SCENE 34: -
(Asubuhi ya kesho yake siku moja
baada ya Liliana kumtambulisha mpenzi wake kwa familia yake, Robert anafika
nyumbani kwa kina Liliana akiwa ni mtu mwenye furaha sana)
Robert
:( anapiga honi)
Mlinzi
:( anatoka) oh shemeji…unamtaka Liliana
Robert:
eeh muite siingii ndani…
Mlinzi:
ingia bwana yaani kila mtu anakupenda jamani humu ndani
Robert:
kuna kitu nataka kumwambia Liliana nampigia simu yake simpati
Liliana
:( anatoka nje) oh Rob?
Robert:
Yes Lily…
Liliana:
njoo ndani bwana
Robert:
No kuna sehemu naenda na ninachelewa sana njoo nikwambie nachotaka kukuambia
halafu mimi naondoka
Liliana
:( anamuendea) nambie baby (anambusu)
Robert
:( anambusu pia)
Liliana
:( anaingia ndani ya gari)
Robert:
I missed you baby (anatabasamu)
Liliana
:( anatabasamu) Asante and I missed
you too my love
Robert:
nilikupenda Zaidi siku Jana
Liliana:
kwanini?
Robert: ukiona mwanamke anatoka katika familia
yenye watu wenye upendo kiasi hicho ujue mwanamke huyo ni mwanamke mzuri sana
Liliana:
kivipi?
Robert:
kwamba ni wife material
(Wanacheka)
Liliana:
Asante sana dear kiukweli ndugu zangu walifurahi sana
Robert:
nataka twende Zanzibar
Liliana:
kuna nini tena baby?
Robert:
kutalii tu
Liliana:
oh, tunaenda lini?
Robert:
wikiendi hii...
Liliana:
okay baby nitamwambia mama kuhusu Hilo halafu nitakupa jibu
Robert:
sawa mpenzi wangu…halafu umependeza halafu unanukia Sana
Liliana:
oh, baby Asante Sana na wewe umependeza na ofcourse unanukia sana
Robert
:( anacheka kidogo) so tunaenda wote
au?
Liliana:
wapi?
Robert:
ofisini kwangu
Liliana:
No baby
Robert:
kwanini?
Liliana:
Nina kipindi chuoni muda sio mrefu nasubiri gari yangu itoke gereji niondoke
Robert:
baby…kwanini nisikupeleke chuo?
Liliana:
hapana sitaki kukuchelewesha mpenzi wangu…wewe nenda tu nikifika nitakutaarifu
Robert:
okay baby…I love you
Liliana:
I love you too my love
(Wanakumbatiana)
Liliana
:( anashuka kwenye gari)
Robert:
tutaonana baadae baby… (Anatabasamu)
mama mzungu huyo
Liliana:
si nilikuambia (anacheka pia)
Robert:
nimempenda bure
Liliana
:( anacheka) nitamuambia kuwa
umempenda (anacheka Sana)
Robert:
tunda halianguki mbali na mti wake
Liliana:
una maana gani?
Robert:
wewe na mama yako ni warembo sana
Liliana
:( anacheka Sana)
Robert:
of course, Na binamu zako wote warembo Sana
Liliana:
yes, my love
Robert
:( anacheka) haya kajiandae uende
chuo
Liliana:
sawa baby nikirudi nitamwambia mama
Robert:
mwambie mama Nampa hi yeye ni mzungu sana yaani ana tamaduni za kizungu sana
Liliana:
hiyo kuniruhusu kuwa kwenye mahusiano huku nasoma?
Robert:
Sana
Liliana:
kawaida tu mbona
Robert
:( anacheka kisha anawasha gari na
kuondoka zake)
Liliana:(anabaki anatabasamu) nafurahia maisha
yangu kwakweli… (anavuta pumzi)
imekuwaje mpaka maisha yangu yaebadilika kiasi hicho…sasa nina ndugu
wananipenda…nina maisha (Anaangalia jumba
lile la kifahari) nina mama na Zaidi nina mwanaume anayenipenda kwa dhati
nina kila kitu nilichokuwa nawazia…nikurudishie nini bwana
Mlinzi
:( anamuona) unaongea peke yako dada Liliana
Liliana
:( anacheka) acha tu niongee peke
yangu Mungu aliyonipa ni Zaidi ya kila kitu
Mlinzi:
mshukuru sasa
Liliana:
namshukuru Sana tu
Mlinzi:
una bahati Sana…anti anakupenda Sana
Liliana:
hata Mimi nampenda Sana mama yangu hata mpenzi wangu amempenda Sana mama yangu
Mlinzi
:( anatabasamu) shemeji ni mkubwa ila
mnaendana sana
Liliana
:( anacheka Sana) jamani
Mlinzi:
kweli tena kwani kina Bella hawajakuambia?
Liliana:
huwa wananiambia Sana tu
Mlinzi:
unaona sasa inamaana ni kweli
Liliana
:( anacheka) wewe bwana naomba
uniambie Kama dereva amerudi nachelewa (anaangalia
saa yake ya mkononi) nachelewa Sana
Dereva
:( anafika)
Mlinzi
:( anaangalia anapotokea dereva) na yeye
hatajwi
(Wanacheka)
Mlinzi:
yaani
Liliana
:( Kwa dereva) umechelewa Sana kaka
Dereva:
nisamehe Sana
Liliana:
jamani usijali kaka yangu
Dereva:
tunakupenda Sana yaani wewe ni mpenda watu sana
Liliana:
jamani…nawapenda pia
Dereva:
haya twende
(Wanapanda gari na kuondoka zao)
Mlinzi: baadae jamani
0 Comments