SCENE 30: -
USIKU WA SIKU ILE ILE: -
(Majira ya saa moja na nusu, hali
ya hewa ni ya kawaida kama siku zote kaubaridi kwa mbali na utulivu wa hali ya juu,
Liliana anafika katika mgahawa mmoja maarufu akiwa anaendeshwa na dereva wa
familia yake)
Dereva:
madam, tumeshafika je una lolote la kunielekeza?
Liliana:
asante sana anko kwa sasa sina la ziada nitakupigia baadae kidogo baada ya
kumaliza
Dereva:
sawa madam
Liliana:(anashuka kwenye gari, anachukua simu yake)
embu ngoja nimpigie nijue kama amefika au mimi ndo nimewahi nisije nikaonekana
nina kihelehele bure
Dereva:
naweza kwenda? Au kuna tatizo?
Liliana:
hakuna tatizo anko wewe nenda tu
Dereva:(anaondoa gari mahali hapo)
Liliana:
mbona hapokei simu huyu mtu ni ana nini?
(Simu yake inaita)
Liliana:(anapokea) hello
Sauti
nzito ya kiume: samahani mrembo sikusikia simu
Liliana:(anatabasamu) oh Robert uko wapi?
Robert:
tulipokubaliana…. kukutana…
Liliana:
mimi nipo hapo Robert
Robert:
nipe kama dakika moja nije nikuchukue malkia...mrembo kama wewe unatakiwa usije
ukaingia sehemu kama hii peke yako
Liliana:(anacheka kidogo) sawa nakusubiri Robert
(Wanakata simu)
Liliana:(anasimama kusubiri)
(Baada ya kama dakika mbili hivi Robert
anakuja mahali hapo)
Robert:
hello beautiful
Liliana:(anageuka huku anatabasamu) Hi
Robert:(anambusu shavuni) karibu… (anamshika mkono kisha anaingia nae ndani)
Liliana:
wow…this restaurant is very beautiful
Robert:(anatabasamu) not as beautiful as you are
(Wanafika kwenye meza alipokuwa
amekaa Robert)
Robert:(anampa Liliana ua) this is for your
beauty… (anavuta kiti)
Liliana:(anapokea huku anatabasamu) asante sana Robert(anakaa)oh
you are such a gentleman
Robert:(anasukuma kiti na kuhakikisha Liliana amekaa
vizuri kisha anarudi kukaa kwenye kiti chake, anachukua glasi yake iliyo na
wine anakunywa kidogo) karibu wine
Liliana:
iam so sorry I don’t drink
Robert:(anaangaza macho yake anamuona mhudumu)
dada…samahani
Mhudumu:(anamjia Robert) karibu...
Robert:
msikilize mrembo hapa
Liliana:
Malta ...only grand malta…
Robert:(anakunywa
kinywaji chake kidogo) nadhani ungejaribu wine iko poa sana
Liliana:
usijali next time
Robert:
una misimamo
Liliana:(anacheka) nimefundishwa na mama yangu
Robert:
oh my God…I must meet your mother…
Liliana:
utampenda…she is my best friend…yaani tunataniana kama tunalingana…yaani mama
yangu ni kila kitu nampenda sana
Robert:
wow
Liliana:
kweli ni muhimu umuone utampenda sana
Robert:
anaonekana ni mrembo sana kama wewe ni mrembo kiasi hiki yeye anaonekana ni
kisu…maana wanasema a fruit doesn’t fall far from its tree...yaani tunda
halianguki mbali na mti wake…
(Wanacheka)
Liliana:
kabisa…
(Kimya kidogo huku kila mmoja wao
anawaza kitu Fulani kichwani mwake)
Liliana:(anakohoa kidogo)
Robert:
I love you Liliana kweli natamani uwe wangu uwe mama wa watoto wangu wapya
nataka kuanza familia mpya niondokane na huu upweke my dear
Liliana:(anabaki amepigwa butwaa)
Robert:
unaweza ukafikiria kwanza sio lazima unijibu leo hii unaweza ukanijibu hata
baada ya siku mbili wala sina haraka mrembo
Liliana:
nitakujibu Robert…
Robert:
asante naomba uendelee kufurahia usiku wako na usifikirie chochote right now
kila kitu kifikirie baada ya hapa kwa sasa naomba niwe na wewe kimwili na
kiroho
(Wanacheka)
Liliana:
eti kimwili na kiroho
Mhudumu:(analeta kinywaji cha Liliana)
Robert:(anashika menu) wa jikoni yuko wapi?
namuomba
Mhudumu:
sawa ngoja nikamuite(anaondoka)
Robert:(kwa Liliana) cheers (ananyanyua glasi)
Liliana
:(ananyanyua kinywaji chake) cheers
(Wanagonga glasi)
Robert:
iam so happy today…
Liliana:
kwanini?
Robert:
napenda kampani yako na tangu siku ya kwanza nimekuona nilikuwa natamani nipate
wasaa kama huu ila nikakosa sasa leo nimepata nimefarijika sana
Liliana:
usijali…
Robert:
nitafurahi sana siku nikikupata
Liliana:(anacheka kwa aibu)
Robert:(anatabasamu)
Mpishi:(anakuja)
karibuni
(Wanaagiza chakula kisha mpishi
anaondoka kurudi jikoni baada ya kuwasikiliza)
Robert:
naomba nikualike kwenye sherehe ya kufungua tawi la moja ya kampuni zangu siku
ya jumamosi kama utakuwa free
Liliana:
oh, asante sana nitakuwa free jumamosi mara nyingi nakuwa sina kazi nyingi
Robert:
karibu sana
Liliana:
asante sana nitakuja…tutaongea tu ni saa ngapi
Robert:
nitakuambia kwenye simu ratiba kamili
Liliana:
okay haina shida
Robert:
:(anatabasamu) wewe ni mrembo sana
Liliana:
hata wewe ni mtanashati sana
(Wanatabasamu
kila mtu anaonekana kuvutiwa na mwenzie)
0 Comments