SCENE 40: -
BAADA YA MWEZI MMOJA: -
NYUMBANI KWA BIANCA: -
(Majira ya saa nane mchana, jua
linawaka kweli kweli na kwasababu hiyo watu mbali mbali wanapata vinywaji vya
baridi kuyapa ahueni makoo yao yaliyokauka kwa sababu ya joto kali. Bianca yupo
nyumbani kwake nae kama ilivyo kwa watu wengine nae anapata kinywaji chake cha
baridi, wakati anaendelea kupata kinywaji chake Robert anafika mahali hapo)
Bianca:
(anamuona) oh mkwe
Robert:
(anatabasamu) habari yako mrembo?
Bianca:
(anashangaa kidogo)
Robert:
mbona unashangaa?
Bianca:
Liliana hayupo
Robert:
sijaja kumuona yeye nimekuja kukuona wewe
Bianca:
kama umekuja kuongelea mahari umeshawahi kuoa na unajua taratibu
Robert:
sijaja kwa ajili hiyo mrembo nimekuja kwa ajili yako
Bianca:
(kwa mshangao) yangu?
Robert:
yes, yako kwani vibaya
Bianca:
sio vibaya ila inashangaza halafu acha kuniita mrembo
Robert:
(anakaa) nakupenda sana Bianca
Bianca:
(kwa ukali) wewe shika adabu yako
Robert:
najua hata wewe unanipenda naonaga unavyoniangalia nikija hapa nyumbani
Bianca:
wewe ni mpuuzi sana
Robert:
tukana unavyoweza nimeshakuambia ninakupenda na ninataka kukuoa wewe na sio
Liliana sijui hata unanielewa
Bianca:
ni kwa bahati mbaya sana mwanangu anakupenda sana
Robert:
mrembo acha kumuongelea Liliana tuoane mpenzi nitaondoka na wewe tutaenda mbali
Bianca:
nina mwanaume tunatarajia kuoana lakini pili Liliana anakupenda na wala sipo
tayari kuharibu uhusiano wangu na Liliana now get out now
Robert:
unaolewa?
Bianca:
ndio
Robert:
utaolewa na mimi tu na sio na mtu mwingine
Bianca:
you are crazy
Robert:
yes, very crazy about you my love nipe nafasi mpenzi
Bianca:
get out now
Robert:
usiolewe Bianca
Bianca:
naomba uniache tafadhali (anaita)
Lupemba, Mbise
(Wanakuja)
Bianca:
naomba mumuondoe huyu mwanaume humu ndani mara moja
Mbise:
sawa aunt
Robert:
msihangaike naondoka mwenyewe ila hatujamalizana (anaondoka)
Lupemba:
Aunt kuna shida gani?
Bianca:
(amekasirika sana) huyu mwanamume ni
mtu wa ajabu sana
Lupemba:
amefanya nini?
Bianca:
naomba msimwambie Liliana tafadhali
Mbise:
hatutamwambia
Bianca:
amenitongoza ananiambia anataka kunioa
(Wanashangaa)
Lupemba:
kumbe ni mtu mbaya ee
Bianca:
sana
Mbise:
maskini halafu Liliana anavyompenda
Bianca:
simtaki tena maishani mwangu huyu mwanaume asije tena hapa
Lupemba:
ni mpenzi wa Liliana na atakuja tu kwasababu ya mapenzi yao
Bianca:
nitatafuta njia ya kumkataza Liliana
Liliana:
(anafika mahali hapo)
Bianca:
(anatulia) Mbise, Lupemba kaendeleeni
na kazi zenu
Liliana:
(anawakaribia)
Mbise:
sawa aunt
lupemba:
(anaongoza njia)
Mbise
(bado amesimama hapo)
Liliana:
(anakaa pembeni ya mama yake)
Bianca:
(anatulia) Mbise, nimesema
kaendeleeni na kazi zenu
(wanaondoka)
Liliana:
vipi za hapa mama…shikamoo mama
Bianca:
(anamkumbatia) marahaba mwanangu
Liliana:
mama kuna jambo nataka kukuambia
Bianca:
nini tena?
Liliana:
mama iam pregnant…
Bianca:
(anashangaa)what?
Liliana:
yes, mama…iam pregnant
Bianca:
Liliana kwanini umekuwa ni mjinga kiasi hicho
Liliana:
(anashangaa) mama?
Bianca:
Robert sio mwanaume mzuri
Liliana:
mama Robert ananipenda sana na ni yeye ndo aliniambia anataka familia nyingine
baada ya familia yake wote kufariki kwenye ajali mbaya
Bianca:
im so disappointed with you Liliana haki ya Mungu sikutegemea hili
Liliana:
mbona sikuelewi, mbona ulikuwa unafurahia?
Bianca:
sitaki sasa… nimebadili mawazo
Liliana:
mama
Bianca:
(anatulia) haya mwambie kuwa una
mimba
Liliana:
(anamshangaa)
Bianca:
iam sorry dear kuna mtu amenichanganya sasa hivi
Liliana:
pole mama…naomba ufurahi maana unaenda kupata mjukuu
Bianca:
asante mwanangu kwa habari hii
Liliana:
okay mama najua Robert atafurahi sana akisikia hii habari
Bianca:
asante haya kapumzike
Liliana:
(anambusu mama yake shavuni kisha
anaingia chumbani kwake)
Bianca: my child, umefanya nini
mama…kumbebea mimba mwanamume mjinga kama Robert umefanya ujinga mkubwa sana
mama hata sijui kwanini umefanya hivyo mama lakini ni kwasababu hujui mama ila
najua utajua tu…(anakaa) utajua tu
…kwamba huyu mwanaume ni BAD NEWS atatusababishia makubwa maana anataka
kutugombanisha mwanangu na sitaruhusu hata kwa nini wewe ni mwanangu na utabaki
kuwa kipenzi changu
0 Comments