SCENE 38: -
NYUMBANI KWA BIANCA: -
(Bianca anatoka ndani kwake huku
anaongea na simu)
Bianca:
(kwa Lupemba) Liliana yupo wapi?
Lupemba:
yupo bustanini
Bianca:
sawa (anaendelea kuogea na simu huku anaelekea
bustanini alipo Liliana)
Liliana:
(amekaa kwa utulivu huku anakunywa
maziwa)
Bianca:
(anamfikia) hi baby
Liliana:
Hi mama
Bianca:
mbona umekaa huku peke yako?
Liliana:
(anamuegemea mama yake begani) hapana
mama nimeamua tu kukaa huku
Bianca:
any problem dear?
Liliana:
No mama, nipo sawa kabisa mama yangu
Bianca:
umeamua tu kukaa peke yako?
Liliana:
ndio mama
Bianca:
au umegombana na mkwe
Liliana:
hapana mama tupo vizuri sana
Bianca:
tunatakiwa kuandaa shera si umesema mtafunga ndoa hivi karibuni?
Liliana:
yes, mama (anafurahi sana) yaani mama
nampenda Robert na ananipenda pia
Bianca:
nimekuwa naota kukuona ukiwa na furaha na ninaitamani siku hiyo mwanangu…yes Robert
anaonekana ni mtu mzuri sana
Liliana:
halafu anakufurahia kweli ananiambia kuwa wewe ni mpole sana na una sifa nzuri
Bianca:
oh mama…mwambie nashukuru sana hata mimi namfurahia sana kama anaweza akakupa
Amani na furaha niliyokuwa natamani niione ukipewa na mwanaume
Liliana:
mama usijalli daddy ananipa vyote hivyo and he bought me a car
Bianca:
(anashangaa huku anaweka mikono mdomoni) a
Car?
Liliana:
yes
Bianca:
girl that is your husband
Liliana:
I know mama
Bianca:
iam so proud of him mwambie nimesema asante sana
Liliana:
nitamwambia
Bianca:
shoga sasa una magari mawili nigawie moja basi
Liliana:
nitakupa lile la zamani
(Wanacheka)
Bianca:
nakutania
Liliana:
najua unanitania maana unayo ya kutosha
(Wanacheka)
Bianca:
ah Liliana asante kwa kuja maishani mwanangu ona sasa nina shoga wa kupiga nae
umbea
Liliana:
mimi ndo niseme asante mama
Bianca:
basi tuambiane
Liliana:
hapo ndo sawa sasa
(Wanacheka)
Liliana:
(Anakunywa maziwa kidogo) mama
Bianca:
nambie mwanangu
Liliana:
ungemkubalia mjomba tu tucheze harusi
Bianca:
amekutuma?
(Wanacheka)
Liliana:
hapana mama ila nahisi ni jambo zuri kumkubalia tu mfunge ndoa tucheze weeee
mpaka basi
Bianca:
kwani sijamkubalia?
Liliana:
(anashangaa) umemkubalia lini?
Bianca:
nakutania mwaya
Liliana:
mkubalie bwana maana wote hamna wenza mngekuwa tu bwana mke na mume, mjomba
wangu ni mchapakazi
Bianca:
alikuwa anakubaka
Liliana:
(anamuangalia mama yake) mama hayo ni
ya kale
Bianca:
siwezi kuyasahau
Liliana:
nimeamua kumsamehe mama na nimeona nguvu ya msamaha nina Amani sina kinyongo
moyo wangu hauumi kama ningeamua kukibeba kitu hicho
Bianca:
(anakaa kimya)
Liliana:
mama msamehe tu na uendelee na maisha kama hicho ndo kitu pekee kinachokufanya
usimkubalie
Bianca:
(anaguna) mtoto una maneno wewe
Liliana:
(anacheka)
Bianca:
au amekutuma?
Liliana:
hapana
Bianca:
ubaya siku hizi haongelei
Liliana:
(anacheka) anaongelea sana tu mbona
yaani kila tukikutana labda kwa chakula au tu stori huwa anakuambia
ungemkubalia
Bianca:
nina miaka 61 tayari nimeshazeeka
Liliana:
mama love doesn’t know age boundaries
Bianca:
na pia mjomba wako ni mdogo kwangu
Liliana:
hamuonyeshi halafu age is just a number mama
Bianca:
sawa ila
Liliana:
usijinyime raha mama na furaha yako ipo njiani unaiona
Bianca:
(anakaa kimya)
Liliana:
nakwambia mama mpe nafasi mjomba mtakuwa wapendanao wazuri sana
Bianca:
(anaguna)
Liliana:
usijizue mama
Bianca:
okay nitachukua ushauri wako
Liliana:
(anafurahi sana) hayo ndo maneno
mama… age is just a number
Bianca:
mpaka aseme yeye
Liliana:
atasema tu
Bianca:
(anacheka) na wewe unajua kupangaa
maneno
Liliaana:
mimi nitafurahi sana nikisikia harusi yako na mjomba
Bianca:
kama itakupendeza basi sawa mama
Liliana:
(anafurahia sana)
Bianca:
muone… (anamshika bega) usisahau
kufurahi hivi mwanangu hata kama ukiwa unapitia magumu gani wewe jua tu Mungu
yupo na anatupigania kazi yetu sisi ni kukaa kwa utulivu tukimtegemea yeye
Liliana:
yes, mama
Bianca:
keep on smiling my daughter
(Wanakumbatiana)
Liliana: oh mama (anamkumbatia)
0 Comments