SCENE 37: -
BAADA YA SIKU TATU: -
NYUMBANI KWA BIANCA: -
(Jioni ya siku ya jumapili honi
inasikika nyumbani kwa Bianca na haraka mlinzi anafungua geti. Gari la Robert
linainga nyumbani hapo.)
Liliana:
(kwa mlinzi) shikamoo Lupemba
Lupemba:
marahaba malikia umerudi?
Liliana:
nimerudi…
Lupemba:
za Zanzibar
Lilian:
salama
Lupemba:
pamekupenda kweli umenawili sana
Liliana:
(anatabasamu)
Robert:
(kwa Lupemba) habari yako…
Lupemba:
nzuri bwana shemeji…karibuni sana
Robert:
asante sana (anaendesha gari mpaka eneo
la maegesho)
Liliana:
(anataka kushuka)
Robert:
you are the queen acha nikufungulie
Liliana:
ah thank you so much jamani
Robert:
(anashuka anamfungulia mlango wa gari)
Liliana:
(anashuka huku anatabasamu) shukrani
daddy (anamuongoza njia kuelekea ndani)
(Bianca amekaa na Bella, Anna
pamoja na baba yao yaani mjomba wake Liliana)
Bianca:
(anamuona mwanae) jamani dear hupokei
simu zangu wewe
Liliana:
iam so sorry mama (anamuendea na
kumkumbatia)
Bianca:
(ananyanyuka na kumkumbatia pia)
Liliana:
shikamoo mama
Bianca:
marahaba shoga yangu na bora umekuja (anamuangalia
Robert) mkwe habari yako
Robert:
nzuri mama… (kwa wote) habari zenu
(Wanaitikia)
Liliana:
(kwa mjomba) shikamoo mjomba
Mjomba:
marahaba mama za Zanzibar
Liliana:
nzuri
Mjomba:
karibu
(Wafanyakazi wanachukua mizigo ya
Liliana na kuingiza ndani)
Bianca:
(kwa Robert) karibu uketi baba
Robert:
no sikai mama…
Bianca:
jamani… sawa kama umeamua hivyo
Robert:
nitakuja siku nyingine sasa hivi nasubiriwa ofisini
Bianca:
usijali… (kwa Liliana) haya mtoe
mwenzio uje unipe ya Zanzibar
Liliana:
(anacheka) haya mama (anamuongoza
njia Robert kuelekea nje)
(Wakiwa nje)
Liliana:
oh, daddy nilitaka nikae na wewe tena
Robert:
tutaonana jioni basi
Liliana:
haya
Robert:
ila una mama mrembo sana…hivi hana mtu? Samahani kwa kukuuliza
Liliana:
No daddy its okay…na pia mama hana mtu ingawa hata mjomba huwa anampenda
Robert:
sasa mjomba na mama yako watapendana vipi?
Liliana:
hivi sijakuambia ee ila mmoja wao hapo hatuna undugu wa damu kwahiyo sio mbaya
wao kupendana
Robert:
mama yako mpole sana mstaarabu sana yaani ni mwanamke ambae anafaa kwakweli
Liliana:
daddy umeanza sasa mi naona wivu
Robert:
ah nasema tu nampa sifa zake jamani kwani vibaya?
Liliana:
hata hivyo nakutania bwana
Robert:
najua
Liliana:
haya wewe nenda nina mambo mengi sana ya kumwambia mama
Robert:
really? (anacheka)
Liliana:
yes, daddy
(Wanabusiana)
Robert:
baadae
Liliana:
see you baby
Robert:
(anapanda gari lake na kuondoka zake)
Liliana:
(anarudi ndani)
Anna:
enhe binamu tuambie sasa
Bella:
umependeza shogaaa uende ukaishi huko
Liliana:
tutaenda kuishi na daddy baada ya harusi
Bianca:
(anashangaa) Oh My God jamani
unaolewa?
Liliana:
ameniambia soon (anatabasamu)
Anna:
all the best cuzo
Liliana:
(anacheka huku anajitupa sofa karibu na
alipokaa mjomba wako)
Anna:
wewe mambo yameshaiva nini…Robert hataki ujinga asije akakosa chombo bureeee
Bella:
umeona ee
Liliana:
(kwa mjomba wake) mjomba unaonaje hii?
Mjomba:
kama inakupa Amani basi na mimi nina Amani lakini
Liliana:
nini mjomba?
Bianca:
hivi mtamuweza huyu ana mambo mengi kichwani wala hakuna uwalakini hapo
Liliana:
(anacheka)
Anna:
nina furahi sana kama binamu yangu una Amani
Liliana:
Robert is best man that I have always waited for
Bianca:
I bless you child
Liliana:
amen mama
Bianca:
jamani (kwa wote) mimi nina njaa kama
bado mnamshangaa aliyetoka Zanzibar pambaneni mtashinda (ananyanyuka na kuelekea eneo la chakula) na Siwema nae sijui kapata
danga gani hayupo
(Wanacheka)
Siwema:
aunt lakini mbona unapenda kunisingizia? (anamuona
Liliana) wow jamani Liliana za huko
Bianca:
ulikuwa umemkumbuka?
Siwema:
saaaana mweee
Bianca:
(anafyonza kisha anawageukia wengine) embu
njooni tule jamani achaneni na Siwema ana matatizo
(Wanacheka huku wananyanyuka
kuungana na Bianca kwa ajili ya chakula)
Bianca:
(kwa Liliana) umekuwa mrembo kweli
binti yangu
Liliana:
(huku anakaa) asante mama
(Wanaanza kula huku wanazungumza
masuala mbalimbali)
0 Comments