SCENE 36: -
SAFARI YA KWENDA ZANZIBAR: -
(Liliana na Robert wanafika
Zanzibar kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa wiki wanafika katika hoteli ya
kifahari ya Golden Tulip Zanzibar Resort)
Robert:
(anafika mapokezi) hello habari
Dada:
salama shikamoo, karibu sana
Robert:
asante…tulifanya booking online
Dada:
jina
Robert:
Robert Masaga
Dada:
(anaangalia) sawa nimeona (Anampa ufunguo) karibuni sana na enjoy
your stay
Robert:
thank you so much
Dada:
(anatabasamu)
Robert:
(anamgeukia Liliana) twende baby
Dada:
(anawaangalia) jamani huyo si baba na
mwana? Au baby amemaanisha mtoto na sio mpenzi…eeh mdomo koma (anaendelea na kazi zake)
Robert:
(anavuta begi huku anaangalia namba ya vyumba)
najua umechoka baby…tutapumzika muda sio mrefu
Liliana:
wala hata usijali nipo sawa
Robert:
najua umechoka
Liliana:
safari ilikuwa ya kawaida mbona hatujalala njiani tumekuja kwa ndege na pia
nataka kufanya kitu kimoja tuweke mizigo kisha tukatalii nasikia Zanzibar pako
vizuri sana kwa upande wa utalii
Robert:
sana (anapata chumba anafungua) njoo
tuingie hapa mara moja halafu tutatoka
Liliana:
sawa baby...
Robert:
call me daddy
Liliana:
Daddy
(wanacheka)
Robert:
(anaweka mizigo chumbani) basi sawa
tunaweza kutoka sasa
Liliana:
tutaenda wapi labda unapajua
Robert:
hapana hata sipajui
Liliana:
tutaulizia tu
Robert:
sawa haina shida
Liliana:
oh, I love Zanzibar
Robert:
and I love you my love
Liliana:
and I love you daddy…lakini Daddy tunafunga ndoa lini?
Robert:
soon baby jiandae tu kuwa bibi harusi my love
Liliana:
(anafurahi)
Robert:
najua unatamani sana kuwa bibi harusi
Liliana:
hakika tena wa kwako baby jamani ninavyokupenda
Robert:
najua baby… (anaangaza angaza) okay
tuulize watu sasa tunaanzia wapi?
Liliana:
kwani baby tunakaa huku kwa siku ngapi?
Robert:
siku moja tu najua unatakiwa uwe chuoni lakini pia na mimi natakiwa niwahi
kazini
Liliana:
lakini daddy hiyo ni mbaya jamani
Robert:
kwanini?
Liliana:
nataka nikae na wewe
Robert:
kusoma kwanza
Liliana:
ah daddy
Robert:
ndo hivyo
Liliana:
ila una roho nzuri sana na unijali sana asante baby kwa upendo wako
(Wanabusiana)
Robert:
usijali nitakutunza milele malkia wangu
Liliana:
na mimi nitakupenda milele I can’t wait for our wedding to happen
Robert:
oh, you little mama
Liliana:
napenda ukiniita hivyo
(Wanacheka wanashikana mkono
kisha wanatoka nje tayari kwa ajili ya kutalii mji mkongwe na wa kihistoria mji
wa Zanzibar)
Liliana:
natamani iwe hivi siku zote
Robert:
na itakuwa
Liliana:
nataka kumnunulia zawadi mama
Robert:
oh, gift for the beautiful mama
Liliana:
(anacheka) yeah
(Wanaendelea kufurahia maisha)
0 Comments