SCENE 22: -
END OF FLASHBACK
(Tunarudi mahakamani ambapo Liliana
anaendelea kuwasimulia kisa chote cha kwanini alimuua Robert ambae alikuwa baba
wa mtoto wake na hawara wa muda mrefu sana. hakimu anaamua awapumzishe watu
kwanza kabla ya kuendelea na kusikilizwa kwa kisa chote. kisa hicho kinaonekana
kuwagusa baadhi ya watu maana wanaonekana wanalia wengine wanasikitika tu)
Hakimu:
mahakama itaendelea kusikiliza mkasa huu jumatatu inayokuja hivyo nawaomba
muendelee kujiandaa (anagonga meza kisha
anaondoka)
Watu
:( wanasimama)
Hakimu
:( anaondoka)
(Watu wanatawanyika)
Lydia
:( anamuendea Liliana) Pole Kwa
maisha uliyopitia binti ila ningependa kujua kwanini ulimuua mume wangu?
Liliana:
fika jumatatu utajua tu kwanini nilimuua mumeo
Raphael:
pole Liliana kwa kila kitu kilichowahi kukutokea katika maisha yako, dah (anaonyesha kusikitika sana) umeteseka sana,
umepitia mengi sana kwenye hii dunia una umri mdogo sana ila dah umepitia mengi
sana, umebakwa sana nimesikia ulibakwa mara mbili na mjomba wako na mlinzi
mmoja
Liliana:
ndio
Raphael:
pole Sana…
Liliana:
ah Ni mapito tu ya dunia
Raphael:
Ni kweli
Lydia:
huyo mama aliyekulea alikuwa anaitwa Bianca ee
Liliana:
ndio
Lydia:
yuko wapi yeye simuoni
Liliana
:( machozi yanamtoka)
Raphael:
its okay Kama hutaki na wala hujisikii kuongelea hilo sasa hivi
Liliana:
nitamzungumzia jumatatu
Lydia:
sawa haina shida
Raphael
:( anamuangalia Liliana kivingine kabisa)
Lydia
:( anagundua kwamba mwanae anamuangalia Liliana)
wewe ndo nini?
Gabriel
:( anakuja walipo kina Liliana) pole Liliana
Kwa yote tunatamani kusikia kisa hicho Zaidi ili tujue baba aliingiaje hapo
mpaka ukamuua
Liliana:
subirini jumatatu kila kitu kitaeleweka
Raphael:
anyway…Anna yule binamu yako aliyekupigania mpaka akaleta watu wa haki za
watoto nyumbani kwenu yuko wapi?
Liliana:
alikuwepo hapa…sijui kaenda wapi
(Kuna sauti inatokea nyuma)
Sauti:
Liliana?
Liliana
:( anageuka) okay…tumemuongelea na yeye
kafika
Anna
:( binti mkubwa kabisa na ni mrembo sana)
Raphael:
okay…na Bella
Anna:
anakuja
Gabriel:
habari zenu
Bella
:( nae anafika) Liliana…
Raphael:
yaani Liliana ametusimulia stori vizuri mpaka nimejikuta nawajua hawa watu… (kwa Bella na Anna) nyie mbona mmekuwa
hivi?
(Wote wanacheka)
Anna:
unatuona sisi tu je Liliana humuoni?
Raphael:
(anacheka Sana)
Lydia
:( anaonekana kutofurahia maongezi Yale)
(Polisi magereza wanakuja na
kumchukua Liliana)
Liliana:
tutaonana jumatatu
(Anna na bella wanaonekana kuwa
na huzuni sana)
Anna
:( anawaaga) jamani sie tunaenda
Bella:
sisi tunaenda
Lydia:
haya
(Anna na Bella wanaondoka)
Raphael
:( anamuangalia Liliana kisha anajisemea
moyoni) nampenda huyu mwanamke, najua aliniulia baba yangu na najua siku ya
kwanza naonana nae nilimzingua sana ila leo nakiri kuwa nampenda jamani
Lilianaa
:( anachukulia anarudi rumande)
Raphael:
you will go through this
Lydia:
jamani…we Raphael unawaza nini mbona sikuelewi muda mrefu
Rapahel:
kivipi mama…Mimi sikuelewi wewe
Lydia:
unamuangalia Sana katika aina ambayo siielewi
Gabriel:
vyovyote vile kumbuka huyu mwanamke ni muuaji wa baba yetu na usisahau hilo
Raphael:
embu subirini kwani kumuongelesha mtu vizuri ni dhambi?
Gabriel:
hapana…sio kwamba kumuongelesha mtu vizuri dhambi…mama anaogopa kitu Fulani unavyomuangalia
ni kama mtu unaemtamani
Raphael:
oh, comeon Gabriel wewe nani kakwambia kuwa namtamani Liliana, for God’s sake
alimuua baba yetu jamani mnahisije kuwa naweza kuwa nimempenda kwanza ana mtoto
wa baba
Michael:(anakuja) hey…Liliana yuko wapi?
Raphael:
amesharudi rumande
Lydia:
huna hasira nae na wewe Michael…yaani mimi hata siwaelewi wote mnajua
Michael:
mama bado hajamaliza kutusimulia sisi na mahakama akimaliza ndo tutapima hata
mahakama itapima kwa sasa naomba tu tuwe wapole maana hatujui baada yay eye na
mama yake kuwakaribisha mjomba na shangazi yake kwenye familia nini kilitokea
Raphael:
Na baba aliingiaje hapo
Lydia:
but still amemuua mume wangu
Raphael:
hakuna anayekataa kuwa amemuua baba
Gabriel:
yeah wanasema no one is guilty until proven by court of law hivyo basi Kama
anavyosema Michael tusubiri
Lydia:
tusubiri nini? Kwani nyie hamuoni kuwa alimuua baba yenu
Gabriel:
mama yaani wewe huelewi ni hapo?
Lydia:
kwamba pamoja na kwamba alimuua baba yenu bado mnamtetea sana
Raphael:
tunamuhurumia Kwa hadithi aliyotupa hilo la kumuua baba ni lingine na hakuna
aliyekataa kuwa amemuua baba na kuchoma nyumba yetu ila tunamhurumia kwa
hadithi aliyopitia
Gabriel
:( anacheka kidogo) dogo unapambana
kumtetea huyu ndugu
Lydia
:( anaonekana kukasirika Sana)
Michael
:( anamshika mama yake) mama just chill usije ukapandwa presha bure
Gabriel:
tuondokeni tujiandae Kwa ajili ya jumatatu
Michael:
exactly
(Wanaondoka
huku kila mmoja wao kasoro mama Yao amehuzunishwa na hadithi fupi aliyoitoa Liliana)
Raphael
:( yupo kwenye gari ameshakaa ila ana
mawazo yake mwenyewe) Liliana…iam sure hili nalo litapita…nimekupenda Liliana
tangu siku ya kwanza nakuona nilikupenda ulionekana huna ukatili wowote
Gabriel
:( anajisemea moyoni huku anamuangalia
Raphael) dogo keshapenda huyu (anacheka)
(Safari inaendelea huku kila mmoja wao anawaza yake kichwani mwake)
0 Comments