SCENE 21: -
(Jioni ya siku nyingine tena,
siku kadhaa baada ya Bianca na Liliana kwenda kuwatembelea familia ya mjomba
wake Liliana, gari kubwa la Bianca linaingia katika jumba lake safi na
kifahari)
Bianca
:( huku analiegesha pembeni ya magari
yake mengine) jamani karibuni
Anna:
wow…jamani bonge la jumba…
Liliana
:( anatabasamu) karibuni…
Bella:
Asante…yaani Lily kwenu pazuri kweli yaani
Liliana:
Asante… (kwa mjomba na shangazi yake)
karibuni
Mjomba:
Asante Sana mwanangu
Shangazi
:( anabenjua midomo na anaonekana
hajafurahi hata kidogo)
Bianca:
karibuni ndani(anawaongoza)
(Jumba ni la kifahari sio mchezo
na kila kitu kinaonekana ni cha thamani sana)
Bianca:(anaita) Siwema
Siwema:(anakuja anakimbia) abee anti…
Bianca:
nina wageni andaa chakula tutakula nao leo...wakati huo naomba uwaletee vinywaji
(kwa wageni) karibuni jamani (kwa watoto) jisikieni nyumbani
Anna
na Bella: asante
Bianca:(kwa Liliana) waonyeshe wenzio mazingira
Shangazi:(anajisemea moyoni) unajishaua umesikia
wanangu wanataka kuona nyumba yako mbaya hii(anafyonza)
Bianca:(anasikia) vipi mbona unafyonza
Shangazi:
wala…
(Watoto wanaondoka na kwenda nje)
Mjomba:
hongera kwa nyumba nzuri dada
Bianca:
asante sana kaka yangu
Siwema:(anakuja na vinywaji na kuvitenga mezani)
he!!watoto wako wapi?
Bianca:
wanacheza nje huko
Siwema:
ngoja niwaite waje wanywe juisi
Bianca:
waache tu wacheze watakunywa tu
Siwema:
sawa(anaondoka)
Mjomba:(anachukua glasi ya juisi kisha anakunywa
kidogo)
Bianca:(nae anachukua juisi na kuanza kunywa)
Mjomba:(anavuta pumzi ndefu sana) ah…dada kwa
niaba yangu na familia yangu napenda kukushukuru sana kwa yote
uliyotufanyia…hatuna cha kukulipa Zaidi ya kukushukuru sana, umelipa madeni ya
mke wangu yote, umewaandikisha wanangu shule yaani kwakweli umeturudisha
tunakushukuru sana
Bianca:
usijali kaka yangu naomba mmshukuru sana Liliana alinisimulia stori yenu kisha
akaniomba niwasaidieni kwa kidogo nilichojaaliwa
Mjomba:
sio kidogo hiki ni Zaidi ya kikubwa…tena mwezi ujao naenda india kutibiwa na
hii ni wewe ndo unawezesha na nikirudi umesema utanipa kazi kwenye moja ya
viwanda vyako
Bianca:
ndio na sio wewe na mkeo pia (anamuangalia
shangazi) kama akitaka
Mjomba:
atataka tu maana ameonja joto ya jiwe na ameona mziki wake
(Bianca na mjomba wanacheka)
Shangazi:(anachukua kinywaji na kuanza kunywa)
Bianca:
kwahiyo bwana ni hivyo tunatakiwa tuhudumiane vyema hii ni kusudi la Mungu,
ukijaaliwa kidogo basi wasaidie na wenzio Mungu atakubariki sana n asana
Mjomba:
ndo maana Mungu anakubariki sana dada…ona ulivyojenga himaya
Shangazi:
amejenga au amehongwa tu…mwanamke utawezaje kujenga hivi
Bianca:(anacheka kidogo) una mawazo madogo sana
nan do maana hata vikundi vya vicoba walikupokonya kila kitu… (anacheka tena) ila ni kweli kitu kama
nilihongwa eeh lakini hata ukihongwa kama huna akilia ya kuvilinda vitapotea
tu…kama wewe uliachiwa jumba kubwa ila si ilikuwa nusu ulipoteze? kwa lile
jumba ulilikjenga kwa nguvu zako?
Shangazi:(anamuangalia kwa hasira sana)
Bianca:
nijibu ulilijenga wewe kwa nguvu zako? si ulipewa, ndivyo hata mimi niliolewa
na mwanamume tajiri sana, alinipa kila kitu nikaishi vizuri sana ila aliniacha
na kwenda kwa mwanamke mwingine na hakutaka kuchukua hata kiwanja kimoja
alichoninunulia hapo sasa sikutaka kuzubaa nilifanya kazi kama mtumwa usiku na
mchana ili nitimize malengo yangu na ndo maana unaniona nina vitu vyangu…ndio
nilihongwa ila pia nilipambana kuvitunza
Mjomba:
safi sana dada wanawake wanatakiwa waige mfano wako wewe ni jasiri sana (anakaa kimya kidogo) kwanini mumeo
alikuacha?
Bianca:
sio yeye tu…wengi tu…
Mjomba:
kisa?
Shangazi:
mkorofi
Bianca:(anacheka kidogo) hapana kisa tu sikuwa
na uwezo wa kuzaa, sikuwazalia mtoto hata mmoja, sina mtoto ila Mungu
akanisaidia nikampata Liliana
Mjomba:
Liliana Baraka hiyo…tulimnyanyasa kwa muda mrefu sana ila badala atuchukie
akatusaidia kwenye dhiki zetu
Bianca:
hicho ndo kitu kinachonifanya nimpende Zaidi huyu mtoto
Shangazi:(anafyonza tena)
Bianca:(kwa shangazi) mbona wewe una roho ya
kichawi au mchawi wewe mama
Mjomba:
msamehe tu dada hajui alitendalo
Bianca:
mkeo akiwa na hii tabia hakuna atakayeweza kumsaidia na anatakiwa atambue kuwa
msaada anaopata ni kwa ajili ya Liliana isingekuwa Liliana nisingemsaidia
Mjomba:
asante sana, na naomba umsamehe mke wangu
Shangazi:(kwa mumewe) unajifanya mtu mzuri…huku
wewe ndo shetani kunizidi mimi
Bianca:
kivipi tena jamani
Shangazi:
aliua dada na shemeji yake…huyu ni katili kuliko hata mimi
Mjomba:
mama Anna, nimeshatubu na nimeshaadhibiwa sana tu unatakaje kwani?
Shangazi:
dunia nzima ijue kuwa wewe ni katili kuliko mimi
Mjomba:
kwahiyo kumbe ni hivyo?
Shangazi:
ndio ni hivyo
Mjomba:
mashindano kwamba nani Zaidi si ndio?
Shangazi:
ndio
Bianca:(anasikitika sana) aisee kaka unaishije
na huyu mwanamke jamani?
Mjomba:
acha tu
Bianca:
anyway, hayo mwengine tutaongea siku nyingine kwa leo tuenjoi tu
Mjomba:
kwakweli dada
Siwema:(anaandaa meza kwa ajili ya kutenga chakula)
(Giza linaingia)
Bianca:
inamaana tumeongea sana jamani?
Mjomba:
giza nalo limeingia
Bianca:
msijali kuna vyumba vya kutosha humu mtalala tu
Mjomba:
sawa dada yangu
Siwema:(anawaita watoto) njooni mnawe mikono
chakula tayari (anawageukiwa wakubwa) karibuni mezani chakula tayari
Bianca:
asante (kwa mjomba na shangazi)
karibuni chakula(anawaongoza)
(Watoto,
shangazi, mjomba pamoja na Bianca wanaelekea mezani kwa ajili ya chakula cha jioni,
wanafurahia harufu ya chakula lakini Zaidi wingi wa chakula kile, Bianca
anawakaribisha kwa moyo mkunjufu kabisa)
Bianca: jisikieni nyumbani
0 Comments