SCENE 31: -
JUMAMOSI: -
SIKU YA SHEREHE: -
(majira ya saa 12 jioni, Liliana
anahangaika na maandalizi ya kwenda kwenye sherehe aliyoalikwa na Robert)
Bianca:
mbona upo juu juu unaogopa kuchelewa au unaogopa kukosa usafiri honey unajua
kabisa una dereva wako na atakupeleka wakati wowote
Liliana:(anamalizia kuvaa) mama tatizo ni kwamba
hata sijui ukumbi ulipo…na hata hivyo amesema kuwa atatuma dereva aje anichukue
Siwema:(anakuja) dear kuna gari nje linakusubiri
Liliana:
are you serious?
Siwema:
ndo nakwambia… (anaongea kwa kunong’ona)
gari ni la ki fahari
Bianca:
wache weeee (anatoka kwenda kulichungulia)
Oh My God…mwanangu mzuri na hawezi kukosa mwanaume mwenye hadhi zake
Liliana:(anakuja akiwa amependeza sana)
Siwema
na Bianca: oh My God…
Bianca:
mwanangu wewe ni chombo
Siwema:
hakika
Bianca:(anataka kulia)
Siwema:(kwa Bianca) sasa usianze kutaka kulia
hapa kama wale wa mama wa kihindi wanaonyeshwa kwenye zee world
Bianca:
hata siwaigi ila nimefurahi tu mwanangu kakua mkubwa na sasa ana maisha yake
nakuombe kheri mwanangu
Liliana:(anatabasamu) asante mama
Bianca:
nakupenda mwanangu enjoy your party
Liliana:(anamkumbatia)
Bianca:
nisije nikakuharibia gauni lako mama…ni zuri
Siwema:
amepewa zawadi na shemeji
Liliana:
exactly
Bianca:
wow…nataka kumuona mkwe wangu jamani
Liliana:
utamuona soon
(Honi ya gari inapigwa)
Bianca:
shoga nenda usije ukaonekana huna adabu bure mwanangu
Liliana:(anatoka nje lilipo gari)
(Bianca na siwema wanamfuata
nyuma na akumsindikiza kwa macho)
Bianca:
wow gari zuri ee
Siwema:
sana
Bianca:
mtoto wetu ana amani sana ona anavyotabasamu…
Siwema:
kabisa Mungu ni mwaminifu…nakumbuka kalikuja kakiwa na umri wa miaka saba (7)
kadogo hakana hata furaha, wala afya…
Bianca:
uzuri wa moyo wake ni wa kusamehe, fikiria alimsamehe shangazi na mjomba
wake…pamoja na mateso yale yote
Siwema:
ndo maana Mungu amembariki sana
Bianca:
namuombea Baraka zaidi
(Gari lililombeba Liliana
linaondoka mahali hapo)
Bianca:
Mungu amlinde mwanangu
Siwema:
amina
Bianca:
twende ndani na sisi kwa umbea
(Wanacheka huku wanaingia ndani)
Liliana:(amekaa kwenye gari kama malkia, anachezea
simu mara ajipige picha mara ajiangalie nywele mara viatu yaani ilimradi tu
afurahi)
(Baada ya mwendo wa dakika 30
njiani hatimaye wanafika kwenye ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya sherehe ya
ufunguzi wa tawi la biashara nyingine ya Robert, Watu wamependeza sana na kuna
shamrashamra za sherehe kila mgeni mualikwa ameshika kinywaji chake mkononi)
Liliana:(huku anashuka kutoka kwenye gari) kuna
watu wengi sana
Dereva:
yaani watu wengi sana ila usijali…nitakusindikiza mpaka kwenye meza
iliyoandaliwa kwa ajili yako na meza hiyo ndo ya boss pia...
Liliana:
oh My God asante sana kaka
(Dereva anamuongoza Liliana mpaka
kwenye meza iliyokuwa tayari kwa ajili yake)
Dereva:
hapa sasa ndo kwenye meza yako
Liliana:(anakaa) asante sana
Dereva:(anaondoka)
Robert:(anakuja huku mikononi mwake amebeba glasi
mbili za vinywaji moja ni juisi na nyingine ni pombe kali) mrembo
Liliana:(anageuka) oh (anatabasamu)
Robert:
karibu… (anamuangalia juu mpaka chini)
umependeza sana mrembo (anampa kinywaji)
asante sana kwa kukubali wito wangu
Liliana:
asante pia kwa mwaliko (anapokea kinywaji)
hata wewe umependeza
Robert:(anaachia tabasamu) asante mrembo
Liliana:
kuna watu wengi sana leo
Robert:
mimi ni mfanyabiashara mkubwa sana nadhani hata mama yako atakuwa ananijua
Liliana:
itakuwa anakufahamu…maana hata yeye ni mfanyabiashara
Robert:ni
muhimu nikutane nae huwezi jua naweza kupata business partner
Liliana:
kabisa
(Kuna mtu anaongea stejini kunakuwa na
utulivu)
Mtu:
naomba nimkaribishe mkurugenzi mtendaji Bw. Robert
(Watu akiwemo Liliana wanapiga
makofi)
Robert:(anaenda mbele na kufungua tawi rasmi)
(Watu wanapiga makofi)
Robert:(anarudi kukaa kwenye meza alipokaa Liliana)
Liliana:
hongera kwa kufungua tawi…
Robert:
asante mrembo...ningependa uje ufanye kazi na mimi
Liliana:
what?
Robert:
yes…njoo please I will be waiting au nitaonana na mama yako nimwambie…
Liliana:
bado nasoma Robert
Robert:
haijalishi…please naomba
Liliana:
okay ngoja niongee na mama nitakujulisha
Robert:
okay…
(Watu mbalimbali wanamfuata Robert
kuna wengine wanaomba apige picha nao, wengine wanampongeza kwa kazi nzuri na
mafanikio ya biashara yake)
Liliana:(anamuangalia huku anajisemea moyoni) ni
mtu muhimu kumbe ona watu walivyo wengi…anafaa kuwa mwanaume wangu…(anatabasamu)
Robert:(anaendelea kuonyesha ukaribu kwa watu)
(Sherehe
inaendelea na kila mmoja wao anaonekana kutosheka na kufurahia hafla hiyo
ndogo)
Liliana:(anamuangalia Robert huku anatabasamu) he is the one!!!
0 Comments