SCENE 20: -
(Asubuhi na mapema sana ndo
kwanza ndo panapambazuka, Liliana na Bianca wanafika katika nyumba wanaoishi
shangazi na mjomba wake Liliana)
Liliana:(anagonga mlango)
Bianca:(amesimama anaangalia mazingira yale)
Anna:(anafungua mlango)
Liliana:
Da. Anna
Anna:
Lily?
Liliana:
ndo mimi
Bianca:(anatabasamu)
Anna:
mbona mapema?
Liliana:
mimi naenda shule…ndo nimepita kumuonyesha mama nilipokuwa naishi
Anna:(anafungua mlango) karibuni… (kwa Bianca) shikamoo
Bianca:
marahaba
Liliana:(kwa Bianca) mama...hapa ndo nilipokuwa
naishi
Anna:na
ndo nyumba yake
Liliana:
hapana nimeiacha tu
Bianca:
ana nyumba nyingine (anamuangalia Liliana
kisha anatabasamu)
Anna:
jamani karibuni
(Liliana na Bianca wanaingia
ndani)
Liliana:(anashangaa mazingira yalivyo) mbona
hakuna makochi?
Anna:
michezo ya mama
Bianca:(anashangaa) alikuwa anadaiwa au?
Anna:
ndio
Bianca:
makubwa…
Anna:
karibuni mkae tu chini
(Bianca na Liliana wanakaa)
Anna:
ngoja nikawaamshe baba na mama
Liliana:
sawa
Bianca:(anabaki anayashangaa mazingira yale)
sasa wanaishije?
Liliana:(anabaki anaguna) sijui
(Shangazi
na mjomba wanakuja wakitokea chumbani kwao)
Mjomba:
Liliana?
Liliana:
shikamoo mjomba
Shangazi:(anamshangaa Liliana jinsi alivyo) wewe
ni Liliana?
Bianca:(anatikisa kichwa)
Mjomba:
marahaba Liliana mwanangu naomba unisamehe sana…mwanangu nipo chini ya miguu
yako mama naomba unisamehe kwa kila kitu nilichowahi kukufanyia mwanangu kuna
mengi sana nimekukosea
Shangazi:(kwa kejeli) amekusalimia tu
hajakuambia uanze kujielezea wewe baba vipi?
Bianca:
sidhani kama amekosea
Shangazi:(anabenjua midomo) semeni shida yenu
Liliana:
shangazi…
Shangazi:(kwa jazba)
Bianca:
wewe dada vipi kwani? si amekuita tu…yaani una roho mbaya wewe… (kwa Liliana) naona hawataki kukusikiliza
mwanangu tuondoke
Mjomba:(kwa Bianca) hapana dada…tulia tu, bwana
usiwe na jazba mpendwa wangu…karibu sisi tunakusikiliza yeye kama
hatakusikiliza ni kimpango wake
Bianca:(anamuangalia shangazi kwa hasira sana)
yaani hata sidhani kama wanao unaishi nao vizuri
Shangzi:(anamuangalia Bianca kwa hasira sana)
Bianca:
huyu mama vipi? yaani mtoto umemlea kwa mateso pamoja ya kuwa mali zote
zilikuwa ni zake, leo kaja kukusalimia unaanza kuleta ujeuri (kwa Liliana) twende mwanangu
Anna:(kwa Bianca) jamani shangazi sisi, (anaonyeshea yeye, baba yake pamoja na Bella)
tunakusikiliza
Bianca:(anashusha pumzi) sawa
Shangazi:(amebaki amevuta mdomo)
Bianca:
kwanza tumepita kuwasidia kitu Fulani…tulipokutana na nyie siku ile tukaona
tuwasaidie kiroho safi tu lakini
Mjomba:
sawa…
Bianca:
mimi Liliana ni mwanangu sasa hivi ni zawadi kutoka kwa Mungu, maana
sikubarikiwa mtoto, ila mungu akaona anipe mtoto kwa njia zake anazozijua
mwenyewe
Mjomba:
sawa kabisa
Bianca:
Zaidi ya Mungu kunipa mtoto Mungu amenipa ndugu ambao ni nyinyi
Anna:(anatabasamu)
Bianca:
tumekaa na Liliana tumeona tu tujumuike pamoja tusaidiane
Mjomba:
sawa ndugu yangu ni wazo zuri sana
Bianca:
asante
Mjomba:
nasi tutaupokea huo msaada wako na tutaubariki sana
Bianca:
asante
(Kimya kinapita kama watu wote
kuna kitu wanatafakari)
Bianca:
sawa…kwahiyo tuanze changamoto zenu ni zipi?
Anna:
shule…na chakula, na baba anaumwa
Bianca:(kwa mjomba) unaumwa nini kaka?
Mjomba:
acha tu dada naona ni malipo yangu ya mabaya niliyowahi kufanya
Shangazi:
umeulizwa unaumwa nini sio kujielezea
Bianca:
yupo sawa kujielezea pia
Mjomba:
naumwa figo...limekufa
Bianca:
pole sana…. utapona tu…tutalishughulikia utapona tu (kwa watoto) na nyie
Anna:
shule na chakula
bianca:
mtapata… (kwa shangazi) na wewe
Mjomba
:(anadakia) madeni yeye ndo chanzo
cha matatizo yetu
Bianca:
okay nitakulipia na pia nitakuomba uje ufanye kazi katika moja ya godown yangu,
mimi ni mfanyabiashara wa mchele nina kampuni na nina wafanyakazi wananifanyia
kazi hapo
Mjomba:
asante sana mpaka kazi utatupa?
Bianca:
ndio kaka, hata wewe ukipona nitakupa kazi pia
Mjomba:
asante sana
Bianca:
msijali (huku ananyanyuka) Liliana
anachelewa shuleni tutapita tena
Mjomba:
asante sana
(Bianca na Liliana wanatoka nje
wakisindikizwa na Anna pamoja na Bella)
Anna:
haya karibuni tena
Bianca:
asante…mbaki salama jamani
Bella:
haya
(Wanaondoka)
Mjomba:(anaguna) Mungu asante sana…ubarikiwe
sana
(Shangazi anarudi kulala bila
kusema kitu, Anna na Bella nao wanarudi chumbani kwao,mjomba anabaki peke yake
sebuleni)
0 Comments