SCENE 41: -
NYUMBANI KWA ROBERT: -
(Liliana anafika nyumbani kwa Robert
akiwa na furaha kubwa sana na yupo tayari kusema habari njema)
Liliana:
(huku anaingia ndani) daddy
Robert:
(hamfurahia) Robert
Liliana:
(anashangaa)
Robert:
sema shida yako maana sina muda mchafu wa kuona sura yako
Liliana:
daddy jamani hayo matani yako siyataki
Robert:
talk woman
Liliana:
(anashangaa) jamani
Robert:
(anakaa kimya)
Liliana:
anyway, daddy nimekuja kukuambia kuwa nina ujauzito wako
Robert:
nani amekuambia nataka mtoto
Liliana:
(anashangaa) daddy ulisema kuwa
unataka mtoto unataka familia mpya
Robert:
nina familia mama…nina mke na watoto wanaishi Canada
Liliana:
(anajikuta anaishiwa nguvu)
Robert:
wewe ni takataka mbele ya mke wangu
Liliana:
(anatokwa machozi) Robert
ulinidanganya kuwa huna mke na watoto
Robert:
akili tu niliitumia kukupata nilikubaka utotoni…siku ile usiku sijui ulikuwa
unatoka wapi...ulinivutia sana kwahiyo nilitaka nikutumie tena ungekubali vipi kama
ningekuambia kuwa nina mke na watoto
Liliana:
(Analia) kumbe ni wewe ndo
ulinifanyia yale utoto kumbe wewe ni yule mlinzi ndo maana sura yako haikuwa
ngeni
Robert:
(anakaa kimya)
Liliana:
nimekusamehe…
Robert:
sitaki unisamehe maana sikupendi nampenda Bianca
Liliana:
mama yangu?
Robert:
ndio…
Liliana:
wewe ni mnyama
Robert:
halafu tamu kuliko…mimi nimeathirika na wewe umeshaathirika…nimeathirika miaka
mingi sana yaani hata mwanangu wa mwisho analingana na wewe nae ni muathirika
Liliana:
(anachanganyikiwa)
Robert:
nakuchukia sana Liliana
Liliana:
nimekukosea nini?
Robert:
hakuna ulichoniudhi…nilikuwa na wewe kisa nilimpenda Bianca sana na wewe ndo
ulikuwa unaniunganisha nae…
Liliana:
(anasikitika) mama anaenda kuolewa na
mjomba
Robert:
hiyo ndoa haitafika nipo radhi niue ila Bianca hataolewa na mtu na nipo radhi
nimuache mke wangu Lydia nimuoe Bianca
Liliana:
unampenda kiasi hicho?
Robert:
nampenda sana
Liliana:
(Analia sana)
Robert:
you disguist me…yaani wewe ni mzuri tu ila hufai kuwa mke unafaa kuchezewa na
kutupwa kama takataka
Liliana:
aisee sikutegemea kusikia haya leo
Robert:
ndo umesikia pasuka sasa
Liliana:
it is not worthy it
Robert:
ndo nimekuambia halafu huwezi amini nimesikia Amani ya ajabu nilipokuambia
ukweli… (anamuonyesha picha za familia
yake) huyu ni Gabriel, Michael na Raphael na mke wangu mpenzi Lydia
wanaishi Canada huwa wanakuja mara kwa mara na ndo maana saa nyingine sitaki
kuonana na wewe
Liliana:
hongera sana
Robert:
asante nakwambia haya ili huyo mtoto utafute njia ya kumtoa huyo mtoto
Liliana:
subiri azaliwe umuue mwenyewe sipo tayari kubeba hii dhambi
Robert:
utaitoa hiyo mimba hutoi?
Liliana:
(anamkazia macho) simtoi…
Robert:
hunijui
Liliana:
utanifanya nini?
Robert:
maskini nakuonea huruma umeshalia sana…ulikuwa unanipenda ee
Liliana:
(Analia sana)
Robert:
get out mke wangu atakuja muda sio mrefu akiondoka tu nakuja kwa Bianca wangu
ni laizma nimuoe hata awe mke wa pili
Liliana:
(anaondoka huku Analia sana)
Robert: (anacheka kwa dharau) mimi ndo Robert
0 Comments