SCENE 26: -
KESHO YAKE JIONI: -
(Rafiki na binamu zake Liliana
wamekusanyika pamoja kwenye ukumbi mmoja ambao umeambatana na sehemu ya mgahawa,
watu wanapata chakula wakati huohuo kuna sherehe ya kumpongeza Liliana kwa
kufikia miaka ishirini na tatu)
Linda
:( mmoja wa rafiki za Liliana)
sikilizeni hii ni surprise party ya rafiki yetu najua jana hatukuweza kufanya
hii pati mama yake alikataa maana alikuwa amemuandalia sherehe nyumbani na
tayari tulikuwa tumeshanchanga ndo tukaona isiwe kesi tuifanye hata leo
Mabel
:( rafiki mwingine) haina shida najua
bado ana mood ya birthday… (Anacheka
kidogo) maana yeye Kwa kusherekea
Anna:
acha asherekee amepitia mambo mengi Sana katika maisha yake
Lucy
:( rafiki yake mwingine) guys… (Anachungulia anaangalia simu yake) Liliana
anapiga simu
Mabel:
pokea sasa unashangaa nini?
Lucy
:( anapokea) Lily…tupo ukumbini Kama
utaweza njoo tumekaa huku tunakunywa
Liliana:
okay nakuja (anakata simu na kuanza
kuelekea ukumbini baada ya hatua chache anafika ukumbini hapo)
(Rafiki zake wanapiga kelele surprise, na
kumpa zawadi kedekede)
Liliana:
jamani asanteni Jana mmenipa zawadi na leo mnanipa zawadi
Mabel:
hii sherehe ilikuwa ya Jana sema tu Aunt Bianca alitukatalia…
Liliana:
jamani asanteni Sana…mbarikiwe Zaidi na Zaidi jamani
(Wakati huo kuna mwanaume mtu mzima Kama mzee
hivi umri wake ni miaka 55-60 anaingia mgahawani hapo, anapoangaza angaza
anatupa macho kwa Liliana, anabaki anamuangalia sana)
Mwanaume:
wow…she is so beautiful (anang’ata midomo)
I want her...ila nitampataje huku hapa wanaonekana kuwa na sherehe na
hawaruhusu yeyote kuingia…nitakaa mpaka mwisho nipate hata namba zake
(Upande wa kina Liliana bado
wanasherekea sherehe hiyo)
Liliana:
People…guys ngoja nakuja naenda kupokea simu mama ananipigia…
Lucy:
okay
Liliana
:( anatoka nje akipitia mgahawani)
Mwanamume
:( anamfuata nyuma) samahani
Liliana
:( anamgeukia kisha anampa ishara kuwa
anaongea na simu)
Mwanaume
:( anakaa kimya huku anamuangalia Sana Liliana)
Liliana:
okay mama baadae naenjoi Sana…baadae (anakata
simu kisha anamsikiliza mwanaume huyo) yes…shikamoo?
Mwanaume:
marahaba… (Anampa mkono)
Liliana
:( anamuangalia usoni sura ya mwanaume
huyo inamrudisha miaka 16 nyuma usiku mmoja akiwa anakimbia kutoka kwa shangazi
na mjomba wake alimuomba msaada mmoja mlinzi mmoja nae akamfanyia unyama kwa
kumbaka) ha!!!
Mwanaume
:( anatabasamu) nini? Mrembo?
Liliana:
labda nakufananisha…
Mwanaume:
Na nani?
Liliana:
Na mtu mmoja aliwahi kunifanyia unyama wakati bado nipo mdogo
Mwanamume
:( anarudisha kumbukumbu nyuma na
anakumbuka tukio lile) hapana sijawahi (anakumbuka
na kujisemea moyoni) huyu ndo yule mtoto niliyevaa mpira na kumbaka…Mungu
wangu nimeumbuka leo
Liliana:
anyway, labda nimekufananisha maana wanasema kuwa binadamu ni wawili wawili
Mwanaume:
anyway…hiyo ni kweli…by the way mimi naitwa Robert
Liliana:
sawa… (Anataka kuondoka)
Robert:
mbona una haraka wewe unaitwa nani?
Liliana:
Liliana… (Anaondoka)
Robert:
subiri…
Liliana: (anasubiri)
Robert:
unaonekana una haraka Sana basi naaomba namba yako nitakutafuta
Liliana:
(anamuangalia tena usoni) ila ni wewe
yaani ni wewe kabisa…
Robert:
naomba namba yako tutazungumza
Liliana
:( anaondoka bila kusema kitu)
Robert:
nitapata tu namba zako…dah katoto kamekuwa katamu haka…Ah (anashusha pumzi) wazungu wanasema destiny…baada ya miaka mingi
kupita hatimaye nimekutana nae tena, kipindi hiki simuachii… (Anakaa na kuendelea na mambo yake)
(Upande wa Liliana anasherekea ila akili yake
inamfikiria Robert)
Liliana:
ila ni yeye kabisa sijui lakini labda kisema chake binadamu wawili wawili ila
nikimuangalia ni yeye kabisa sema tu amezeeka ila ni yeye…anyway haina shida
kwa vyovyote sitaki anaizoee (anageuka na
kuangalia alipokaa Robert)
Robert:
(anamkonyeza)
Liliana
(anafyonza) sijui
lipoje?
(Anaendelea
kusherekea sherehe aliyoandaliwa na afiki zake ila tayari akili yake
imeshavurugika)
Robert: she will be mine (Anatabasamu)
1 Comments
Naomba muendelee kunisapoti
ReplyDelete