I KILLED MY LOVER 33

 


SCENE 33: -

BAADA YA WIKI MBILI: -

(Majira ya saa moja usiku wanawake, Bianca, Siwema, mfanya usafi, Liliana, Anna na Bella, wapo jikoni wanamalizia maandalizi kwa ajili ya kumpokea Robert kwenye familia)

Bella :( Kwa Liliana) Lione linavyotuweka roho juu juu utasema tunapokea mahari Leo

Bianca: si dalili jamani

(Wanacheka)

Mjomba :( amekaa sebuleni peke yake) kwahiyo Mimi mlinzi huku sebuleni

Bianca: ukitaka njoo upike na kifua chako

(Wanacheka)

Anna: anatujaribu ee

Siwema: mi nishaanza kutenga

Bianca: nyie huyu ana usongo… khaaaa

Liliana: jamani si ndo maana kamili ya kuwa punctual hataki mambo yafanyike deadline

(Wanacheka)

Bianca: aende zake huko

Siwema: jamani Mimi Nina raha…leo namuona shemeji jamani

(Wanacheka)

Mjomba :( anakuja walipo)

Bianca :( anatania) maskini njaa imembana mpaka kaona aje atusimamie

Mjomba: namuona mlinzi anafungua geti halafu kuna gari Fulani linaingia sijui ni la mgambo

(Wanakurupuka na kuanza kufanya kazi kwa haraka Zaidi)

Bianca: gari la mgambo wapi huku ni gari la mkwe

Siwema: Yallah!!!!Yaani Shem kaja kabla ya sisi kumaliza kitu chochote jamani huko kulikuwa sio kujivuta ni kuhangaisha

Liliana :( anatoka na kwenda nje)

Robert :( Kama kawaida yake kupendeza anashuka kutoka kwenye gari lake la kifahari)

Liliana :( anamuona) wow...Umependeza

Robert :( anaachia tabasamu la kuvutia Zaidi) Asante

Liliana: karibu nyumbani nadhani huwa unakuja ila mara nyingi unaishia nje

Robert: yes

Liliana: karibu ndani Leo baby

Robert :( anatabasamu) Asante mama (anamkumbatia)

Liliana :( anamkumbatia pia)

(Bianca, Anna, Bella na Siwema wamesimama dirishani wanachungulia)

Bianca: aaaah mkwe mzuri bwana

Siwema: ndo maana Liliana wetu kanasa hapo

Mjomba: kuna majitu ni mambea

Bianca: eeeh eeh wewe umbea kwa mwanamke ni kawaida kusutwa suna babuuuuuu

Mjomba: wache weeeeee…

(Liliana na Robert wanaingia ndani walipo wengine)

Bianca: karibu Sana baba

Robert: oh, Asante Sana mama (anamshika mkono) na wewe ni…

Bianca :( anampa mkono) Bianca…mama Liliana

Robert: wow…nimeona tunda halianguki mbali na mti wake

Bianca :( anacheka) kwanini?

Robert: you are as beautiful as Liliana

(Wanacheka)

Liliana :( anaenda Kwa mjomba) Na huyu ni mjomba wangu…

Robert :( anampa mkono)

Mjomba :( anamkumbatia) karibu Sana mkwe

Robert: Asante Sana mjomba

(Wanacheka)

Liliana :( Kwa Anna na Bella) hawa ni my bestfriends, my cousins and my sisters

Robert: wow… (Anawapa mikono)

Anna na Bella :( wanamsalimia)

Robert: marahaba

Liliana:(kwa Siwema na wafanyakazi wengine) na hawa ni marafiki zangu na dada zangu wa nguvu

Robert: oh (anawasalimia)

Siwema: Karibu shemeji yangu

Robert: Asante Sana

Bianca :( anaketi kwenye sofa kubwa) tafadhali karibu mketi jamani msisimame

(Wanakaa kila mmoja kwenye Sofa Lake)

Bianca :( Kwa Liliana) come child come sit with me

Liliana :( anakaa pembeni ya mama yake)

Bianca :( Kwa Siwema) njoo mara moja dear

Siwema :( anamuendea Bianca)

Bianca :( ananong’ona) andaa supu watu wakute wanaburudisha midomo Yao

Siwema: sawa aunt (anaondoka)

Bianca :( Kwa Robert) jisikie nyumbani baba…

Robert: Asante mama…Asante kwa mwaliko huu kiukweli nimefurahi sana kuwepo hapa jioni ya leo

Bianca :( anatabasamu) tumefurahi kwamba umekubali wito wetu…tumefurahi Sana kuwa na wewe jioni ya leo

(Siwema na wafanyakazi wengine wanaleta supu kwenye trei lenye matairi, wanaendesha mpaka walipo watu, watu wote waliopo sebuleni wanachukua bakuli la supu kwa zamu)

Robert :( anaonja) wow…wonderful soup

Bianca :( anatabasamu) mambo ya mwanangu Liliana

Robert :( anacheka) Safi Sana

Liliana :( anacheka Kwa aibu)

Robert :( anamuangalia Liliana kisha anatabasamu)

(Watu wanaonekana kufurahia maongezi na ugeni ule, wanaongea mambo mengi sana yahusuyo maisha. Kila mmoja kwenye familia anaonekana kumpokea vizuri Robert mpenzi wa Liliana)

Siwema :( anatoa vyombo vya supu)

Robert: wow nimeenjoi supu

Bianca: eti eeh…. (Anamuangalia siwema) chakula tayari?

Siwema: ndio aunt

Bianca: karibuni mezani jamani (anaongoza njia)

(Watu wanamfuata nyuma, wanapofika mezani wanakaa kwenye viti, kila mmoja na sahani yake, wanapakua chakula kwa zamu na kila kitu kinaonekana kuwa sawa kati ya familia hiyo na mgeni wao, wanakula huku wanaendelea na mazungumzo. wanakunywa vinywaji mbalimbali na kila mmoja wao amependeza sana ama hakika walikuwa wamejipanga kwa ugeni ule)

Bianca: nimeenjoi jamani…nyinyi je

Wote: tumeenjoi pia (wanagonga glasi ishara ya kufurahia maisha)

Post a Comment

0 Comments