SCENE 23: -
JUMATATU
(asubuhi ya siku ya jumatatu siku ambayo kesi
ya mauaji inayomkabili Liliana inaendelea kusikilizwa, watu wakiwemo familia ya
bwana Robert inaingia mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo, baada ya
watu kukaa na kutulia Liliana anakuja akiwa anasindikizwa na askari magereza,
anasimama kizimbani na hakimu anamruhusu kuendelea na simulizi ili wapate
sababu ya yeye kumuua Robert ambae alikuwa ni hawara yake, baada ya kupewa
nafasi hiyo anaendelea na simulizi hiyo)
FLASHBACK: -
(mchana mzuri kabisa, jua
linachoma sana, Bianca, Liliana, shangazi, annna, Bella pamoja na mjomba wapo
uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kwenda India kwa ajili ya matibabu ya
mjomba)
Bianca
:( anapiga simu) ah huyu nae mbona
hafiki hapa unajua tunaweza kuchelewa yaani watu bwana
(Simu inaita)
Mtu:(anapokea simu)
Bianca:
finally, jamani umepokea simu…njoo basi unajua tunakusubiri wewe tu
Mtu:
samahani boss nakuja
Bianca:
okay fanya haraka (anakata simu) ah…unajua
kaka unaenda na meneja wangu mimi nitabaki hapa kumlea mwanangu na pia
kuangalia biashara zangu
Mjomba:
haina shida dada nakushukuru sana
Shangazi:(anabenjua midomo kama hapendi)
Bianca:
usijali kabisa kaka yangu (anamuangalia shangazi)
na wifi atakuwa kazini na akiwa na akili mambo yatanyooka na Maisha yatarudi
kama hapo awali…
Mjomba:
oh, asante sana dada yangu wewe ni kama malaika uliyetumwa na Mungu mwenyewe
kuja kuniokoa mimi na familia yangu
Bianca:(anacheka kidogo) ila mbona kama vile
wifi anaonekana hapendi? yaani au hataki kufanya kazi inawezekana tu wewe ukae
nyumbani haina shida
Mjomba:
hapana dada usimjali huyu…wewe fanya unachopanga dada yangu ni kitu kizuri tu
dada…
Bianca:(anamshika Liliana) mwanangu…muage mjomba
anaenda India kutibiwa
Liliana:(anatabasamu kidogo) safari njema mjomba
wangu
Mjomba:
asante sana mwanangu
Shangazi:(anacheka kimbea) eti mwanangu…mwanao?
ungekuwa unambaka kila usiku utasema ni mkeo?
Bianca:(anakasirika sana)
Liliana:(anabaki anamshangaa sana)
Bianca:
sasa hayo yameingiaje huku sisi tunaagana ili kaka yangu hapa aende India akiwa
na Amani na furaha...
Liliana:(kimya)
Anna:
mama…
Shangazi:
kelele…na wewe
Bianca:
wewe dada vipi? mbona unakuwa kama mwendawazimu wewe?
Shangazi:
mwendawazimu ni wewe…sijui unafanya hayo kwa mume wangu ili umchukue nimeshakujua
mipango yako
Bella:
mama?
Shangazi:
nini mnadhani siwezi kusema kwasababu eti yeye ni tajiri?
Bianca:(anakasirika sana)
Shangazi:
huna mume unamendea waume za watu kama ulivyomendea mtoto wa watu
Bianca:(anashikwa hasira na machozi yanamlenga)
Liliana:(anamshika Bianca bega) mama
Shangazi:
yaani nyie mnachonyenyekea ni kwamba mnamuogopa kwa ajili ya mali zake...na sio
vinginevyo
Anna:
mama huo sio ukweli…mama yake Liliana ni mtu mzuri sana na sote tunampenda
sababu ya roho yake nzuri…wewe ndo mwenye roho mbaya mama
Shangazi:(anamzaba kofi Anna) wewe mtoto shika
adabu yako …mimi ni mama yako
Anna:
una roho mbaya sana mama
Shangazi:(anataka kumpiga kofi)
Bianca:(anamzuia) inatosha…acha ukichaa wako
wewe mwanamke
Shangazi:na
hiyo kazi yako siitaki
Bianca:
sijakulazimisha…unaweza ukaacha
Shangazi:na
wanangu sitaki uwasaidie
Bella:
mimi nataka kusaidiwa kwa kweli
Shangazi:
mimi ndo mama yako na nimesema hiyo kuwa sitaki muende shule hiyo aliyosema
huyu mwanamke
Anna:
tunaenda
Shangazi:
halafu wewe Anna wewe unajifanya wewe ndo wewe…unanijibu mimi ni mama yako
Mjomba:
mama usiyejitambua…embu acha ujinga wako wewe…na utulie tupo kwenye halaiki ya
watu hapa
Shangazi:
unadhani naogopa kwamba tupo kwa watu? siogopi na wala sijali (anapaza sauti) simpendi huyu mwanamke
mjinga mjinga
Bianca:
usiniite mimi mjinga…wewe dada hunijui
Shangazi:na
wala sitaki kukujua mwanamke uliyekuja kuharibu familia yangu
Mjomba:
familia uliiharibu mwenyewe ndugu yangu na unalijua hilo
Shangazi:
yaani hata sikutaka kuwepo hapa
Bianca:(anaita) security…kuna mtu anatusumbua
hapa
(Security wanakuja mahali hapo)
Mmoja
wa walinzi: aunt ni nani analeta fujo mahali hapa?
Bianca:(anamnyooshea kidole shangazi)
Mlinzi:
samahani... (anamshika shangazi)
naomba utoke nje hatuhitaji watu wakorofi ndani hapa
Shangazi:
nataka kumuaga mume wangu anasafiri
Mlinzi:
toka nje tafadhali
Shangazi:
sitoki sasa
Mlinzi:
unataka tutumie nguvu?
Shangazi:
jaribuni muone timbwili lake
(Walinzi wanaangaliana kisha kwa
nguvu wanamvutia nje)
Bianca:
unaleta ubabe kwenye hamna… (kwa watoto
wa mjomba) hivi mnaishi vipi huko?
Anna:(anaguna)
Meneja:(anakuja) samahani boss nimechelewa
Bianca:
sio sana...haya jiandaeni muondoke
Meneja:
haina shida mkuu
Bianca:
mambo mengine tutakuwa tunawasiliana…
Meneja:
sawa boss
Bianca:
kila kitu kipo tayari ni kufika tu na kutibiwa…malzi na chakula vyote vipo
vizuri
Meneja:
sawa boss
Mjomba:
asante sana dada Mungu akuzidishie
Bianca:
usijali ni kidogo sana hicho…nafanya hivi kwasababu ya Liliana
Mjomba:
usijali dada nakushukuru sana
Bianca:
nendeni ndege yenu imeshatangazwa
(Wanaagana
kisha mjomba na meneja wanaondoka na kuwaacha kina Bianca wanajiandaa kuondoka
kurudi nyumbani)
0 Comments