I KILLED MY LOVER 32

 


SCENE 32: -

(Kesho yake asubuhi Bianca anaingia chumbani kwa Liliana ambae anaonekana bado amelala na wala hana dalili za kuamka kwa wakati ule)

Bianca:(anafunua mapazia)

(Mwanga unaingia ndani)

Liliana:(kwa sauti ya usingizi) jamani da Siwema

Bianca: sio Siwema ni mama

Liliana:(anakurupuka) shikamoo mama

Bianca: marahaba…hujambo

Liliana:(anapiga miayo) sijambo

Bianca: umechoka sana ee

Liliana: kiasi mama(anatabasamu)

Bianca: nambie mwanangu za kwenye sherehe?

Liliana: nzuri… (ananyanyuka kutoka kitandani na kwenda bafuni anachukua mswaki anasimama mlangoni ili aendelee kuongea na mama yake)

Bianca: jana ulirudi saa ngapi?

Liliana: saa saba usiku

Bianca:(anashangaa) mbona hukuniamsha

Liliana: mama jamani ningeanzia wapi? nilikuwa naona nitakusumbua hata hivyo nilikuwa nina usingizi

Bianca: enhe ilikuwaje

Liliana:(anapiga mswaki)

Bianca: wewe nae niambie

Liliana: tulikula, tulikunywa, tukacheza maisha yakawa mazuri kweli kweli

Bianca: wow…enhe mkwe anasemaje kuhusu kuja huku?

Liliana: atakuja mwisho wa mwezi huu…hata hivyo anataka kukutana na wewe…pia for business purpose

Bianca: unadhani mimi nina tatizo basi? (ananyanyua mabega) yeye aje tu

Liliana:(anacheka)

Bianca: lakini una amani mwanangu?

Liliana: nina amani mama…mimi na yeye tumeanza mahusiano yetu

Bianca: kweli?

Liliana: yes, mama na ninajua mahusiano yetu yatadumu…(anatabasamu)jana amenionyesha kuwa mimi ni wa muhimu nilikaa meza moja na yeye na unajua yeye ndo alikuwa mkurugenzi mtendaji…yaani acha tu

Bianca: wow, nice child

Liliana :( anacheka)

Bianca: na mimi kwa umbea nimeshamwambia mjomba wako

Liliana: sio mbaya mama

Bianca: I hope hujachukia

Liliana: wala maana hata Kama tungeficha vipi lazima angejua tu

Bianca :( anatabasamu)

Liliana :( anacheka) mama bwana

Bianca: nimefanyaje?

Liliana: yaani wewe mzungu kweli

Bianca:(anaguna kidogo) unajua kwanza umeshakuwa kale kamtindo kakunyima ndo matokeo yake unaenda kuboronga huko tunabaki tunatoa macho mimi nakuruhusu huku nakufundisha kama haupo tayari kuwa mama sasa hivi kuwa makini…sikufundishi umalaya ila tu nahisi wewe ni msichana mkubwa na ni mwanamke kamili nikisema nikunyime kuwa na mahusiano mimi itanisaidia nini mimi? Matokeo yake utaenda huko ufanye bila kuwa na kinga yakakukuta nikaumbuka na ukali wangu…ila tu kuwa makini mwanangu

Liliana:ni kweli mama…

Bianca: halafu wewe sio mtoto miaka yote mwanangu tangu nimekupata nimekuwa nikikufundisha kuhusu haya si unakumbuka

Liliana: ndio mama

Bianca: kwahiyo unajua…sasa kama umepata tena mtu mzima I feel iko safe zaidi maana hautapata mpasuko wa moyo

Liliana: yes mama

Bianca: umeshafika chuo najua akili yako ni pana sana

Liliana: kabisa mama

Bianca: mkwe anaitwa nani?

Liliana: Robert

Bianca: I feel he is good for you

Liliana :( ananawa mdomo kisha anamuendea mama yake) asante mama... (Anamkumbatia na kumbusu)

Bianca: okay ngoja tujiandae kwa mapokezi ya kumpokea kwenye familia tunataka kumuona ili tujue mtu uliyenae

(Wanakumbatiana kwa mapenzi ya mama na mtoto)

Post a Comment

0 Comments