SCENE 19: -
(Anna na mdogo wake wanarudi
nyumbani wakionekana wana furaha sana, wanarudi na madeli yakiwa bado na
vitumbua)
Shangazi:
nyie mbona mmerudi na madeli yana vitumbua? au biashara ni mbaya leo? (amekaa barazani nay eye anauza vitumbua na
vinaonekana havijaguswa) mi mwenyewe leo watu hawajavigusa toka asubuhi
yaani bora jana walikuja kuniunga kidogo ila leo hamna kabisa
Bella:
mama leo tumemuona Liliana
Shangazi:(anashtuka) eti kawa mzuri kama yule
mmbea alivyokuwa anasema
Anna:
ndio….na zaidi anatembea kwenye gari na anaenda shule nzuri sio kama alivyokuwa
hapa kwakweli
Shangazi:
anha!!! Basi bora yake…
Bella:
yaani nikikumbuka alivyokuwa anaenda shuleni na sketi imechanika leo anaenda
shule ndani ya gari
Shangazi
:( anaguna)
Anna:
yaani Mungu amemuokoa sana jamani
Shangazi:
basi sawa…kama amefanikiwa ni vyema
Anna:(anaingia ndani kuweka deli kisha anarudi)
Shangazi:(anajisemea moyoni) imekuwaje?
Anna:(anarudi kutoka ndani)
Shangazi:
ila mbona kama mna furaha sana
Anna:
mimi nimefurahi maana nimemuona binamu yangu niliyedhani amekufa siku nyingi
leo nimemuona tena akiwa na afya nzuri na mwenye furaha
Shangazi:
sawa kama ni hivyo sawa (anaonekana ana
kinyongo sana)
Anna:
ametupa hela
Shangazi:
nani amewapa?
Anna:
huyo mama anayemlea Liliana
Shangazi:
wametoa wapi
Bella:
we mama yaani wana hela kweli yaani…lile gari tu ni la kifahari sio mchezo
Shangazi:
kumbe
Bella:
ndio hivyo mama
Anna
:( anatoa elfu kumi tano na kumpa mama
yake)
Shangazi:
yote hii? (anaichukua)hapa nikalipe
kwenye kikundi
Anna:(anampokonya) ukalipe kwenye kikundi kwanini?
huku ndani hakuna chakula na baba anaumwa na kila kitu hakipo sawa hapa...unalipaje
sasa huku kuna vitu vingi vya kufanya
Shangazi:
mimi ndo mama mwenye nyumba hii…usinijibu
Anna:
mama hali yetu ni mbaya na ni wewe ndo umesababisha maisha yetu yamekuwa hivi
yaani mama…halafu sasa hivi tunapata hela ya chakula unataka kupeleka kwenye
kikundi
Shangazi:
unataka tuendelee kudaiwa? unataka hii nyumba iende?
Anna:
sasa mama kwa hii elfu hamsini utalipa nini ili nyumba isiende?
Shangazi:
nimekuambia kuwa nitaipeleke kwenye kikundi
Bella:
mama hatuna chakula
Shangazi:
mtashindia hivyo vitumbua, na kesho tena mtaenda kujianika hapo ili huyo binamu
yenu awaone tena awape tena hela
Anna:
mama wewe upoje mama, mbona una roho ya ajabu hivyo?
Shangazi:(anamzaba kofi) pumbavu naona unataka
kunitawala wewe mtoto
Mjomba:(anaonekana amesimama mahali hapo muda mrefu
sana na ameshuhudia yote) Anna anasema ukweli (anaonekana amekonda sana) ni kweli kabisa kwanini una roho mbaya
hivyo?
Shangazi:na
wewe kelele kazi tu kula na kulala sasa hivi mpaka wanao wanakushinda kutafuta hela,
umekaa ndani kama mzoga halafu mwisho wa siku unajifanya wewe ndo kila kitu na
kibaya Zaidi unajifanya wewe ndo unajua nani ana roho nzuri na nani ana roho
mbaya
Mjomba:
mimi ni mume wako na baba wa watoto wako
Shangazi:
umeshapoteza hiyo hadhi ya kuwa baba wa watoto wangu…na mume wangu wewe ni
mwanaume suruali
Mjomba:
mama Anna...hayo ni maneno gani…unaongea tena mbele ya watoto
Anna
na Bella:(wanaangaliana)
Shangazi:
nitaongea navyotaka baba na wewe hutakuwa na chochote Zaidi ya kukaa kimya na
kufuata nachotaka mimi
Mjomba:(anacheka sana)
Shangazi:
unacheka nini? unanidharau sio
Mjomba:
ndio…nakucheka na kukudharau hela sio yako ila unaitolea matumizi zinakutosha
kweli wewe
Shangazi:
nimekuambia kuwa nyamaza na sitaki kusikia sauti yako
Mjomba:
dhambi zinakutafuna mama Anna na bado zitakutafuna sana mpaka utajuta
Shangazi:
wewe mwenyewe dhambi zinakutafuna…unaumwa magonjwa ambayo hata hayeleweki
tumekupima mpaka UKIMWI hauna sasa utakuwa ni nini?
Mjomba:
mimi natafunwa na dhambi ila sio kama wewe mwenzangu
Shangazi: nimefanyaje?
Mjomba:
watu hata hawakutaki, unauza vitumbua vinang’ong’wa na nzi hapa mpaka unaona
uviingize ndani viliwe na watoto
Shangazi:(anakasirika sana) nakuchukia wewe baba
kuliko chochote
Mjomba:
sijali…mimi nimebaki tu kufa na kulipa dhambi nilizowahi kutenda
Anna:
baba usiseme hivyo
Mjomba:
hapana mwanangu nasema ukweli kabisa na wala sina nachoficha mwanangu nimetenda
dhambi nyingi na nyingine ni mbaya mpaka nashindwa kuzitaja
Anna:
Mungu amekusamehe baba…kwakuwa umezijua dhambi zako na kuzikiri
Mjomba:
mwanangu
Shangazi:
eti Mungu kamsamehe (anacheka sana)
(Mjomba, anna na Bella
wanaangaliana)
Shangazi:
mtaangaliana sana lakini hiyo pesa ni ya kupeleka kwenye kikundi
Mjomba:
unashangaza sana mama Anna yaani hela ya watu wewe unaibeba utasema umeitafuta wewe
Shangazi:
huyo Liliana aliwahi kuwa chini yangu kwanza hii hamsini haitoshi kwa malipo ya
kumlea
Mjomba:(anacheka tena) embu niacheni mimi
Anna:(anacheka pia)
Mjomba:
eti kumlea kwanza nani amekuambia Liliana kakupa hiyo elfu hamsini kama malipo
eti ya kumlea?
Shangazi:
ndio si alikuwa anaishi nyumbani kwangu
Mjomba:(kwa mshangao kidogo) nyumbani kwako?
(Anna na bella wanacheka sana)
Shangazi:
mnanicheka
Mjomba:
unachekesha
Shangazi:(anaingia ndani kwa hasira)
Mjomba:
kwahiyo kachukua hela?
Anna:
ndio
Mjomba:
muacheni, tutapata tu nyingine
(wanabaki
wanamshangaa mama yao kwa kitendo hicho cha kuchukua pesa kwa nguvu)
Mjomba: mke wangu
anachanganyikiwa taratibu jamani
Anna: yaani acha baba
Mjomba: alivyo anaweza kumfanyia
kitu kibaya Liliana… (anabaki anasikitika)
0 Comments