SCENE 29: -
KESHO YAKE ASUBUHI: -
(Liliana anatoka chumbani kwake
akiwa bado amevaa nguo za kulalia anaenda moja kwa moja mpaka chumba maalumu
cha kupata chakula (dining room), huko anawakuta wafanya kazi wake wanaandaa
meza kwa ajili ya watu kupata kifungua kinywa)
Liliana:(kwa mpishi) shikamoo dada Siwema
Siwema:
marahaba…umeamkaje? (kwa mshangao kidogo)
leo mbona umechelewa kuamka?
Liliana:
ah (anacheka)jana nilichelewa kulala
Siwema:
mbona uliingia mapema chumbani kwako?
Liliana:
nilikuwa naangalia tamthilia
Siwema:(anacheka) au ulikuwa unaongea na
shemeji?
Liliana:(anacheka) lakini mna nini nyie?
Siwema:
sio vibaya ukiwa nae na wala hadhuru kuwa nae
(Wanacheka)
Bianca:(anakuja mahali hapo) za asubuhi (anavuta kiti anakaa)
Liliana:(anasimama na kwenda kumbusu mama yake
shavuni)
Bianca:(anambusu pia) good morning child
Liliana:
morning mama
Bianca:
umechelewa sana kuamka
Liliana:
iam so sorry mama
Bianca:
huna vipindi chuoni
Liliana:ni
mchana mama sasa hivi nakaa nyumbani siku nzima nipo kwa ajili yako
Bianca:
nice, na nilikuwa nimemisi sana kukaa na wewe…sasa unaonaje asubuhi hii ukaenda
kule mashineni mimi nimezeeka nimechoka sana na pia sioni vizuri
Liliana:
haina shida mama…nitaenda
Bianca:
ukirudi najua utaenda chuo ukirudi kutoka chuo tutatoka mimi na wewe tukakae
mahali tufurahie
Liliana:
ah…mama nilitaka kukuambia kuwa jioni nitakuwa na mtoko
Bianca:na
kina Anna?
Liliana:
No mama
Siwema:
ndo maana umechelewa kuamka leo
(Wanacheka)
Liliana:
jamani dada
Bianca:(anatabasamu) oh jamani nina mkwe?
Liliana:
hapana mama si nilikuambia bado ndo kwanza tunaanza kujuana
Bianca:
okay mama ila you have to be very careful my child hawa vijana siku hizi wana
mambo mengi sana
Liliana:
mama sio kijana ni mtu mzima
Bianca:
that’s good my dear
Liliana:(anacheka)
Siwema:
mlete tumuone shemeji
Liliana:(kwa Siwema) bado hatujaanza mahusiano na
wala hatujui kama tutakuwa na chochote kati yetu
Bianca:
mtakuwa tu na chochote nawaombea
Liliana:(anacheka)
Bianca:
ila mimi nina vituko natamani kumjua tu hata kama hamjaanza mahusiano nataka
kumuona mwanaume aliyefanikiwa kuubeba moyo wa mwanangu kipenzi
Liliana:
mama hata sina uhakika kama nampenda
Bianca:(anacheka) unanidanganya hata mimi shoga
yako?
Liliana:
kweli
Bianca:
mlete nataka kumuona
Liliana:
mama
Bianca:
consider me your friend usinifiche nataka kumuona kuanzia mwanzo mpaka
mwisho…kwani hajaoa?maana umeniambia ni mtu mzima
Liliana:
alikuwa na familia ila kwa bahati mbaya wote wakafariki kwneye ajali ya ndege
(Siwema na Bianca wanasikitika)
Bianca:
dah kupoteza wapendwa wake kwa wakati mmoja this must be very challenging
Liliana:
sana
Siwema:
sasa wewe ndo ujipange umpe watoto kwa mkupuo ili aone anaweza kuwa na amani
tena
Liliana:(anacheka) jamani mimi sijaanza nae
mahusiano naongea just nimempenda
Bianca:
najua ila sisi tunaongelea tu ukipata nafasi hiyo ndo ufanye yote hayo kama kunionyesha,
kumzalia watoto kwa mkupuo
Liliana:
yaani nyie wawili mnapenda umbea Loh
Siwema:(anacheka kimbea)
Bianca:
umbea kwa mwanamke ni kawaida kusutwa suna shoga yangu
Liliana:
mama
(Wanacheka)
Siwema:
sasa ukimleta nyumbani si tunaanza kuandaa harusi
Liliana:(anashangaa) walaaaaaa…
Siwema:
jamani
Bianca:(anacheka) mwenzangu wewe Siwema umetisha
kuzidi mimi
Siwema:
nimefanyaje anti
Bianca:
yaani kuja mara ya kwanza tu tayari unataka na wali (anashangaa)umenimaliza nguvu (anacheka
sana)
Liliana:
jamani nawapenda mnapenda sana kunipa raha
Bianca:na
sisi tunakupenda zaidi
Siwema:
tuletee tu huyo shemeji
Bianca:(kwa Siwema) wewe nae si amesema kuwa
atamleta au?
Siwema:
sijasikia vizuri
(Wote wanacheka)
Liliana:
jamani kuna watu wana vituko kwenye huu ulimwengu loh
Siwema:(anacheka kidogo) sasa kama sijasikia
nisiseme
Bianca:(anakunywa chai yake) enhe…kwahiyo Liliana
unaenda mashineni
Liliana:
naenda muda sio mrefu ngoja nikaoge
Bianca:
okay my child ila usisahau kumleta mkwe
Liliana:
mama
(Wanacheka)
Siwema:
sasa nani ana shauku kuzidi mwenzie
Bianca:si
wewe mpaka unataka wali kabla hata ya watu hawajuana vizuri
Siwema:na
sisi tunataka wali sio kila siku sijui kwa jirani Fulani mara nani mara nani na
mimi nataka humu ndani
Bianca:
kuwa mpole
Liliana:(ananyanyuka) ngoja mimi niondoke maana
nikiendelea kuwashangaa nitawashangaa mpaka ratiba zangu zitaingiliana (anacheka huku anaelekea chumbani kwake)
Bianca: wacha weeeeee mbona ratibaaaaa
(anacheka kimbea)
Siwema:(anacheka pia)
0 Comments