SCENE 35: -
USIKU WA SIKU HIYOHIYO: -
(Usiku wa kawaida hali ya hewa ni
ya kawaida sana, Bianca yupo chumbani kwake amekaa kitandani anasoma kitabu
Fulani kama kawaida yake kabla ya kulala)
Bianca
:( anavua miwani) ah nimechoka kweli
Leo (anajinyoosha)
Liliana
:( anagonga mlango) mama
Bianca:
karibu mwanangu…
Liliana
:( anafungua mlango)
Bianca:
oh, my child…Leo hatujaonana kabisa
Liliana:
kabisa mama...Tumekuwa tukipishana Sana
Bianca:
karibu ukae mama
Liliana:
Asante mama (anakaa pembeni yake)
Bianca:
nambie…unaonekana umechoka Sana
Liliana:
nimechoka ndio (anamuangalia usoni)
wewe ndo umechoka Zaidi mama
Bianca:
Ni kweli Leo nimeshinda kiwandani yaani nimechoka Sana
Liliana:
pole Sana mama yangu ni muda wako muafaka sasa wa kupumzika...Mjomba si yupo?
Bianca:
Ni kweli yupo ila sipendi kumchosha na yeye ana stress zake
Liliana:
stress za kukosa mke au?
Bianca
:( anacheka) sijui mwenyewe
Liliana:
by the way mama…kwanini ulikataa mjomba akuoe
Bianca
:( anacheka) wewe ni nani?
Liliana:
mwanao
Bianca:
Na yeye Ni?
Liliana:
mjomba wangu…
Bianca:
sasa nitaolewa vipi na kaka yangu
Liliana:
jamani mama (anacheka)
Bianca:
ndo hivyo…siwezi kuolewa na kaka yangu
Liliana:
wacha weeee ila tungecheza kwenye harusi yenu...Fikiria basi
Bianca:
wewe mtoto mjomba wako amekutuma nini?
Liliana:
wala Mimi Nina shida zangu nyingine tu
Bianca:
sawa nambie shida yako maana ushaanza kuniogopesha...Una shida gani?
Liliana
:( anacheka kidogo) nambie
Bianca:
wewe ndo uniambie shida yako mwanangu una shida gani? Au una mimba?
Liliana:
jamani mama
Bianca:
kwani vibaya? Nataka mjukuu nikae nae siku nzima namshika mashavu namchezea
chezea
Liliana:
kweli mama unataka mjukuu?
Bianca:
kabisa
Liliana: nitakupatia mjukuu mama
Bianca:
Asante kwa kunipa ahadi nzuri kama hiyo
Liliana
:( anacheka)
Bianca:
enhe nambie sasa
Liliana:
kuna mtoko wa kwenda Zanzibar wikiendi hii…naweza kwenda mama?
Bianca:
oh, my child uko huru kufanya yanayofurahisha nafsi yako
Liliana:(anafurahi) asante mama
Bianca:
anything for you child
Liliana:
tunaondoka ijumaa jioni tunarudi jumapili jioni
Bianca:
okay child…haina shida Sana my love
Liliana:
nakupenda mama
Bianca:
nami nakupenda mwanangu
Liliana
:( anamkumbatia) acha nikalale…usiku
mwema mama
Bianca:
usiku mwema mama… (Anamkumbatia pia)
Liliana:
haya lala sasa
Bianca:(anacheka)
Liliana:(anaondoka)
Bianca:(anabaki anatabasamu anazima taa kisha
anajifunika shuka na kulala)
Liliana: oh, my mama…Mungu
amlinde mama yangu...aje ale matunda yangu (anapiga
hatua kuelekea chumbani kwake) yupo kama mama yangu mzazi nakumbuka mama
yangu alikuwa kama mama yangu Bianca...ni kama Mungu amemrudisha mama yangu
kupitia Bianca…asante Mungu kwa nafasi hii ya kuwa na mama (anaingia chumbani kwake)
0 Comments