyo na kumkumbatia)
Anna:(anamkumbatia pia huku Analia sana)
Liliana:
nini kimetokea?
Bianca:(amesimama pembeni yao anawaangalia
wanavyopokeana)
Liliana:
pole usilie dada…
Anna:
acha tu…ulipoondoka tu ikawa kama vile umeondoka na kila kitu chako Liliana
Liliana:
kwanini?
Bianca:
watoto
Anna:(anamsalimia) shikamoo
Bianca:
marahaba mtoto mzuri hujambo?
Anna:
sijambo…
(Wakati huo na Bella nae anakuja
mahali walipo)
Bella:(anamshangaa Liliana) Lily???
Liliana:(bila kinyongo anamkumbatia)
Bella:
unaenda shule?
Bianca:(anaonekana ana shauku ya kujua wale ni kina
nani)
Liliana:
ndio naenda kuanza leo
Bella:
umependeza (kwa Bianca) shikamoo
Bianca:
marahaba… (kwa watoto wote) mi naona
tutoke hapa maana ni barabarani sana
Liliana:
sijakutambulisha
Bianca:
tupande gari mwanangu tutatambulishana kwenye gari
(Wanapanda kwenye gari na haraka
Bianca analiondoa gari hilo)
Bianca:
enhe!!nambieni
Liliana:
hawa ni binamu zangu, (anamshika Anna) huyu anaitwa Anna…ni dada yangu na huyu
(anamshika Bella) anaitwa Bella hawa ni watoto wa shangazi na mjomba wangu
Bianca:
wale uliokuwa unakaa nao?
Liliana:
ndio…
Bianca:
okay (anageuka nyuma kuwaangalia maana
wamekaa kwenye siti za nyuma) sasa imekuwaje wanauza vitumbua barabarani?
Anna:ni
umaskini umetuvaa ghafla…
Bianca:
poleni...kivipi sasa?
Anna:
mama ana mikopo mingi sana sehemu mbalimbali alikuwa anachukua mikopo kisha
anafanyia starehe yeye na baba sasa kila kitu kinaondoka kilichobaki ni nyumba
tu na wala sijui kama nyumba nayo itasalimika maana ana madeni mengi sana
Bianca:
pole sana…
Bella:(anamshangaa sana Liliana)
Anna:
hatuna kitu sasa tunaishi kwa kuunga unga kama hivi
Bianca:
aisee poleni sana ila kuna jambo mmejifunza?
Anna:
ndio yapo mengi mama
Bianca:vizuri..kwamba
kila tunachokifanya kiwe kibaya au kizuri kitakurudia tu, ukitenda mazuri
yatakurudia mazuri na mpaka utafurahi mwenyewe lakini ukitenda mabaya,utavuna
mabaya na mpaka utajuta kwanini uliyatenda yale…Mungu hutupa jinsi na kadiri ya
matendo yetu mema au mabaya,yeye ndo hakimu mkuu na wa haki anatoa hukumu kwa
haki na bila upendeleo utadanganya wote ila sio Mungu utatoa hongo unavyoweza
ila kwa Mungu utachemsha mwenyewe kwahiyo utavuna jinsi ulivyopanda kama umepanda mahindi
utavuna mahindi na sio mbogamboga kwahiyo tujitahidi sana kutenda yaliyo mema
Anna:ni
kweli mama yangu
Bianca:
mama yenu na baba yenu walifanya mambo wakidhani Mungu haoni, au walidhani kwa
kuwa haonekani basi haoni na wala hasikii…Mungu ni muumba dunia na kila kitu
hapa duniani ni mali yake na ni yeye anayetawala kila mtu na kila kitu yupo
kila sehemu na kwa kila mtu anaangalia kila kitu tunachofanya na ndo maana
mwisho wa siku akitoa majibu tunabaki tunashangaa
Bella:(anasikiliza kwa umakini na anajikuta
anahuzunika)
Bianca:
ila msijali…mimi na Liliana tutakuja kuwatembelea na Mungu akiruhusu
tutawasaidia kidogo tutakachokuwa nacho
Anna:
tutashukuru sana mama
Bianca:(anatoa noti za shilingi elfu kumi kama tano hivi)
hii hapa elfu hamsini itawasaidia siku mbili tatu wakati tunajiandaa kuja kuwatembelea
(anawapa pesa)
Anna:(anapokea kwa mikono miwili) asante mama
Liliana:(anawaangalia kisha anawachekea)
Bianca:
msijali…anyways naenda kumpeleka Liliana shuleni, tutaonana
Anna:
asante mama(anashuka)Bella tushuke…
Bella:(anashuka huku anataka kulia akimuangalia Liliana)
Bianca:
nyumbani wapi? embu ngoja niwape nauli (anatoa
elfu kumi na tano) haya kamsalimieni mama
Anna:
haya asante mama(wanaondoka)
Bianca:(kwa Liliana) haya mwanangu twende shule
eeh
Liliana:
sawa mama
Bianca:(analiondoa gari kuelekea shule)
(Anna na
Bella wanabaki wanaliangalia lile gari mpaka linapotokomea)
0 Comments