SCENE 39: -
CHUONI KWA KINA LILIANA: -
(Liliana anashuka kwneye gari
lake jipya alilonunuliwa na mpenzi wake, anatumia funguo kufunga gari kisha kwa
mwendo wa kujidai anatembea kuelekea darasani)
Liliana:
(anapiga hatua chache)
Sauti:
(kutokea nyuma yake) Liliana?
Liliana:
(anageuka) oh Gervas
Gervas:
naam umepotea sana na siku hizi huonekani kabisa
Liliana:
mbona mimi nipo jamani?
Gervas:
(anamfikia) I miss you (anataka kumkumbatia)
Liliana:
(anasogea nyuma kama kukwepa Fulani hivi)
Gervas:
lakini kwanini hunitaki Liliana?
Liliana:
kwasababu nina mpenzi
Gervas:
mpenzi yule anayelingana na baba yako au babu kabisa
Liliana:
it doesn’t matter nampenda hivyohivyo age is just a number
Gervas:
yule ni mume wa mtu
Liliana:
yes, alikuwa ameoa ila mke na watoto wake wote wameshatangulia mbele za haki
Gervas:
(anasikitika) siku moja utakuja
kukumbuka maneno yangu ungekuwa na akili ungemfuatilia mapema huyo mwanaume...
Liliana:
Gervas please kama humpendi Robert endelea kumchukia kimya kimya sio kuanza
kusema unayoyasema
Gervas:
wake up ni wewe tu ndo umelala kila mtu anaona kwa macho lengo lake ni
kukuchezea
Liliana:
nimekuambia acha
Gervas:
nakupenda sana Liliana nitaumia sana nikisikia umeharibikiwa
Liliana:
kuharibikiwa na nini? Kwani ni kosa kupenda?
Gervas:
hapana sio kosa Liliana ila kosa ni kupenda sehemu ambayo sio sahihi
Liliana:
na kwa Robert sio sehemu sahihi?
Gervas:
kabisa
Liliana:
nitavunga sijakusikia Gervas ila ukirudia nitasahau kwamba tuliwahi kuwa
marafiki
Gervas:
(anasikitika)
Liliana:
sasa unasikitika nini?
Gervas:
nakusikitikia wewe Liliana ambae kwa sababu ambazo sizijui unakataa kukubali
ukweli juu ya hawara yako
Liliana:
sio hawara yangu ni mpenzi wangu
Gervas:
ni mume wa mtu yule
Liliana:
unataka nini Gervas embu niambie mbona unapenda kuniumiza
Gervas:
sikuumizi
Liliana:
au kwasababu nilikukataa?
Gervas:
hapana hiyo sio sababu nimekuwa nikikupenda kwa miaka sasa tangu hata bado
hatujaanza chuo
Liliana:
kwahiyo?
Gervas:
nakutakia mema tu Liliana siku moja utayakumbuka maneno yangu
Liliana:
niyakumbuke kwa lipi?
Gervas:
yaishe
Liliana:
please leave me alone jamani sitaki shida mimi na wewe na wala mtu yoyote
nicheni niishi maisha yangu kwa Amani
Gervas:
sijakugusa na wala sina mpango wa kukugusa nakushauri kama rafiki
Liliana:
kama utaendelea kuniambia hivyo basi sitakuwa rafiki yako navunja urafiki na
wewe
Gervas:
sijui una nini? Umekuwaje Liliana mbona ulikuwa mtu mzuri sana huyo mwanaume
amekufanya nini mbona kama umekuwa mjinga?
Liliana:
umeanza kuniita mjinga?
Gervas:
ona sasa yaani umekuwa sio muelewa
Liliana:
ndo nimekuwa hivyo sasa embu niache sasa
Gervas:
aisee
Liliana:
excuse me
Gervas:
Liliana nisamehe kama kuna sehemu nimekosea
Liliana:
hujanikosea mimi umemkosea mpenzi wangu…mume wangu mtarajiwa
Gervas:
mumeo mtarajiwa?
Liliana:
ndio hujapenda?
Gervas:
imenishangaza kidogo
Liliana:
ndo hivyo…now if you don’t mind iam going to my class
Gervas:
sawa masomo mema
Liliana:
(anaondoka)
Gervas:
(anabaki amebutwaa) mume mtarajiwa?
0 Comments